Samson Mwigamba: CHADEMA ndumilakuwili

Samson Mwigamba: CHADEMA ndumilakuwili

Na. Mwandishi wetu.

Kada wa chama cha Mapinduzi CCM ambaye kwa nyakati tofauti amepata kuwa mwenyekiti wa mkoa wa wa Arusha chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na baadae kutimkia ACT WAZALENDO kuwa muasisi na katibu mkuu wa kwanza wa chama hicho Samson Maingu Mwigamba amewasikitikia watanzania wa vyama vyote wanaohama vyama vyao na kujiunga na CHADEMA na kusema hawana tofauti na mtu anayeruka vumbi na kukanyaga moto na kusisitiza kuwa sifa kuu ya kukuwezesha kuishi kwenye chama hicho ni UNDUMILAKUWILI.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake mkoani Arusha hivi karibuni, mwigamba amesema kwamba chama hicho chake cha awali kimepoteza uwezo wake wa asili wa kujisimamia na hivyo kujikuta kinaenda enda tu sambamba na kusema kuwa chama hicho sio mfano mzuri wa kimbilio la demokrasia na utawala wa sharia unaofuata katiba na usimamizi bora wa fedha akitoa mifano kadhaa.

‘’huwezi hama CCM halafu useme unafuata Demokrasia CHADEMA, utakuwa unachekesha rafiki yangu, pale CHADEMA demokrasia ni Mwenyekiti na mwenyekiti ndio Demokrasia, analotaka ndio huwa na ukijaribu kumkosoa lazima uende na maji’’. Anaanza kueleza Mwigamba

‘’mimi ni kama nimekulia ndani ya Chadema nikishiriki katika nafasi mbalimbali za ndani ya chama, nakuhakikishia kama kuna chama kinasigina katiba basi CHADEMA ni namba moja…kumbuka namna mbowe na wenzake walivyokinyofoa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama ili kimpe yeye nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kudumu, na kumbuka siku tu niliyoanza kuhoji kuhusu hilo nilivyofurumushwa kama kuku pori’’. Anaongeza Mwigamba huku akicheka

Mwigamba anaendele kusema kuwa mara baada ya mbowe kuchukua kijiti cha uenyekiti wa chama hicho alijidhatiti kuhakikisha chama hicho kinakuwa na agenda ya kuisimamia ili kipate kuaminiwa na wananchi na hatimaye kupewa dola jambo ambalo chadema ilifanikiwa kwa kujitanabaisha wazi kuwa wao ni watetezi wa rasilimali za nchi na wapinga ubadhilifu na ain azote za ufisadi.

anasema aliwahi kusimuliwa kisa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe kuhusu chanzo chama hicho kushikilia ajenda ya kupiga vita ufisadi ambapon alimwambia kuwa mwaka 2004 baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti taifa alialikwa kwenye mikutano mikuu ya vyama vya Republican na Democrats vya Marekani alipokutana na Mwanasheria Kivuli aliyetokana na chama cha Democrats wakati huo Republican ikiwa inaongoza nchi chini ya Rais George Bush na mwanasheria huyo kumweleza Mbowe kwamba haijalishi chama kina sera nzuri kiasi gani, lazima kiaminiwe na wananchi.

Aidha mwigamba anasimulia zaidi kuwa mwanasheria huyo alimweleza mbowe kwamba ameishi Tanzania kwa vipindi tofauti na katika kufanya kazi zake na utafiti aligundua kwamba nchi ilikuwa inapoteza pesa nyingi kupitia ufisadi na kumwambia Mbowe kwamba kama nchi ikifanikiwa kuzuia pesa zinazopotea kwa ufisadi, haitahitaji tena kuwa na bajeti tegemezi kwa mataifa ya nje na kumshauri kuangalia vitabu vya taarifa za Mdhibiti na MKaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anazozitoa kila mwaka ataona pesa nyingi zinavyopotea na huo ndio ukawa mwanzo wa Mbowe wakati huo akiwa mbunge wa Hai, kuanza kuzunguka mikoani akiambatana na wabunge wengine wa CHADEMA ya wakati huo ambao ni Marehemu Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Dr. Willibrod Slaa (Karatu), Dr. Amani Walid Kabourou (Kigoma mjini) na Grace Kiwelu (Viti maalum) kuelezea mapungufu waliyoyaona wakiwa na ripoti za CAG wakiwaeleza wananchi jinsi ufisadi ulivyokuwa unatafuta mabilioni ya pesa za watanzania maskini.

