Anaandika Sheikh, Dr Yahya Msangi(PHD).
LOME, TOGO.
Ni vyema wenzangu mkaelewa yanayojiri nchi nyingine ili mtafakari kwa makini.
Kumekuwa na harakati za kuandaa maandamano nchi mbalimbali Afrika toka kipite kimbunga cha ARAB SPRING. Kipunga kiklichoanzia Tunisia kikasambaa kwa kasi Misri. Lakini wengi hamjui mlengwa haswa wa kile kimbunga cha facebook na tweeter alikuwa nani. Hakuwa Tunisia wala hakuwa Misri!
Baada ya kumuua Sadam wababe wa kimagharibi walilenga mitutu na makombora yao kwa Algeria, Libya na Syria. Wengi mnajua kuhusu kilichofanywa Libya na sasa Syria. Lakini wengi hamjui kuhusu Algeria.
Algeria ni nchi ya 10 kwa ukubwa duniani (geographically). Nchi kubwa kama hiyo haikosi kuwa na mali asili zinazowatoa mate mafisi makubwa! Lakini pia Algeria imepakana na kina Morocco, Mali, Tunisia, Libya, Niger, Mauritania na Sahara ya Magharibi. Kutokana na hili Algeria inapakazwa kuwa ni mfadhili mkubwa wa vikundi vya kigaidi! Hakuna ushahidi wowote ila hila hii inafanywa ili kupata sababu ya kuivamia na kuivuruga Algeria.
Mfaransa bado hajamsamehe Algeria kwa kiichowakuta enzi ya vita ya ukombozi! Mfaransa bado anayataka mafuta ya Algeria. Mfaransa anaona Algeria ndio inaofadhili wa TOURAG wanaompiga vita kutokana na wizi wa Uranium kaskazini mwa Chad na Mali! Wapiganaji wa kitourag walikuwa wakihifadhiwa na Gadaffi. Watourag wanatetea mali zao na nchi yao iliyotwaliwa kwa mabavu na kampuni ya kifaransa inayochimba uranium! Kuna taarifa zisizo na shaka kuwa umeme woote unaowaka ufaransa unatokana na Uranium inayoibwa Chad na Mali. Mazingira, wanyama na watu wamelemaa kwa athari za uranium mfaransa hajali! Wakubwa wamefumba macho! Mijizi combined! Baada ya Libya kuvamiwa sasa ni Algeria inatafutwa! Ukumbuke Algeria ina utajiri mkubwa wa mafuta! Algiers na Cairo ndio miji pekee Africa in aundergroung transport system ya hadhi ya kimataifa!
Arab spring ililenga Algeria ikaja bahati mbaya akabondwa Tunisia na kipenzi chao Misri! Ndio maana pamoja na arab spring kupamba moto Misri na Tunisia zimekufa kifo cha mende! Waliokuwa nyuma ya Arab Spring walipoona mlengwa kakwepa wakatuliza ngoma! Vijana wa facebook na tweeter wakaumia buree!
Sasa kuna nchi 2 maandamano yanatumika kutaka kuzivuruga. Ni Tanzania na Togo. Kila moja na sababu zake tofauti.
Tuanze na Togo.
Togo ni kanchi kadogo kabisa barani Afrika. Nadhani ni Sao Tome na Principe pekee ndio ndogo kuliko Togo. Wakazi wa Togo ni kama milioni 8 hivi na mji mkuu wa Lome una wakazi takriban milioni moja. Ni mji ambao kwa tuliozoea Dar hauna mikikimikiki kabisa. Togo haina madini isipokuwa ina bandari maarufu toka enzi za ukoloni. Ikitumika kama bandari maalum kwa makoloni ya Ufaransa. Kwa kipindi cha kuanzia mwaka jana Togo imekabiliwa na maandamano mawili au matatu kila wiki! Mjumuiko wa vyama vya upinzani hapa (unaweza kuwaita UKAWA TOGO BRANCH) vimekuwa vikiandaa maandamano haya. Yamesababisha watu kufa na mali kuharibiwa kila yanapoitishwa. Ilishangaza watu ni wapi watu hawa ambao vyama vyao ni dhaifu mno walipotoa fedha za kuendesha maandamano kila wiki? Pia ikashangaza wengi ni kwa nini maandamano haya yamechukua sura ya udini? Baadhi ya mashehe na misikiti imetumika sana. Inashangaza kwa kuwa asilimia 54 ya watogo wanaamini vodoo!
