Kwa Miaka kadhaa nimekuwa mtumiaji mzuri wa Note na S series za Samsung, pia nimejaribu J series kidogo though sikupendezwa sana.
Hapa Majuzi kama miezi miwili iliyopita nikaamua nijaribu kutumia A Series za Samsung, Nikachukua A51.
Kwanza Kabisa Simu design ya Upande wa Back Cover ni mbaya yaani haivutii.. inazidiwa hata na note 5 ya mwaka 2015 huko.
Simu ina bad music experience, Note 5 ina mziki mzuri kuizidi.
Simu hii ina performance mbovu mno.. yaani ipo slow sana.
A series zinastack sana zikizidiwa.
Mbaya zaidi inabagua earphones na kuna wakati inastack na uko on call.
Ukitaka uinjoy Simu za Samsung achana na hizi A series.