‘’Huo ndio ukawa mwanzo wa CHADEMA kushikilia ajenda hiyo ya ufisadi mpaka wakaingia nayo kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo Mbowe aligombea urais na kushindwa na Jakaya Kikwete lakini wakapata wabunge watano wa kuchaguliwa na sita wa viti maalum. Ni uchaguzi huo ndio uliowaleta bungeni akina Zitto Kabwe, Halima Mdee na wenzao na hoja ya ufisadi ikawa ni hoja hasa’’. Anaendelea Mwigamba

Mwigamba anasema kuwa Mbowe alimwambia kwamba waliamua kwenye kamati kuu kwamba kabla ya wabunge wao hawajaenda bungeni, chama kiwe kimefanya utafiti na kuvumbua madudu ya ufisadi ili wanapoenda bungeni wayasimamie hayo na ndio zama zilizoibuka kashfa ambazo majina yake yamebaki kwenye kumbukumbu za watanzania kashfa kama za Meremeta, Deep Green, EPA, Richmond, Buzwagi, na nyinginezo

“Ajenda hiyo ikaipelekea CHADEMA kuwa maarufu sana nchini kiasi cha uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa akagombea urais na kuchuana vikali na Kikwete. Ingawa hakushinda, chama kilichupa kutoka wabunge watano wa majimbo mpaka 23 na baadaye 24, na kutoka wabunge 6 wa viti maalum mpaka 25. Chama kikawa maarufu kiasi cha kufikiriwa kuingia madarakani mwaka 2015. Mbowe alirudia kunihadithia kisa cha huyo mwanasheria kivuli wa kimarekani mara pili tukiwa Karatu mwaka 2012 akitamba juu ya kuutumia vizuri ushauri wa mwanasheria huyo”, anasema Mwigamba.

Mwigamba anasema kwa kipindi kirefu chama hicho kilifanikiwa kujijengea sura ya kuwa watetezi wa Rasilimali za nchi na waoinga ufisadi wakiwa nje lakini wanapokuwa ndani ya chama wanakuwa na madudu makubwa hasa yanayohusu matumizi ya fedha hasa zinazotokana na ruzuku na hivyo kusababisha mitafaruku mikubwa miongoni mwa wananchama na viongozi wao kama ile iliyowahusisha Mbowe na Marehem Chacha Wangwe, na huu wa karibuni baina ya Mbowe na Zitto kabwe ulioishia kwa Zitto kufukuzwa uanachama na hatimaye kutimkia ACT WAZALENDO

“Lakini ndugu mwandishi hebu rejea mwaka 2013 uone Mbowe alivyofanya juhudi kubwa kuvuruga chama kwa matayarisho ya kuja kumpokea yule waliyempachika nembo ya ufisadi. Walianza na Zitto, Kitila na mimi wakamalizia kwa Slaa 2015 na gia ikawa imebadilishiwa angani. Muulize leo Mbowe kuhusu ushauri wa yule mmarekani na wapi wameipotezea ajenda yao ya ufisadi mpaka wananchi wanakosa Imani na chama chao, atakuambia alibadilisha gia angani’’. anasema

‘’alibadilisha gia angani akamchukua Lowassa ambaye Lema alisema kumzomea fisadi kama Lowassa ni heshima kwa Mungu, Msigwa akasema anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili, Lissu akasema CCM wamempa fomu ya kugombea urais fisadi anayetakiwa kuwa gerezani. Leo Nyalandu anaenda kujiunga na chama cha kubadilishia gia angani!!!? ameshajua Mbowe 2020 akibadilisha gia angani ataelekeza wapi chama?” anahoji Mwigamba huku akicheka kwa utani.

‘’huwezi kuwaelewa chadema kama ni popo au ndege, mchana wanasimamia hili, jioni lile basi ilimradi tu…hebu ona mbowe alivyokuwa anasema Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA…leo amebanwa nayeye kwenye madili yake amegeuka anasema Magufuli dikteta/…hakuna Dikteta katika siasa za Tanzania kumzidi Mbowe nakuambia mimi, chadema wanalijua hilo na UKAWA halikadharika’’.

