Samuel Sitta: Historia yangu kunibeba katika Urais

Samuel Sitta: Historia yangu kunibeba katika Urais

Ni kweli alikuwa SPIKA MZURI SAANA lakini ajiulize kwa nini 2nd term aliambiwa ili achaguliwe ni lazima ajibadilishe na kuwa Mwanamke.Yeye ni Spika pekee aliyekaa kwa term moja tu.
Aliharibu kwenye BMK...na hapo aliingizwa mkenge baada ya wajanja kuona nyota yake ya urais inangara na hao wajanja walijuwa katiba mpya popote duniani inakuwa ni mgogoro..sijui kwa nini SEVEN minus ONE hakujuwa hili.
Umri wake pia umeenda mbali wasiwasi anaweza ngangania kama Mzee Mugabe.
Yeye na Mh.Pinda hawana support ya waumini wa dini zote...kwa sababu ya mahakam ya kadhi.Kosa walichukuwa viongozi wa kidini wasiokubalika na kufanya nao mazungumzo.Kwa mfano zaidi ya 90% ya waislamu hawamkubali Alhad....sheikh wa mkoa wa Dar ....kwani aliwekwa kinyume na katiba ya Bakwata.
 
Urambo kwake sasa hv hata kumsikia hawataki, huyu mzee akili zake kwisha kabisa, Alipokuwa spika, he talks points alot, but tangia AWE SPIKA WA BUNGE LA KATIBA, KAWA HOVYO HOVYOOO....sijui kaharibika hivi kwnn, huyu si RIZIKI kabisa...utafikiri kabadilishwa ubongo...i can't believe ndio yuleed mzee wa STANDARD AND SPEED...!!! kwisha kabisa...!!!
 
Samuel Sitta kupitia Mwananchi amedai kuwa historia yake nzuri ndiyo itakayomfanya aungwe mkono katika harakati zake za kuomba ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania.

Kwanza anadai kuwa atakumbukwa kwa kutimiza ndoto za watanzania ya kuwapatia katiba mpya.

Pili kwa utumishi wake wa muda mrefu Serikalini na tatu ni utendaji wake kama Spika wa Bunge.

Chanzo: Mwananchi leo

Naiona ileeee october mirembe inavyomiminika wagonjwa wa akili.
 
Anajidanganya alishachemka na CCM wakirogwa kumweka huyo wapinzani wanachukua kiulaini sana
 
Makalio yake

Nikiangalia hiyo picha kwenye jina lako naona haiendani na hii kauli!

Huyu Mzee hakujua kama JK alikuwa anamwingiza mjini-kwa kumchafua kupitia Katiba mpya kwa sasa Kazi yake kwisha-hauziki tena si ndani ya CCM wala Upinzani.
Asubiri fadhila ya kuendelea kuwa Waziri kwenye serikali ijayo na tena awe makini akicheza karata vibaya Ubunge na Uwaziri atausikilizia Redioni na Tv.
 
Samuel Sitta kupitia Mwananchi amedai kuwa historia yake nzuri ndiyo itakayomfanya aungwe mkono katika harakati zake za kuomba ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania.

Kwanza anadai kuwa atakumbukwa kwa kutimiza ndoto za watanzania ya kuwapatia katiba mpya.

Pili kwa utumishi wake wa muda mrefu Serikalini na tatu ni utendaji wake kama Spika wa Bunge.

Chanzo: Mwananchi leo

Hahahaaaaa eti historia itanibeba
Wadanganyika wameshastukia dili siku nyingi sana bwana 6, yaani watu walikua absent kwenye mchakato wa katiba ila kula zao zilihesabiwa!!! Tanzania haiishi maajabu tusubiri hata mzee wa vijisenti ipo siku atasema historia itambeba
 
Amefuta mazuri yake yote na katiba mbovu wanayoipendekeza ikiwa ni pamoja na kutukana viongozi wa dini.Atunze fedha alizojipatia kwa kumalizia uzee wake
 
Sitta kwangu ni fisi! Hovyo kabisa!!!
 
Huyu mzee akaharibu sana kwenye Katiba, halafu hajui kwamba kaharibu. Ni bora akipumzika tu nyumbani kwake, atumie hiyo pesheni yake vizuri basi baada ya muda wake kukoma
 
Sitta amesahau kwamba alishiriki na wenzake wa CCM kutupilia mbali maoni yetu tuliyoyatoa kwa Jaji Warioba? Asitufanye wajinga, hasa sifa hata robo ya kuwa Rais wa nchi.
 
Ni kweli historia yake ya kuwatukana viongozi wa dini itambeba kweli. Kama anadhani tumeshasahau matusi aliyoyatoa dhidi ya viongozi wetu wa kiroho AMEPOTOKA.
hao viongozi ni wapuuzi. hata mimi namuunga mkono sitta kuwatukana. niwapuuzi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom