CORAL
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 2,827
- 1,862
Timu ya wataalam wa teknolojia wa Samsung Adanced Institute of Technology (SAIT) kwa kushirikiana na wataalam toka Seoul National University's School of Chemical and Biological Engineering, "wamevuka mipaka" kwa kutengeneza betri zinazoweza kujaa chaji toka 0% hadi 100% kwa dakika 12 tu!!
Walichokifanya ni kuboresha lithium ion batteries kwa kutumia material iitwayo graphene balls. Hii material ina uwezo wa kupokea electrons kwa haraka zaidi na kwa kiwango kikubwa zaidi hivyo kupunguza muda wa kuchaji betri. Betri za graphene balls zina sifa zifuatazo:
Jambo lingine la kufurahisha ni kuwa tusitarajie teknolojia hii kuongeza sana bei ya betri kwa kuwa graphene balls zinapatikana kwa urahisi na kwa gharama ndogo.
Huenda Samsung wakatengeneza hizi betri wenyewe au wakatoa leseni.kwa makampuni mengine ili yafanye kazi hiyo. Lakini vyovyote iwavyo bila shaka hii ni neema kwa maendeleo ya dunia nzima.

- kupokea umeme kwa haraka kwa hiyo kupunguza muda wa kuchaji yaani 1/5 ya muda wa kawaida wa fast charging ambao hufika hadi dakika 60.
- betri kuhimili joto kali: betri za lithium ion zina kasoro ya kulipuka zinapopata joto kali hasa wakati wa kuchaji lakini kwa kuziongezea graphene balls betri zinahimili joto hadi centigrade 60 bila tatizo. Kwa hiyo teknolojia hii itapunguza hofu ya betri kulipuka wakati wa matumizi.
- kukaa na chaji muda mrefu zaidi (battery capacity): yaani betri pamoja na kuchajiwa kwa muda mfupi sana (dk 12) inakaa na chaji muda mrefu zaidi kwa kuwa inabeba nishati nyingi zaidi