Sanamu ya Nebukadneza na 'Watanzania Masalia'! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sanamu ya Nebukadneza na 'Watanzania Masalia'!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Nov 4, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]
  Lula wa Ndali-Mwananzela​
  [​IMG]
  MOJA ya visa vya kusisimua katika masimulizi ya kale ya Kibiblia ni kile cha marafiki wa tatu wa Nabii Daniel waliokutwa na kile ambacho tunaweza kukiita kuwa ni "kisongombingo" cha Mfalme Nebukadneza wa Wababeli aliyetawala kama miaka 600 hivi kabla ya Kristo.
  Wengine wanaweza kuita kisanga kile kuwa ni “kasheshe” la karne. Tunawafahamu marafiki hao kwa majina ya Shedraki, Meshaki, na Abednego.
  Unaweza kusoma kisa chenyewe kwenye kitabu cha Daniel sura ya tatu. Mimi hata hivyo ninaangalia siasa za simulizi hilo na kuona mfanano wa ajabu kati yake na kile kinachoendelea katika taifa letu Tanzania leo hii; hususan katika ulingo wa siasa.
  Kisa hiki kinaanza pale ambapo Mfalme Nebukadneza alipoamua kusimamisha sanamu ya dhahabu yenye urefu wa kama mita 27 hivi (dhiraa sitini) ili watu wake waiabudu. Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa dhahabu ya thamani ilipokamilika aliisimamisha kama “mungu” wa wababeli hao.
  Na kisha ukatumwa ujumbe katika pande mbalimbali za Babeli na mataifa yaliyokuwa chini ya ufalme huo kuwa watu waje kuiabudu sanamu ya Nebukadneza.
  Na kwa maelfu yao walikusanyika mbele ya sanamu hiyo na ikatolewa amri kuwa watu watakaposikia sauti ya tarumbeta basi wote waanguke mbele ya sanamu hiyo na kuiabudu; vinginevyo watawekwa kwenye tanuru ya moto.
  Tunasimuliwa kuwa: “Basi maliwali, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wa jimbo walikusanyika kwa ajili ya kuizindua sanamu ile ambayo mfalme alikuwa ameisimamisha. Nao wakasimama mbele ya hiyo sanamu.”
  Kwa maneno mengine ni kuwa yeyote aliyekuwa “mtu kati ya watu” alikuwepo kwenye uzinduzi wa sanamu hiyo.
  Tunachoambiwa ni kuwa wanasiasa na watawala na wasomi wa wakati ule wote walikuwepo kwenye uzinduzi wa sanamu hiyo na pale panda ilipopigwa tunasimuliwa kuwa “watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha wakaanguka chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.”
  Hapa tunachodokezwa ni kuwa maprofesa, madaktari, wanafizikia, wafanyabiashara wakubwa, n.k wote walianguka mbele ya sanamu hiyo ya Nebukadneza.
  Hawa wote walifanya hivyo kwa sababu waliamini kabisa kuwa maisha yao na mafanikio yao yamo mikononi mwa Mfalme Nebukadneza. Maelfu hawa wa watu kila ulipofika uchaguzi walijikuta hawana jinsi isipokuwa kuendelea kuchagua utawala wa Nebukadneza na kutokana na ukweli huo walipoitwa kuipigia magoti sanamu yake walijua hawana uchaguzi.
  Walijua utawala wa Nebukadneza ulikuwa na ufisadi wa kila namna, lakini pia ndio uliowafanya waishi wakijisikia wako na “amani, utulivu, na mshikamano”.
  Kilichowatisha ni moto
  Watu hawa wote walipiga magoti mbele ya sanamu hii baada ya kusikia tarumbeta kwa sababu tangazo lilisema kuwa “mtu ye yote ambaye hataanguka chini na kuiabudu sanamu hiyo atatupwa saa hiyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto.’’
  Watu walijua kuwa wakifanya uamuzi kinyume na hilo agizo la mfalme, basi watakiona kile wahenga walikiita cha “mtema kuni”; yaani kutupwa kwenye tanuru la moto ambalo bila ya shaka lilitumika kufulia dhahabu ile.
  Ukitupwa kwenye tanuru hiyo hakuna kupona. Hivyo watu wote waliojua ukweli huo na wengine labda wakijua pia kuwa sanamu ile “si lolote wala chochote” walijikuta wanaanguka kifudifudi ili kusalimisha maisha yao na ya watoto wao.
  Kwa maneno mengine, waliuza utu wao na haki yao ya kuwa huru kwa sababu ya kumuogoa Mfalme Nabukadneza. Isipokuwa vijana watatu.
  Vijana wale watoto walijua kuwa hawawezi kuiabudia sanamu hata kama imetengenezwa kwa thamani kubwa na inasimama kama “jitu la dhahabu”. Walifahamu kuwa imani yao (ya Kiyahudi) inawakataza kuabudu sanamu ya aina yoyote.
  Hawa walijua kuwa uchaguzi wao ulikuwa ni rahisi kweli. Kwamba kama ukiabudu sanamu hiyo utakuwa na mafanikio, usalama, maisha mazuri na kutengemaa kwa kila namna.
  Walijua pia kuwa kutoabudu sanamu hiyo na kukana imani na dhamira yao kunamaanisha kifo. Walijua gharama ya kutokuiabudu sanamu.
  Walikuwa ni masalia ya wale wenye kuamini katika “Mungu mmoja” na ambao wanajua kuwa hana mshirika na wala hashirikishwi na kitu chochote au kiumbe chochote. Walijua kuwa Mungu hana mbia mwingine yoyote, na hivyo walikuwa tayari kuingia kwenye tanuru ya moto kuliko kukana imani yao hiyo.
  Vijana Meshaki, Shedraki na Abednego (majina yao ya Kibabeli) walishitakiwa kwa kutopigia magoti sanamu na mwisho wake wakutupwa kwenye tanuru la moto. Hawakujua kama wataokolewa lakini walikuwa tayari wamejisalimisha kwa Mungu wao kuwa ni heri kufa kuliko kupigia sanamu magoti. Tunaambiwa waliokolewa na yule “mtu wanne” ndani ya tanuru ile.
  Sanamu yetu ya leo ni CCM!
  Katika taifa letu hili tumesimamishiwa sanamu kubwa iliyotengenezwa kwa thamani nyingi sana nayo yaitwa CCM. Sanamu hii tunaambiwa na watawala wetu kuwa ndiyo njia pekee ya uhakika ya watu wetu kufanikiwa. Watu wetu leo hii wanaamini kabisa kuwa pasipo “CCM” hawawezi kuishi kwa mafanikio na pasipo kujisalimisha kwake basi maisha yatakuwa magumu na mipango ya mafanikio itakoma.
  Hivyo tunakuta makundi ya wasomi wetu mbalimbali, wafanyabiashara, wanataaluma na watu ambao wanaonekana kuwa na upeo mkubwa wa kimtazamo wakipiga magoti mbele ya chama hiki.
  Wapo majaji, wakuu wa majeshi, polisi, magereza, wasomi kwenye vyuo vyetu na hata wananchi wa kawaida ambao wamechagua CCM kwa sababu moja tu; nayo ni kuwa pasipo CCM maisha yao hayawezi kwenda mbali na hawawezi kufanikiwa kiurahisi.
  Hivyo, utaona kuwa hata katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na ufisadi kama Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro n.k wanaichagua CCM kwa wingi zaidi kwa sababu kutoipigia magoti ni kutaka kuingizwa kwenye tanuru ya moto!
  Huko tunakoenda kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani tutawaona watu wengi zaidi wakijitokeza zaidi kujiunga na CCM, na kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho kwa sababu wanajua bila ya hivyo wamekwisha.
  Hata kwenye kikao cha bunge kinachokuja utaona watu wenye akili timamu na wasomi waliobobea wakikitetea chama chao (sanamu) kuwa “ni safi” na kuwa ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja.
  Kama vile waliotukuza dhahabu iliyotengeneza sanamu ya Nebukadneza, vivyo hivyo tutawaona watu wengine wakiitukuza CCM kama vile sanamu ile!
  Pamoja na mgongano tunaouona ndani ya CCM hivi sasa , ukweli ni kuwa hawa wote wanaabudu sanamu ile ile, na hawawezi kufikiria maisha nje ya CCM. Wanahofu kuna tanuru la moto!
  Wanatafutwa Watanzania Masalia!
  Wanatafutwa wananchi wasomi na wasio wasomi, matajiri na wasio matajiri, wenye kitu na wasio na kitu, wazee kwa vijana, kinamama kwa kinababa kuwa kama wale vijana watatu wa zama za Daniel ambao watakuwa tayari kukataa kuipigia magoti sanamu hii iliyosimamishwa katika taifa letu.
  Watu hawa watatakiwa kuwa majasiri ambao wako tayari kulipa gharama kubwa zaidi hata ya maisha yao ili kuiokoa nchi yao.
  Wanaotafutwa ni wale ambao wanajua Tanzania ndiyo iko juu ya chama chochote cha siasa, juu ya itikadi yoyote, sera zozote au mwelekeo wowote wa kisiasa.
  Wanaotafutwa ni watu ambao hawajali majina na hadhi zao, majasiri wasioteteleka, wajuzi wa tunu bora za kale, walinzi wa njozi za kizazi kilichopita! Wanatafutwa tena watu ambao watamkatalia mtawala wetu wa leo kuwa hawako tayari kupiga magoti mbele ya CCM!
  Watu ambao watafuata mfano kama wa Augustine Lyatonga Mrema ambaye amelipa gharama kubwa zaidi ya kisiasa na kimaisha na aliyetupwa kwenye tanuru ya moto na kufikiriwa kuwa ameungua na ameteketea. Mrema ni mmoja wa vigogo wachache wa zamani ambao hadi sasa hawajakubali kurudi na kuipigia sanamu hii magoti ili maisha, afya, na mambo yao yafanikiwe.
  Pengine Mrema ndiye mtu pekee katika historia yetu ambaye alilipa gharama kubwa zaidi katika zama hizi za CCM kwa kukejeliwa, kupuuzwa na kufanywa duni.
  Ni mtu ambaye amekataa kuipigia sanamu hii (CCM) magoti ingawa anajua kabisa kuwa akifanya hivyo mambo yake yatamnyookea; kwani amewaona wenzake waliokuwa pamoja walivyouza dhamira zao, utu wao na hadhi zao ili mambo yao yawanyokee!
  Wanatafutwa ‘Watanzania Masalia’ ndugu zangu! Je wewe ni mmoja wa wanaoendelea kuipigia magoti CCM kwenye sanduku la kura? Je wewe ni mmoja wa wale wanaoamini kabisa kuwa sanamu hii ina uamuzi juu ya maisha na hali yako?
  Kama ndiyo, endelea kufuata imani yako hiyo; kwani wewe ungekuwa mmoja wa wale walioipigia magoti na kuisujudia sanamu ya Mfalme Nebukadneza!
  Tanzania itajengwa na wale waliosalia; ambao ikibidi wataingia kwenye tanuru ya moto kama Augustine Mrema!  Source: Raia Mwema
   
