Kirikou Wa Kwanza
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 3,564
- 1,991
Jamaa kaenda kwa mganga wa kienyeji, alipofika tu mganga akamwambia, "Wewe una matatizo na mkeo." Jamaa akajibu, "Yaa ni kweli mtaalamu umejuaje?" Mganga akajibu, "Mimi nimejua tangu huko ulipotoka. Sasa ili kuokoa ndoa yako isivunjike, kesho njoo Tsh milioni 2 mkononi, njoo na majogoo wawili wekundu, unga kg 5, mafuta ya kula dumu 1, vitunguu, nyanya, ndimu, pilipili, chumvi, karoti na hoho. Lakini pia usisahau simenti mifuko 3, bati 2 na misumari...kuna kakibanda kangu nataka kukamalizia hapo nje tehe tehe tehe!"