‘’akigeuka huku anaona waliojihusisha na ufisadi wanapukutishwa kutoka serikalini, akigeuka anaona utumishi wa umma unavyorejea kwenye uadilifu na uchapakazi, miradi ya maji inatekelezwa hata iliyolala kwa miaka, miradi ya barabara za juu iliyohubiriwa kwa miaka inaanza, reli ya standard gauge iliyoishia kusemwa midomoni kwa karne inanyanyuka, miradi ya umeme, nk, akaona hapo hana jinsi, akasema rais anatekeleza ilani ya CHADEMA’’. Anaendelea Mwigamba

‘’ Mbowe na CHADEMA yake walipoona rais anawashughulikia mpaka wale waliowachangia wao pesa za kampeni na hatimaye kumgusa Mbowe mwenyewe kwa ufisadi mkubwa aliolifanyia shirika la nyumba la taifa kwa makumi ya miaka, hali yao ikawa ngumu vijana wa mtaani wanasema siku hizi vyuma vikakaza, wakaanza kusema rais anavunja sheria na hatimaye wakaibuka na udikteta’’. Mwigamba anaongeza

Tukio jingine alilolibainisha Mwigamba ni la Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye.

’’ Ni Sumaye huyu huyu aliyeshambuliwa sana na Mbowe na CHADEMA yake miaka ya 2000 pale wafanyabiashara wasio wana CCM walipolalamika kunyanyaswa na mamlaka ya serikali hususani TRA. Sumaye akaibuka na kusema,…. Kama mfanyabiashara unataka mambo yako yakunyookee, tundika bendera ya CCM kwenye biashara yako…. Walimtukana Sumaye kila matusi na kuonyesha anavyotumia vibaya madaraka ya uwaziri mkuu lakini leo Sumaye ni nguzo kuu kwenye CHADEMA’’.

‘’Hauwezi kuwa na akili timamu halafu uwaamini chadema si unakumbuka Kwenye uchaguzi wa 2015 kimsingi Sumaye ndiye alikuwa mpiga zumari mkuu na sasa ni mmoja wa watu wanaopigiwa upatu ndani ya CHADEMA kugombea urais 2020 mtu aliyekaa kwenye uwaziri mkuu kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote lakini anayeongoza kwa kukosa alama hata moja aliyoiacha eti leo agombee urais!!!? Hiyo ndiyo CHADEMA’’. Anazidi kueleza

“Mtazame hata huyuNyalandu mwenyewe. Angalia clip ya video ya Joshua Nassari bungeni, angalia tweets za Mch. Msigwa na Halima Mdee. Hivi hawaoni hata aibu mtu ambaye haijapita hata miaka mitatu tangu mmwite majina ya kila aina (mshika makalio ya mabinti askari wa wanyamapori, mtalii wa kutumbua kodi za watanzania na wasanii Marekani, fisadi wa hati za rais za uwindaji, nk) leo mnamwita kamanda, jembe, mara dume, mmh!”

Mwigamba anawapa pole sana wale wote wanaokimbilia CHADEMA na wale wanaojiandaa kufanya hivyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020.

''Kama ni mafisadi waende maana kwenye seerikali ya Magufuli hamna namna ya fisadi kusurvive. Ni sawa na kumwambia mwenye dhambi asurvive mbele ya nuru ya Mwenyezi Mungu. Haiwezekani. Wa namna hiyo watangulie tu CHADEMA ndiko kwenye ngome mpya ya mafisadi. Lakini wale walio waadilifu wanaodhani kule ni kimbilio, wamuulize Dr. Slaa atawasimulia vizuri zaidi. CHADEMA mchana unaweza kuwaona malaika safi toka mbinguni na usiku ukakuta ni mashetani wenye mapembe kabisa!''. alimalizia

SOURCE. JAMVI LA HABARI

Well spoken
 
733d126634100f39197079e1c713d829.jpg
mbowe.jpg
 
Hakuna mwanasiasa ambaye maneno yake yamenyooka wote wachumia tumbo tu,ptuu ngoja tuendelee kupambana na hali zetu tu.
 
CHADEMA wenyee wanasema ni kama Kanisa la kilokole, ukiokoka unapolekelewa na kutumainishwa kwamba UKIFA utaenda mbinguni kwa baba. Ila apana ruksa kuhoji chochote, we ukiambiwa hiki au kile unatakiwa kuitikia "Amin".
 
