Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,226
Maximo adaiwa hana uwezo zaidi ya hatua aliyoifikisha Taifa Stars
MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Hussein Sappi amesema tukubali ukomo wa kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na staili ya soka anayofundisha timu haiwezi kufika mbali.
Akizungumza katika kipindi cha Kumepambuzuka cha Radio One jana, Sapi alisema makocha wa Brazil wengi hawana rekodi katika ulimwengu wa soka zaidi ya nchi yao.
Alisema Brazil wazuri kwa wao wenyewe lakini hawana rekodi nzuri duniani.
"Mimi nadhani wakati umefika sasa tubadilike, tuangalie Ulaya Mashariki, kule tunaweza kupata makocha wazuri na hata soka yao inajulikana.
"Tunakubali kuwa Brazil wana makocha wazuri lakini kwa faida yao, wapi kuna mafanikio kwa kocha wa Brazil? Tunaona Afrika Kusini inavyoyumba.
"Kulikuwa na Felipe Scolari, alikuwa Ureno, hakuna kitu, kaondoka akaenda Afrika Kusini, akatoka akaja Chelsea, na sasa hayupo, kuna nini pale. Angalia makocha wa Hispania, Ufaransa, Uholanzi, Russia, Jamhuri ya Czech wapo na naamini tunawamudu...," alisema.
Akizungumza huku akionyesha kukerwa, alisema: "Isije kufika wakati tukapigana mawe Uwanja wa Taifa pale, mimi hili nalisema kama Mtanzania mwenye haki ya kuzungumza langu na sidhani kama Maximo anatufaa tena," alisema.
Chanzo: Mwananchi
Huyo hana shukrani hata kwa Rais aliyemwajiri kocha huyo. Aende akafundishe yeye Taifa Stars tuone ataifikisha wapi. Wabongo tumezidi sana longo longo mara ooh! Kesho utasikia Oooh! Mfumo wa soka la sasa hivi unaweza kulilinganisha na enzi za akina Ndolanga au Rage? Inatubidi tukabiliane na changamoto jamani. Uingereza inasifika kwa kupenda soka duniani mbona wameajiri kocha wa nje? Ina maana hakuna makocha wa ndani wenye sifa na ujuzi? Mimi nadhani bwana Sappi angekuwa more analytical "yakinifu" kuhusu anachokizungumza kwa kuweka data na sio kupiga domo.
Jamani jamani, hivi hamuoni kwamba Maximo ni failure????. nashangaa sana wachangiaji humu wanavyosema ati hatuna shukurani kwa alipotufikisha Maximo. katufikisha wapi????, Hivi wewe ikiwa safari yako ni ya kufika Dodoma na ukanunua vyote vinavyoweza kukufukisha Dodoma, na mwishowe ukaishia Chalinze hata morogoro hujafika utajisifia kufika chalinze tena kwa wiki mbili badala ya masaa tu?
nasema hivyo ajili Maximo kapewa kila alichotaka na hata zaidi kutoka kwa TFF na wadhamini na wadau wengine lakini mafanikio ni 20% ya alichostahili kufanikisha je tumsifu, hivi do we need 20% of performance from him kwa support anayopata?. Mfano mdogo tu kama mtakumbuka enzi za Serengeti boys na Kibadeni wakitembeza bakuli kupitia ITV na matokea yalionekana kwa muda mfupi tu, sasa hivi tunawachezaji maarufu waliotokana na serengeti boys na hata maximo anawatumia baadhi. Hakika sijaona kikubwa alichofanya Maximo.
Wabongo tunajua kubwabwaja tuuu huyu Sappi na wenzake wote mfano wake wazushi tuuuu. Maximo kwa uwezo wake amejitahisi sana na hata hapa tulipofika sasa nafikiri anahitaji pongezi sana.
uwezo wa maximo ni mdogo sana, we kocha gani miaka miwili hana first eleven wala formation hana. jamaa ana support kubwa sana lakini ndio uwezo wake umefikia kikoma. mafanikio tunayoyapata ni sababu ya juhudi binafsi za wachezaji.
Amekataa kumwita Kaseja ambaye i believe ni TZ 1.
Alimwita Mrisho Ngassa kwa kulazimishwa sana
Amewakataa Mwakingwe akamng'ang'ania Mapunda ambaye alitu-cost sana.
Halafu Brazilian hawana records za mafanikio Africa, wape Wafaransa, Germany,Soviets n Africans
MMSIMKUBALI KABISA HUYO MAXIMO
Akhsante Waungwana Marcio Maximo, hana tatizo ktk idara Zote MuhimuUdhamini Pesa Malazi Vitendea Kazi Ungwaji Mkono nk. Lakini ikubalike katlka historia(kama itakuwa ina nafasi hapa)na takwimu Makocha Wa Kibrazil hawana Rekodi nzuri katika medani ya soka afrika Mpaka Napochangia kumbukumbu zinaonyesha Mbrazil pekee Mwenye Mafanikio Ni Jose Faria(Baadae aliitwa Jaffar Faria) Mwalimu Wa Lion of Atlas Morroco Mwaka 1985-1988 mafanikio yake ni kuifikisha Hatua ya pili Morrocco katika fainali Za Kombe la Dunia 1986 Mexico Hakuna Zaidi Ya huyo Alieishia kutupiwa Virago kwa Aibu baada ya kutolewa katika Nusu Fainali Ya CAN 1988 Na Cameroun Huku Morroco wakiwa Wenyeji.Makocha Waliopita Hapa Tanzania Kutoka Brazil Ni Moreira"Wonder"Foreirra(Yanga)Mafanikio 0 Clouves Oleveira(Taifa Stars) 0 Sijui Mpaka Sasa Nader do Santos(Simba SC Azam FC) Na Nilsein(Simba SC)
,,,Mmh lakini wazee hata mimi huwa najiuliza sana,hivi wachezaji wetu wa Tanzania,mbona hizi skills za kawaida tu za ki futball,Controlling,Driballing hatuzioni kwa wachezaji wetu,yaani mchezaji wa STARS akipewa mpira utafikiria kapewa KAA LA MOTO,ni haraka sana kwa mwenzake au kuutoa nje,na hili ndo linatufanya kila siku kwa tunaoungalia mpira tujione kama hatujui hivi,Kwanini kocha MAX,na kukaa kooote huku na timu hii,Hawezi kuwapa wachezaji wake KUJIAMINI,hiki nikitu hata mimi na wasiwasi nacho,Ndio RESULTS ina matter,lakini tunataka wachezaji wetu wajisikie hutu kidogo,pewa pasi,tuliza,vuta moja mbili,geuka huku,maguu mawili matatu kama ya RONALDO,then release mpira.