JK alidhani kumuingiza Samwel Sitta katika serikali yake labda itakuwa ni njia mojawapo ya kuponya majeraha na mpasuko ndani ya chama chake. Lakini mambo yameenda tofauti. Samwel Sitta amekuwa akiikosoa serikali na maamuzi ya serikali hivyo kwenda kinyume na dhana nzima ya Uwajibikaji wa pamoja(Collective Responsibility). Majuzi na hata leo amepingana na uamuzi wa serikali wa kuilipa DOWANS. Ikumbukwe kuwa ni yeye aliyeifikisha CCM hapa ilipo.
Rais JK, mfukuze Sitta. Atakudhuru na ataiangusha serikali. Mbona wenzake akina Mwakyembe wametulia na wanachapa kazi? Sitta hakufai. Wanasema waswahili. ukimchekea nyani, utavuna mabua. Ana chuki baada ya kuukosa uspika.
''You are always clear'' with the lack of clarity! Acha kuwa mvivu wa kufikiri , na usipende kuwa hodari wa umbea! Sitta anajaribu kuwa na mawazo huru yasiyo fungwa na uwaziri! Si lazima ukiwa waziri ushabikie usiri haramu! Je unamkumbuka bi clare short wa uingereza wakati wa sakata la radar ya tz?