Ni kweli chadema ni ndumi la kuwili,bali Mwigamba ni ndumi la kutatu.Yaani Act,chadema na ccm.Ila amejikita ktk kuangalia tumbo lake.
 
Hebu Watanzania tufike mahali tujifunze kutafakari kwa dhati ili kujua kama kuna haja ya kusema kila jambo unalolifikiria ama la. Samson Mwigamba bado ni rika la vijana ambao kimsingi kuwepo kwao kunapaswa kuonyesha uhai na ustawi wa taifa la kesho. Hali ilivyo kwa sasa Mwigamba hakupaswa hata kuwa mwanasiasa wa chama chochote tena ama la angekuwa mwanasiasa asiyekuwa muumini wa chama chochote la mwanachama wa chama chake yeye pekee yake. Si sahihi kwa ujenzi wa demokrasia mtu akahama chama zaidi ya kimoja halafu bado akajiita mwanasiasa na kulilia demokrasia.

Demokrasia haimanishi uhuru wa kila kitu! Ni kweli kwamba hata maamuzi yanayofikiwa kwa kura huwa ni ya kidikteta kwani huwapa fursa wengi na wachache kukosa. Lakini katika demokrasia wale wachache hulazimika kukubaliana na maamuzi ya wengi na hivyo mambo huendelea kwa namna hiyo.

Ningetarajia kuwa kijana Samson angezungumzia kushindwa kwake kushirikiana na wenzake kukiendesha chama chao cha ACT-Wazalendo ambacho yeye ni miongoni mwa waasisi badala ya kuanza kuizungumzia CHADEMA ambacho yeye si mwanachama tena! Anaizungumzia CHADEMA ya wakati ule kabla hajaihama na sasa anataka kuiminisha jamii kuwa chama hiki hakifai. Kimsingi yeye Mwigamba ndiye hafai kuwa mwanachama kwenye chama chochote.

Ninadhani vijana wote aina ya Mwigamba wajifunze namna nzuri ya kufanya siasa wasirithi style moja tu ya kisiasa kwamba ukikihama chama chako basi umepata uthubutu wa kuanza kukishambulia it is rubbish! Serious we get fade up with your political styles!
 
CCM kuna ukwasi gan wa kutosha?Hebu tusaidie
Wana fursa ya kula hela ya umma bila kuhojiwa. Hukuona mgao wa 10m kwa wabunge wote ili tuu waseme ndio muswada wa madini upite kwa dharula?
 
Na. Mwandishi wetu.

Kada wa chama cha Mapinduzi CCM ambaye kwa nyakati tofauti amepata kuwa mwenyekiti wa mkoa wa wa Arusha chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na baadae kutimkia ACT WAZALENDO kuwa muasisi na katibu mkuu wa kwanza wa chama hicho Samson Maingu Mwigamba amewasikitikia watanzania wa vyama vyote wanaohama vyama vyao na kujiunga na CHADEMA na kusema hawana tofauti na mtu anayeruka vumbi na kukanyaga moto na kusisitiza kuwa sifa kuu ya kukuwezesha kuishi kwenye chama hicho ni UNDUMILAKUWILI.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake mkoani Arusha hivi karibuni, mwigamba amesema kwamba chama hicho chake cha awali kimepoteza uwezo wake wa asili wa kujisimamia na hivyo kujikuta kinaenda enda tu sambamba na kusema kuwa chama hicho sio mfano mzuri wa kimbilio la demokrasia na utawala wa sharia unaofuata katiba na usimamizi bora wa fedha akitoa mifano kadhaa.

‘’huwezi hama CCM halafu useme unafuata Demokrasia CHADEMA, utakuwa unachekesha rafiki yangu, pale CHADEMA demokrasia ni Mwenyekiti na mwenyekiti ndio Demokrasia, analotaka ndio huwa na ukijaribu kumkosoa lazima uende na maji’’. Anaanza kueleza Mwigamba

‘’mimi ni kama nimekulia ndani ya Chadema nikishiriki katika nafasi mbalimbali za ndani ya chama, nakuhakikishia kama kuna chama kinasigina katiba basi CHADEMA ni namba moja…kumbuka namna mbowe na wenzake walivyokinyofoa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama ili kimpe yeye nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kudumu, na kumbuka siku tu niliyoanza kuhoji kuhusu hilo nilivyofurumushwa kama kuku pori’’. Anaongeza Mwigamba huku akicheka

