Samsung yafeli mtihani wa kuwa ndani ya maji

High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,915
2,131
Simu ya kisasa ya Samsung Galaxy S7 inayopigiwa upatu kuwa na uwezo wa kustahimili kuwa chini ya maji imefeli majaribio ya shirika la moja la kutathmini ubora wa bidhaa za kielektroniki.

Programu ya simu hiyo ya Samsung Active ilizima punde baada ya kutumbukizwa ndani ya pipa la maji.

Kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa bidhaa, Consumer Reports ilirejelea jaribio hilo kwa mara ya pili wakitumia simu tofauti na kama ile ya kwanza ikafeli.

Kampuni ya kutengeza simu hiyo ya Samsung ikijitetea imesema huenda simu hizo zilikuwa ni mbovu na hivyo kuruhusu maji kuingia ndani.

Simu hizo za Samsung zilizima baada ya kutumbukizwa ndani ya maji

Simu hizo zilitumbukizwa ndani ya mapipa ya maji na kutolewa baada ya dakika.

Simu hizo za Samsung zilizima.

Kulikuwa hata na maji katika eneo la kamera za simu hizo mbali na viputo.

Kampuni inayotengeza simu hizo kutoka Korea Kusini Samsung imejitetea vikali ikisema kuwa Galaxy S7 Active, inayouzwa Marekani imefanyiwa majaribio kabambe na hata kupewa cheti maalum cha IP68.

Kampuni inayotengeza simu hizo kutoka Korea Kusini Samsung imejitetea vikali ikisema kuwa Galaxy S7 Active, inayouzwa Marekani imefanyiwa majaribio kabambe na hata kupewa cheti maalum cha IP68.

Hati hiyo maalum inathibitisha kuwa simu hizo zinauwezo wa kustahimili kutumbukizwa ndani ya maji.

Consumer Reports iligonga vichwa vya habari kote duniani ilipotambua kuwa simu aina ya Iphone 4 ilikuwa na matatizo ya ya kifaa cha kuungia mbali.

''kwa kawaida tumekuwa tukiamini pale mtengezaji wa bidhaa akituambia kuwa bidhaa yake inaweza kustahimili hata kutumbukizwa ndani ya maji, lakini leo tulipojaribu kuhakiki madai ya Samsung tuligundua kuwa simu hizo zinazima baada ya kutumbukizwa ndani ya pipa la maji ''

''Bila shaka wale walionunua simu hizo kwa imani kuwa haitoharibika hata baada ya kutumbukizwa ndani ya maji, watalazimika kutafuta ridhaa kutoka kwa watengenezaji,,,''
 
Ebu ngoja nijaribu kutumbukiza yakwangu kwenye ndoo ya maji. Ikizima na claim samsung wanipe simu nyingine maana ipo ndani ya warrant
 
Siwatetei Samsung, ila naamini mazingira ambayo ilo shirika walifanyia majaribio hayakua fair.

Galaxy S7 ipo IP68 certified, hivyo ni dust proof na water resistant katika kina cha maji cha 1.5m in 30mins max.

Hujasema walitumia pipa la kina gani na waliiweka cm kwa dakika ngapi. Besides, katika mazingira ya kawaida, only girls ndio wataingia na simu kwenye swimming pool na kujipiga selfie.

Simu kua water resistant wameweka katika zile scenerio za bahati mbaya kama kunyeshewa na mvua au kuloweka na nguo wakati unataka kufua.
 
Huo utaalamu wa kuzuia maji kwenye simu anao Sony tu wengine wababaishaji tu.
 
Huo utaalamu wa kuzuia maji kwenye simu anao Sony tu wengine wababaishaji tu.
Sony Z series ni water resistant ila watu wengi tu wameua simu zao kwa kujifanya wanataka piga picha kwenye swimming pool
 
mbna kuna video YouTube wanafanya comparison ya iyo S7 na iphone 6S plus ya kuweka kwe maj ana zote baada ya hapo zina work fresh tuu
 
kama wamesema s7 haingii kwenye maji haimanishi kwamba uende ukaiweke kwenye maji uangalie kama hayata ingia. hapo utakuwa ni mpumbavu.
labda itokee bahati mbaya.
 
Back
Top Bottom