Samsung galaxy tabs 10.5

Northern Lights

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
383
347
Amani iwe kwenu wana teknolojia
Katika kufanya utafiti wa ipi tablet nzuri inayoweza kunifaa kwa ajili ya matumizi yangu ya shule na matumizi binafsi ( kusoma PDF, kupiga picha, kurekodi video, ku-surf kwny internet pamoja na matumizi mengine) nimekutana na hii galaxy tab S 10.5 na nimevutiwa nayo sana. Kwa mtu mwenye experience nayo ningeomba atupatie na pia anayefahamu sehem zinapopatikana pamoja na bei zake itakuwa ni vyema zaidi
. Ahsanteni
 

Attachments

  • samsung-galaxy-tab-s-10.5-malaysia-03.jpg
    samsung-galaxy-tab-s-10.5-malaysia-03.jpg
    30.8 KB · Views: 209
  • t800_600x600_xlarge_cr.jpg
    t800_600x600_xlarge_cr.jpg
    31.3 KB · Views: 176
  • samsung-galaxy-tab-s-105-1.jpg2.jpg
    samsung-galaxy-tab-s-105-1.jpg2.jpg
    74.8 KB · Views: 159
una laptop/desktop ya shule? kama huna achana nayo tafuta real os kwanza iwe ni osx/windows/ubuntu etc

android haiwezi kutumika kwa matumizi ya kishule shule, kusoma vitu kama pdf na documents utaweza ila kuzitengeneza ni mtihani. mambo mengine ya kawaida kama kucheza game, kubrowse net, kuchukua video na kupiga picha utaweza.

kama tayari una computer ya shule ila unataka tu tablet ya ziada unaweza kuinunua ni kati ya tablet bora za android lakini kama unataka ununue s series ya hizi tablet ni bora usiulize bei sababu zipo juu sana. hizi s series ndio tablet za kwanza duniani kutumia vioo vya amoled ambavyo ni vya bei ghali. kwa tab kama hii inayotumia line ya simu kwa maduka yetu huwenda ikawa ni milioni au inakaribia hio bei.

kuna jamaa alinunua juzi hapa ngoja nikuitie
Kitimoto

thread hii hapa
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...nataka-kununua-tablet-aina-gani-ni-nzuri.html
 
Last edited by a moderator:
Kwa Mawakala wa Samsung bei zinatofautiana, bei ya chini ni Tshs. 950,000.00 na zinafika mpaka Tshs. 1,250,000.00. Kwa hizo Tablets zipo zenye kutumia SIM card na ambazo hazitumii SIM card, nadhani zilizoko kwenye Maduka yetu zinatumia SIM Card. Yangu ni 8.4", model T705 yenye kutumia Sim Card, kuna model T700, hizi hazitumii Sim Card. Tab S 10.5", model T800 ni WiFi tu na T805 inatumia Sim card
Screenshot_2014-12-06-12-59-53.jpg
 
Shukran sana Chief Mkwawa
tayari nina Windows PC ila Hii nina ihitaji haswa kwa sababu ni portable na inakaa na chaji kuliko kutembea na PC. Ningependa kujua pia hivi na zanyewe huwaga kuna COPY kama kwenye simu. Naogopa nisije nikaspend pesa nyingi halafu nkaingizwa mjini
 
Shukran sana Chief Mkwawa
tayari nina Windows PC ila Hii nina ihitaji haswa kwa sababu ni portable na inakaa na chaji kuliko kutembea na PC. Ningependa kujua pia hivi na zanyewe huwaga kuna COPY kama kwenye simu. Naogopa nisije nikaspend pesa nyingi halafu nkaingizwa mjini

cha muhimu ni warranty kaka inabidi wakupe, na kama zina adh(am not sure) inabidi pia wakufanyie registration. kama itatokea ni fake basi watakuwa responsible wao na sio wewe
 
Shukran sana Chief Mkwawa
tayari nina Windows PC ila Hii nina ihitaji haswa kwa sababu ni portable na inakaa na chaji kuliko kutembea na PC. Ningependa kujua pia hivi na zanyewe huwaga kuna COPY kama kwenye simu. Naogopa nisije nikaspend pesa nyingi halafu nkaingizwa mjini


Kama upo Dar hamna duka la Samsung Authorised dealers linauza simu Copy
ukienda maduka uchwara ndo utakutwa na hilo nenda maduka ya kuaminika na yanajulikana kwa hapa Dar posta kule,Mcity nk

Ila kwa sasa sijasikia au kuona clone za hizo tab...clone/copy zipo nyingi s3-s5 note2-n3
 
Back
Top Bottom