Shilingi ina pande mbili na mantiki haichagui upande. Kama sifa za aliyofanya mtu mmoja unampa mwingine basi hata makosa halikadhalika.
Mtoa mada umelenga kabisa jambo ambalo hata mimi nimekuwa nikilieleza hapa mara kwa mara. Huwezi kuwa na keki ukaila na ukabaki nayo wakati huohuo. Hawa FISIWENU, hupenda sifa lakini wanapoboronga lazima wamwangushie mzigo mwingine. Kabisa umeweka mambo bayana. Ama wakubali kuwa aliyetekeleza mradi wa maji Shinyanga ni Lowasa ama Mkapa? Kama ni Mkapa kwa kisingizio kuwa hakuna linalofanyika bila rais, kwa hakika hata Richmond isingeweza kufanyika bila rais. Mbona ni rahisi kuelewa!
Lakini pia kuna upande wa pili wa hoja hii. Tunaona Kuwa tangu Lowasa aondoke Wizara ya Maji hakuna tena mradi mkubwa wa aina yake ambao umetekelezwa. Lakini kumeendelea kuwepo ufisadi wa kutisha zaidi baada ya yeye kutoka serikalini. Kwa mantiki hiyo ni dhahiri kuwa Richmond ilikuwa na wenyewe ambao waliendelea nayo kwa majina mengine (Dowans na baadaye Symbion) na fisadi nyingine (mfano ESCROW), bila uwepo wa Lowasa, lakini maji (kama ya Shinyanga) yalikuwa ya Lowasa kwani alipoondoka serikalini na miradi ya aina yake haikuonekana tena.
Tumshukuru Mungu kwa kumtumia Mr. Six kuwafungua macho Wadanganyika.