 2. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kaka hii habari nimeisoma kwa masikitiko sana, yaani the interpretation is looking similar na maisha ya mfalme CCM, CCM imejifanya kama chama cha kifalme, nafikiri tunahitaji kutambua wapi tunaenda, maake Tanzania ya leo hata Raisi nae akiamua kutengeza sanamu yake na akaamuru watu waisujudu nafikiri kuna watu hata ndani ya JF watafanya hivo (kama ndugu yangu Kibunango) atapiga magoti yote na kuanza kuililia hiyo sanamu ili isije bomoka. inachekesha sana fikra ya Mtanzania wa leo inavokwenda, tulitegemea kuwa kutokana na Watanzania wengi kwa sasa kupata elimu then kutakuwa na mabadiliko ya kifikra na maono kuhusu Taifa lao na linakokwenda, kumbe tumezidi kuwa watu wasio na mtazamo? we jaribu kufikiriia kikawaida tu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa jinsi hii sanamu CCM walivoshinda, inaashiria vipi hii sanamu ilivowashika watu mashati, ukitaka kujua people are still under total ignorance, utawasikia bwana isingekuwa CCM tusingesoma, tusingekula-----------that is stupidity argument people you find them arguing, they forget kwamba kusoma kwao ni kutokana na kodi ambayo baba yake anatozwa and after all mtu unasoma kwa mkopo, na ili kupata mkopo wenyewe mpaka ugome, na ndugu yangu MBONEA ukitaka kujua we are still far way back, ni pale uchaguzi ukifanyika hiyo sanamu inapata kura nyingi sehemu za vyuo vikuu, imagine sehemu ya wasomi inavosujudu maisha ya leo na sio ya kizazi chake cha baadae.

  Ni hatari sana, we need change na katika hizi changes watu wakubali kuingia kwenye hiyo tanuru.
   
 3. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Absolutely ryt.
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  well said kabuche
   
 5. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mhh! Nchi hii wachache watatumeza kabisa
   
Loading...