Mwigamba anaendele kusema kuwa mara baada ya mbowe kuchukua kijiti cha uenyekiti wa chama hicho alijidhatiti kuhakikisha chama hicho kinakuwa na agenda ya kuisimamia ili kipate kuaminiwa na wananchi na hatimaye kupewa dola jambo ambalo chadema ilifanikiwa kwa kujitanabaisha wazi kuwa wao ni watetezi wa rasilimali za nchi na wapinga ubadhilifu na ain azote za ufisadi.

anasema aliwahi kusimuliwa kisa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe kuhusu chanzo chama hicho kushikilia ajenda ya kupiga vita ufisadi ambapon alimwambia kuwa mwaka 2004 baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti taifa alialikwa kwenye mikutano mikuu ya vyama vya Republican na Democrats vya Marekani alipokutana na Mwanasheria Kivuli aliyetokana na chama cha Democrats wakati huo Republican ikiwa inaongoza nchi chini ya Rais George Bush na mwanasheria huyo kumweleza Mbowe kwamba haijalishi chama kina sera nzuri kiasi gani, lazima kiaminiwe na wananchi.

Aidha mwigamba anasimulia zaidi kuwa mwanasheria huyo alimweleza mbowe kwamba ameishi Tanzania kwa vipindi tofauti na katika kufanya kazi zake na utafiti aligundua kwamba nchi ilikuwa inapoteza pesa nyingi kupitia ufisadi na kumwambia Mbowe kwamba kama nchi ikifanikiwa kuzuia pesa zinazopotea kwa ufisadi, haitahitaji tena kuwa na bajeti tegemezi kwa mataifa ya nje na kumshauri kuangalia vitabu vya taarifa za Mdhibiti na MKaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anazozitoa kila mwaka ataona pesa nyingi zinavyopotea na huo ndio ukawa mwanzo wa Mbowe wakati huo akiwa mbunge wa Hai, kuanza kuzunguka mikoani akiambatana na wabunge wengine wa CHADEMA ya wakati huo ambao ni Marehemu Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Dr. Willibrod Slaa (Karatu), Dr. Amani Walid Kabourou (Kigoma mjini) na Grace Kiwelu (Viti maalum) kuelezea mapungufu waliyoyaona wakiwa na ripoti za CAG wakiwaeleza wananchi jinsi ufisadi ulivyokuwa unatafuta mabilioni ya pesa za watanzania maskini.

‘’Huo ndio ukawa mwanzo wa CHADEMA kushikilia ajenda hiyo ya ufisadi mpaka wakaingia nayo kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo Mbowe aligombea urais na kushindwa na Jakaya Kikwete lakini wakapata wabunge watano wa kuchaguliwa na sita wa viti maalum. Ni uchaguzi huo ndio uliowaleta bungeni akina Zitto Kabwe, Halima Mdee na wenzao na hoja ya ufisadi ikawa ni hoja hasa’’. Anaendelea Mwigamba

Mwigamba anasema kuwa Mbowe alimwambia kwamba waliamua kwenye kamati kuu kwamba kabla ya wabunge wao hawajaenda bungeni, chama kiwe kimefanya utafiti na kuvumbua madudu ya ufisadi ili wanapoenda bungeni wayasimamie hayo na ndio zama zilizoibuka kashfa ambazo majina yake yamebaki kwenye kumbukumbu za watanzania kashfa kama za Meremeta, Deep Green, EPA, Richmond, Buzwagi, na nyinginezo

“Ajenda hiyo ikaipelekea CHADEMA kuwa maarufu sana nchini kiasi cha uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa akagombea urais na kuchuana vikali na Kikwete. Ingawa hakushinda, chama kilichupa kutoka wabunge watano wa majimbo mpaka 23 na baadaye 24, na kutoka wabunge 6 wa viti maalum mpaka 25. Chama kikawa maarufu kiasi cha kufikiriwa kuingia madarakani mwaka 2015. Mbowe alirudia kunihadithia kisa cha huyo mwanasheria kivuli wa kimarekani mara pili tukiwa Karatu mwaka 2012 akitamba juu ya kuutumia vizuri ushauri wa mwanasheria huyo”, anasema Mwigamba.

