OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
- Thread starter
- #41
Sitta hata kutembea hawezi anatembea kama kama mbwa nayemymelea mayai ya kuku
actually hatupo pamoja na sitta,fisadi mkubwa
Mzee Sita naomba nikwambie tu wazi, kwa sasa hauna mvuto kabisa, wananchi wameshakugundua we ni mtu wa aina gani, (nikisema hapa nitaonekana sina nidhamu kwa wazee)....
Kuanzisha kwako CCJ ni uhaini na usaliti mkubwa kwa chama cha mapinduzi.... Leo hii uneona haitoshi umemtuma kijana wako Ramadhani Semtawa aanzishe chama kingine, kweli unatapa tapa mzee wangu, naomba unisikilize tena, ushapoteza mvuto kwa jamii....
Kwenye swala la katika uliingia mkenge bila kujua unaingia mkenge, ulishindwa kufanya what we call political projection, naomba nikwambie hatutaki wanasiasa wasio na uwezo wa kufanya political projection...... Kwa katiba hiyo hiyo leo hii ukienda Arusha au Mara walai unapigwa mawe, wananchi hawakutaki, na wanakuona kama msaliti, mtu wa visasi, wa kupenda sifa na mtu wa maslahi binafsi....
Mzee wangu Sita, yale majumba yako Tabata, Kinondoni na Knyama uliyajenga kwa mawe? leo umenipa maajabu mengine ya dunia kwamba mawe yanaweza kujenga nyumba, nyumba zaidi ya 3 ni za nini kama huo nao siyo ufisadi?, au ndiyo muongozo mpya wa azimio la Arusha.
Mzee wangu Sita, unapogawa laki moja moja kwa wajumbe wa mkutano mkuu, (hata mimi mke wangu amepata huo mgao) umezitoa wapi hizo fedha, au wewe laki moja moja zako ni fedha feki? Au ni makaratasi tu
Mzee wangu, ukiona sisi vijana wadogo tunakushauri usikasirike bali chukua ushauri wetu. Kwa sasa hauna mvuto mzee, usipoteze muda wako kuwaza urais mzee wangu....
Kutana na Sitta Samuel anayekengeuka!
Samuel Sitta sasa kakengeuka! Hii ndiyo lugha rahisi unayoweza kutumia.
Awali nilidhani kuwa anachanganyikiwa kutokana na madaraka mapya ambayo yanaambatana na ulaji mkubwa lakini hapana! Sitta si mgeni katika kupata madaraka na haijawahi kuonekana kuwa amekuwa mgeni! Jambo ambalo linamuelezea vema katika maisha yake ni tabia ya tamaa.
Tamaa ya kupata makubwa, tamaa ya utukufu, tamaa ya kutaka kuabudiwa na tamaa ya kutaka kuonekana kuwa mtu wa mwisho katika maamuzi na pia mtu asiye na baa lolote katika maisha.
Sitta ni aina ya binadamu ambao wangependa kutakatifuzwa kama jambo hilo linawezekana kufanyika wakati binadamu akiwa anaishi. Ni mtu ambaye kwake kujifunza hutokea tu pale anaponyanganywa cheo na sio vinginevyo.
Sifa zake hizi zimempambanua kama binadamu hatari kabisa kuishi naye kwani ana tabia mithili ya Kifaru, huwezi kungamua ni lini atajipindua na kukudhuru hata kama umekuwa ukimtunza na kumlisha mapochopocho na vyakula vingine vyenye nakshi na kumvisha lebasi!
Wakati uchaguzi unamalizika wa mwaka 2005 alikimbilia kwa Rais JK na kutaka apewe madaraka ya Waziri Mkuu. Inaelezwa hakukuwahi kupatikana- katika historia ya nchi mtu kumkimbilia Rais na kujieleza shauku yake na kiu ya kutaka madaraka hasa pale Rais anapokuwa tayari kaapishwa! Sababu kubwa ni kuwa hata kama alikuwa karibu na wewe, anapoapishwa tu anakuwa kapakwa mafuta, anakuwa mteule na hivyo ili umuone na kueleza shida zako lazima ziwe zimechujwa vema na wewe mwenyewe kichwani.
Hii ilikuwa tofauti kwa Sitta! Yeye kaenda kusaka Uwaziri Mkuu na akaambiwa with an open eye kuwa sikupi! Alipotoka hapo akaanza vita, vita hivyo aliviweka moyoni lakini wakubwa kwa kumuheshimu wakaona wamsitili kwa kumpa Uspika.