Lakini wengine tunajua chanzo!
Mwaka jana Netanyahu alijitahidi kupitapita nchi mbalimbali za kiafrika na hata kuhudhuria kikao cha wakuu wa nchi za Afrika mjini Addis na kuhudhuria sherehe za kumuapisha Uhuru mjini Nairobi japo hakwenda kiwanjani! Netanyahu huyo huyo aliitisha kikao cha wakuu wa nchi za kiafrika wakati wa kikao cha UN General Assembly mjini New York kikao ambacho Kagame aligoma kuhudhuria! Agenda kuu ya Netanyahu ilikuwa kuomba nchi mojawapo ikubali kuandaa IZRAEL AFRICAN SUMMIT ili tu aonyeshe Izrael inakubalika Afrika na ili kuwadhibiti Wapalestina baada ya Taifa lao kutambulika. Izrael inamezea mate kiti Baraza la Usalama na inadhani Afrika itaunga mkono siku wakiwasilisha ombi. Katika harakati zake hizi alifanikiwa kuishawishi Togo iandae hiyo Summit.
Kabla hata Togo haijaanza maandalizi maandamano yakaanza! Nia ni kuizuia isiandae hiyo Summit na wahusika wanaungwa mkono na mataifa yoote ya kiarabu na baadhi ya mataifa mema ya Ulaya. Wanapinga Afrika kumpa Netanyahu karata ya kuendelea kuikandamiza Palestine na watu wake!
Kweli summit imeshindikana kuandaliwa kutokana na hizi vurugu lakini pia kutokana na mataifa mengi ya Afrika kuiambia Togo utahudhuria wewe na Netanyahu hiyo Summit! Hii ndio hali tete iliyopo Togo hivi sasa. Kuna maandamano ambayo nguvu inatoka nje! kelele za uchaguzi, tume huru, uvunjifu wa haki ni geresha tupu!
Turudi Tanzania
Toka JPM adhibiti uporaji wa kimataifa kwa kiwango cha kutishia maslahi ya nje pameibuka watu ambao kutwa kucha wanawaza maandamano! Huhitaji akili ya ziada kujua ni wao au wanaowalipa! Kwa ilivyo Tanzania wamekwama ila msiwadharau kamwe! Tayari wameanza kuingiza udini kwenye harakati zao! Tumeanza kuona baadhi ya viongozi wa kiroho wakigeuka kuwa wanasiasa! Hawakemei mambo ya kiroho wanakemea mambo ya kisiasa! Utashangaa kiongozi wa kiroho hakemei watu kusoma misa ya wafu mbwa! Hawakemei kiongozi wa kiroho kutoka hadharani na kumtukana kiongozi mwenzao wa kiroho eti ni mjinga na kala maharage! Wao kwao haya ni sawa! tatizo kwao ni katiba ya nchi!
Hapa Togo maandamano yamefikia ukomo! Serikali iliwakusanya viongozi woote wa UKAWA na kuwafungia ndani toka alfajiri hadi usiku wa manane wiki mbili zilizopita baada ya wao kutangaza maandamano tena! Wiki imepita sasa bila maandamano! Waandamanaji waliokuwa wakilipwa wamerejea makwao!
Najua Tanzania leo haikuwezekana ila serikali isidhani yameisha! Kuna watu na mataifa yanatamani amani itoweke wapenye kama walivypenya DRC, Libya, Syria, Iraq, Afghanistan, Somalia, Sudan na kwingineko! Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa sana uliokuwa ukinufaisha wengi! Sasa unanufaisha Tanzania imekuwa nongwa.
Serikali itafute dawa ya kukomesha maandamano! Haiwezekani maandamano yakafanywa ni mchezo wa kitoto! Maandamano yanayoshinikizwa na watu wa nje ni uhaini! Wahusika watendewe kama wahaini!
Najua makala ni ndefu lakini soma!