Mwigamba anasema kwa kipindi kirefu chama hicho kilifanikiwa kujijengea sura ya kuwa watetezi wa Rasilimali za nchi na waoinga ufisadi wakiwa nje lakini wanapokuwa ndani ya chama wanakuwa na madudu makubwa hasa yanayohusu matumizi ya fedha hasa zinazotokana na ruzuku na hivyo kusababisha mitafaruku mikubwa miongoni mwa wananchama na viongozi wao kama ile iliyowahusisha Mbowe na Marehem Chacha Wangwe, na huu wa karibuni baina ya Mbowe na Zitto kabwe ulioishia kwa Zitto kufukuzwa uanachama na hatimaye kutimkia ACT WAZALENDO

“Lakini ndugu mwandishi hebu rejea mwaka 2013 uone Mbowe alivyofanya juhudi kubwa kuvuruga chama kwa matayarisho ya kuja kumpokea yule waliyempachika nembo ya ufisadi. Walianza na Zitto, Kitila na mimi wakamalizia kwa Slaa 2015 na gia ikawa imebadilishiwa angani. Muulize leo Mbowe kuhusu ushauri wa yule mmarekani na wapi wameipotezea ajenda yao ya ufisadi mpaka wananchi wanakosa Imani na chama chao, atakuambia alibadilisha gia angani’’. anasema

‘’alibadilisha gia angani akamchukua Lowassa ambaye Lema alisema kumzomea fisadi kama Lowassa ni heshima kwa Mungu, Msigwa akasema anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili, Lissu akasema CCM wamempa fomu ya kugombea urais fisadi anayetakiwa kuwa gerezani. Leo Nyalandu anaenda kujiunga na chama cha kubadilishia gia angani!!!? ameshajua Mbowe 2020 akibadilisha gia angani ataelekeza wapi chama?” anahoji Mwigamba huku akicheka kwa utani.

‘’huwezi kuwaelewa chadema kama ni popo au ndege, mchana wanasimamia hili, jioni lile basi ilimradi tu…hebu ona mbowe alivyokuwa anasema Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA…leo amebanwa nayeye kwenye madili yake amegeuka anasema Magufuli dikteta/…hakuna Dikteta katika siasa za Tanzania kumzidi Mbowe nakuambia mimi, chadema wanalijua hilo na UKAWA halikadharika’’.

‘’akigeuka huku anaona waliojihusisha na ufisadi wanapukutishwa kutoka serikalini, akigeuka anaona utumishi wa umma unavyorejea kwenye uadilifu na uchapakazi, miradi ya maji inatekelezwa hata iliyolala kwa miaka, miradi ya barabara za juu iliyohubiriwa kwa miaka inaanza, reli ya standard gauge iliyoishia kusemwa midomoni kwa karne inanyanyuka, miradi ya umeme, nk, akaona hapo hana jinsi, akasema rais anatekeleza ilani ya CHADEMA’’. Anaendelea Mwigamba

‘’ Mbowe na CHADEMA yake walipoona rais anawashughulikia mpaka wale waliowachangia wao pesa za kampeni na hatimaye kumgusa Mbowe mwenyewe kwa ufisadi mkubwa aliolifanyia shirika la nyumba la taifa kwa makumi ya miaka, hali yao ikawa ngumu vijana wa mtaani wanasema siku hizi vyuma vikakaza, wakaanza kusema rais anavunja sheria na hatimaye wakaibuka na udikteta’’. Mwigamba anaongeza

Tukio jingine alilolibainisha Mwigamba ni la Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye.

’’ Ni Sumaye huyu huyu aliyeshambuliwa sana na Mbowe na CHADEMA yake miaka ya 2000 pale wafanyabiashara wasio wana CCM walipolalamika kunyanyaswa na mamlaka ya serikali hususani TRA. Sumaye akaibuka na kusema,…. Kama mfanyabiashara unataka mambo yako yakunyookee, tundika bendera ya CCM kwenye biashara yako…. Walimtukana Sumaye kila matusi na kuonyesha anavyotumia vibaya madaraka ya uwaziri mkuu lakini leo Sumaye ni nguzo kuu kwenye CHADEMA’’.