Alipopata Uspika akaomba apewe Escort kama ya Waziri Mkuu. Rais Kikwete akamwambia omba lingine hilo sikupi! Akatunga sababu kuwa kuna watu wanamtafuta hivyo apewe ulinzi! Haikuonekana shida system ikampa na hata sasa hataki kuwaachia licha ya kwamba ni mwaka wa tano unafika tangu aache nafasi ya Uspika.
Hakuishia hapo akaenda tena kuomba na uwaziri wa mkewe Magreth wakubwa wakaona isiwe nongwa wakampa! Vyote hivi alivyopata havikuondoa sumu iliyoujaa moyo wake mithili ya mtu aliyekula sifongo.
Akautumia Uspika kwa lengo la kuiangusha serikali na mwisho ni Edward Lowassa Waziri Mkuu wa wakati huo, aliyeona nia mbaya ya Sitta dhidi ya serikali ya CCM, hivyo akaamua kuachia nafasi yake ili kukilinda chama chake pamoja na serikali yake.
Lowassa akakubali msalaba mzito, akaubeba kwa uchungu na matusi na dharau! Hadi leo anafanya hivyo, lakini la kushangaza ni kuwa Watanzania wamegundua alichokifanya Lowassa nai sasa wanamuimba kila kona na wakimtaka achukue fomu kwani wao tayari wamejiandaa kumpigia kura awe Rais wao.
Hapa ndipo inapofikia hofu nyingine ya Sitta. Alitegemea dhamira yake chafu dhidi ya Srikali ambayo iligunduliwa na Lowassa na yeye kukubali kubeba msalaba ingeendelea hata leo. Kila akipita anasikia wananchi wakimtaka Lowassa na wala hawamtaji yeye. Anabaki akichanganyikiwa hali inayomfanya hata sasa kuanza kupambana na hata rafiki yake wa zamani Harrison Mwakyembe kwa kisa tu kuwa Mwakyembe alimkanya kutotumia ugonjwa wake katika harakati zake za kutangaza uadui wake na Lowassa.
Tena, haikuishia hapo, akamchukia Mwakyembe kwa kuwa tu alisikia amekutana na Lowassa na kuzungumza kuhusu yaliyotokea na namna ya kuishi vema huko tuendako. Sasa anamdhalilisha kila kukicha kwa kupindua kila jambo ambalo alilifanya wakati akiwa Waziri wa Uchukuzi.
Wanasiasa wa aina ya Sitta licha ya kuwa na vijana wake wenye hulka za kifisadi na kihuni ambao hivi karibuni walianzisha mtandao wenye kura za maoni ambao ulilenga kuwadanganya wananchi kuwa Sitta anakubalika, wameamua kwa makusudi sasa kupiga kelele mithili ya mfa maji ambaye hakosi kutapatapa!
Ndio maana juzi Sitta kaanza naye kuingia katika mitandao ya kijamii kutukana. Anatukana na sijui anapata wapi muda huo katika nchi ambayo haina ndege na wala reli haifanyi vema.
Sitta hajui majukumu yake, anawaza urais tu licha ya kuwa alishaharibu na kuihudhi Tanzania wakati alipotumia hila na rushwa za wazi wazi kupitisha Katiba Pendekezwa!
Nitumie nafasi hii kumsalimu kwa leo na nakuja tena na jingine maana natambua salamu za leo hazitamuingia sana!
Stay Tuned: Mukambila......
Sita, Nape, Kilango, Mwakyembe ni wapenda vyeo. Tuwaogope kuliko tunavyoogopa UKIMWI
Mleta mada unaitwa Suzan alafu mkewako ataitwa nani?
Mtoto Wa Kawe UKWAMANI. Ila Mkuu PERFECT Huyu Dogo Ni Mpambanaji Mno Tena Kushinda Hata Hao Wasomi Unaowajua Wewe. Namkubali Mno!
Vile viboko alicharazwa na Mwl. J K Nyereree havikumbadilisha tabia, sasa afundishwe na dunia
Wewe ni punguani mambo ya katiba sio ya Jamii?Mleta mada naona km umeleta mambo ya kibinafsi zaidi, ungeongelea maswala ya yanayogusa zaidi maslai ya jamii, mambo ya nyumba 3 kwa mtu km sita wala sioni tatizo, labda yawe maghorofa km ppf tower, hilo la kuburuza bunge la katiba hata mm alinikera sana. Sasa na mkeo kapewa laki moja,? Za nini zote hizo, toa taarifa takukuru, au mpeleke mkeo mahakamani kwa kupokea rushwa, hapo utakuwa umeonyesha uzalendo kwelikweli.
chama gani ameazisha sitta na kijana wake semtawa?mtoa mada ungetusaidia hilo
Hahaaaa
Acha nicheke tu