‘’Hauwezi kuwa na akili timamu halafu uwaamini chadema si unakumbuka Kwenye uchaguzi wa 2015 kimsingi Sumaye ndiye alikuwa mpiga zumari mkuu na sasa ni mmoja wa watu wanaopigiwa upatu ndani ya CHADEMA kugombea urais 2020 mtu aliyekaa kwenye uwaziri mkuu kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote lakini anayeongoza kwa kukosa alama hata moja aliyoiacha eti leo agombee urais!!!? Hiyo ndiyo CHADEMA’’. Anazidi kueleza

“Mtazame hata huyuNyalandu mwenyewe. Angalia clip ya video ya Joshua Nassari bungeni, angalia tweets za Mch. Msigwa na Halima Mdee. Hivi hawaoni hata aibu mtu ambaye haijapita hata miaka mitatu tangu mmwite majina ya kila aina (mshika makalio ya mabinti askari wa wanyamapori, mtalii wa kutumbua kodi za watanzania na wasanii Marekani, fisadi wa hati za rais za uwindaji, nk) leo mnamwita kamanda, jembe, mara dume, mmh!”

Mwigamba anawapa pole sana wale wote wanaokimbilia CHADEMA na wale wanaojiandaa kufanya hivyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020.

''Kama ni mafisadi waende maana kwenye seerikali ya Magufuli hamna namna ya fisadi kusurvive. Ni sawa na kumwambia mwenye dhambi asurvive mbele ya nuru ya Mwenyezi Mungu. Haiwezekani. Wa namna hiyo watangulie tu CHADEMA ndiko kwenye ngome mpya ya mafisadi. Lakini wale walio waadilifu wanaodhani kule ni kimbilio, wamuulize Dr. Slaa atawasimulia vizuri zaidi. CHADEMA mchana unaweza kuwaona malaika safi toka mbinguni na usiku ukakuta ni mashetani wenye mapembe kabisa!''. alimalizia

SOURCE. JAMVI LA HABARI
Wazungu wanasema Ignorance is a bliss...yan hapa kinachomsumbua Mwigamba ni ujinga na kukosa maarifa, hafahamu kuwa yeye ndiye ndumilakuwili aliyehama vyama vi3 hadi sasa ndani ya kipindi kifupi tu!
 
angeeleweka kama angetaja majina ya mafisadi walioko ccm kwa sasa sio mtu akishatoka ccm ndio tunaambiwa fisadi,huo ufisadi ameufanya lini?
 
KWAN AKITAJA MAFISADI YALIYOKO CHADEMA KWA SASA KUNA TATIZO?
 
Hongera samson,'sizitaki hizi ni mbichi',kazana ukuu wa wilaya na vyeo vingine kwako vipo mlangoni mwako, ongeza bidii
 
Wazungu wanasema Ignorance is a bliss...yan hapa kinachomsumbua Mwigamba ni ujinga na kukosa maarifa, hafahamu kuwa yeye ndiye ndumilakuwili aliyehama vyama vi3 hadi sasa ndani ya kipindi kifupi tu!
wALIOHAMA VIWIILI KINA lOWASA NDIO WANA MAARIFA?
 
Kwa hiyo unataka kusema waliohama CCM kina Lowasa,Sumaye,Kingunge,Masha na Nyarandu wanasumbuliwa na njaa kwenye tumbo?
Ni halali kuhamia cdm lakini ni haramu kuhama cdm. Hizo ndiyo akili za nyumbu wa cdm
 
Mbona kama vile ana matatizo? Why CHADEMA everytime??
Usipoisema CHADEMA utaonekana hujafanya kazi iliyokupeleka ccm.
Hawana hoja, wakihojiwa wanatuma polisi badala ya kujibu hoja. Nyalandu ametoa sababu 6 zilizomfanya ajiondoe ccm, hawajajibu hoja hizo mpaka leo. Zoidi wanamwita fisadi.
 
Mimi sijasema.sijaelewa, bali sijaona jipya. Na kwa nini unasema "walituaminisha? Ina maana nyie hamna uwezo kuona jambo na kutambua wenyewe? Na huko ACT mliaminishwa nini ambacho mmegundua siyo kweli!!! Na huko CCM mnasuburi kuaminishwa nini tena ambacho hamjawahi kukiamini?
mkuu chanzo cha imani ni kusikia na kuona. kwa maana hiyo unaaminishwa kwa kusikia au kuona. sasa hawa chadema walituaminisha au kutuonesha uongo. ndio maana waliempachika jina la fisadi ndo akawa mgombea tena wa bila kupingwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom