Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Arusha, Samson Mwigamba, ambaye amesimamishwa kwa muda usiojulikana, ameelezea namna uongozi wa juu wa chama hicho, unavyobagua watu wa kuwaadhibu wakati wa kutoa maoni kuhusu chama.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mwigamba pia alikiri kutoa maoni katika mtandao wa Jamii Forum, huku akificha jina lake, akiwasiliana na wanachama wenzake.

Alisema kwa sasa ni vema uongozi uliopo upumzike na kuwaachia wengine, kama walivyofanya viongozi wote waliotangulia. Alisisitiza kwamba alimaanisha alichokiandika na alikuwa habahatishi.

Alitaka wanachama wenzake, waelewe kuwa ni kawaida kiongozi akiwa na maoni yanayohusu mambo ya ndani anayotaka wanachama wenzake wayapate bila kuhusisha cheo chake, huchagua njia yoyote ambayo ataona inafaa, ikiwa ni pamoja mitandao ya jamii kwa kuficha jina lake.

Kawaida hiyo kwa mujibu wa Mwigamba, imetokana na Katiba ya Chadema, kukataza viongozi kutoka hadharani na kuzungumza mambo ya chama, badala yake watumie vikao. Hata hivyo, kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye amewahi kufanya kazi makao makuu ya Chadema, vikao hivyo vimeshindwa kushughulikia udhaifu wa uongozi kwa kuwa kila anayejaribu kuhoji, hutangazwa kuwa msaliti wa chama.

"Ni wajumbe wachache sana kwenye Kamati Kuu kwa mfano ambao bado wanaweza kusimama kidete na kukosoa uongozi, watu hao hawazidi watatu au wanne, ambao ni Dk Kitila Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, Mzee Shilungushela (amemtaja kwa jina moja) na mzee Sgerembi ambaye sasa ni marehemu," alisema Mwigamba.

Alisisitiza kuwa viongozi wengi ndani ya Chadema, wana majina yasiyojulikana kwenye mitandao ya jamii na huyatumia kuzungumza na wanachama mambo mengi, ambayo hawataki yahusishwe na vyeo vyao na mambo hayo hubaki kuwa maoni ya mwanachama binafsi.

Alisema kama angetoka kwenye vyombo vya habari na kujitambulisha na kuanza kuzungumza yale aliyoandika, viongozi wangekuwa na haki ya kumshitaki kwenye mamlaka yake ya nidhamu.

Lakini, alidai hakuna mtu yeyote awe mtaalamu wa Teknolojia ya Habari, au vyovyote vile, mwenye haki ya kwenda kwenye mtandao na kuanza kutafuta anuani kufahamu kilichoandikwa kimetoka kwenye kompyuta gani au nani katuma.

Aliutaka uongozi huo, ueleze wanaofanya kazi ya kufuatilia kila mtu anayetoa maoni kuhusu chama katika mtandao, wametumwa na nani? "Je wanachunguza na kuingilia mawasiliano ya watu wameajiriwa na nani na kazi hiyo wameianza lini na wameshapata watu wangapi?" Alihoji.

Alisema hata kama wameanza kazi hiyo Ijumaa iliyopita na mtu wa kwanza kumpata akawa yeye, wamueleze baada tu ya tukio hilo, wameshapata wengine wangapi, maana bado viongozi wengine wanaendelea kufanya kama alivyofanya yeye.

"Au kuna mtu ama watu fulani ndani ya chama, ukiwagusa tu ndio unatafutwa au kuitwa msaliti wa chama?" Alihoji.

Alisema miezi kadhaa iliyopita, kuna viongozi walijitokeza katika mitandao na kueleza kwa kurudia rudia udhaifu wa viongozi wa chama, akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto lakini hivi sasa mmojawapo kati ya watu waliosemwa sana kupitia mtandao huo (hakumtaja jina), amepandishwa cheo na kuwa Ofisa wa Makao Makuu ya chama hicho.

"Siku zijazo tutakuwa na madikteta ambao watatumia demokrasia kujihalalishia utawala wa milele ndani ya vyama vyao na hata ndani ya nchi na ikiwezekana kurithishana utawala kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto, mtoto kwenda mkwe kama ilivyo sasa," alisema huku akisisitiza kuwa alichoweka katika mtandao alimaanisha Katika mtandao Mwigamba alimpongeza Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kufanya mengi katika chama hicho.

Alitaja baadhi kuwa ni pamoja na kutoa chama kutoka kuwa cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.

"Kakichukua kikiwa na wabunge watano bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10, kina wabunge 49. Ni mafanikio makubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake Chadema imebeba ajenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa rasilimali, Katiba mpya na kadhalika," alisema.

Hata hivyo, alisema kuna matatizo yameanza kujitokeza na wanachama wasipochukua hatua haraka, huko mbele watapata shida kubwa. Alimtaka Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo, asitake kulazimisha kusonga mbele, akidhani bila yeye hakuna Chadema.

"Akiache chama kikiwa salama, abaki kama Mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao," sehemu ya andiko hilo la Mwigamba ilieleza.

Chanzo:Habari leo.
 
Ulaghai kisiasa ni nguzo dhaifu sana katika mazingira ya siasa endelevu.

CHADEMA kilianzishwa kilaghai na kwa maana hiyo lazima uwe mlaghai kuweza kuwa kiongozi endelevu ndani yake, ndiyo maana wale walaghai ndiyo wanapandishwa vyeo na wasio walaghai wanatapata msukosuko mpaka uongozi wao utakoma.

Samson Mwigamba uzalendo ulimshinda ndiyo maana akaamua kutoa sauti kwa watanzania kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku na vyenzo zingine zitokanazo na pesa za wananchi ambazo zinatumiwa isivyostahili kikanuni na kikatiba na baadhi ya genge la watu wanaokifanya chama kama personal investment lakini kibaya kabisa watu waliojimilisha chama hawakupenda mtu wa Magu kuwa kiongozi wa eneo lao Arusha.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

Chama kilichojengwa kwa misingi ya kilaghai hata uendeshaji wake utakuwa niwa kilaghai.

Waliojimilikisha chama baada ya kugundua kuwa hawana uwezo wa kushinda katika chaguzi za ndani wameamua kuahirisha chaguzi na sasa wanakuja na sababu wakisema kwa mujibu wa katiba, uchaguzi unatakiwa kufanyika 2014 kama vile hawakufahamu wakati wanasema uchaguzi utafanyika 2013.

Hawawezi kushinda katika mapambano yao ya kilaghai kwa sababu ulaghai siku zake ni arobaini na kikubwa zaidi, Watanzania wanafahamu ulaghai wao.

Waacheni wafu wazikane.
 
wakuunatumaini yeye ni mjumbe wa halmashauri kuu kwa nini hakutumia nafasi yake ndani ya chama kuandika barua na kuipeleka mwenyekiti akitoa malalamiko yake ahdi kuja hapa JF na kuanza kulalamika.Ndo Maana kuna maadili na Miiko ya uongozi ukienda kinyume nayo lazima utaonekana hufai kwa jamii.Kimsingi lazima kuwepo na matumizi ya nguvu kidogo ili kupushi maendeleo.Nchi za wenzetu wametumia nguvu na udikteta hadi wamefanikiwa hii kitu inaitwa demokrasia nadhani inahitaji kuangaliwa tena.
 
Ni kweli Chadema kuna ubaguzi. Ukiwa msaliti ni lazima wakubague. Naona hilo ndilo alilotakiwa kulisema sio bla bla anazoleta baada ya kuchezea kichapo cha usaliti humu. Nadhani wewe gamba uliyeleta ushuzi huu umenipata.
 
Ulaghai kisiasa ni nguzo dhaifu sana katika mazingira ya siasa endelevu.

CHADEMA kilianzishwa kilaghai na kwa maana hiyo lazima uwe mlaghai kuweza kuwa kiongozi endelevu ndani yake, ndiyo maana wale walaghai ndiyo wanapandishwa vyeo na wasio walaghai wanatapata msukosuko mpaka uongozi wao utakoma.

Samson Mwigamba uzalendo ulimshinda ndiyo maana akaamua kutoa sauti kwa watanzania kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku na vyenzo zingine zitokanazo na pesa za wananchi ambazo zinatumiwa isivyostahili kikanuni na kikatiba na baadhi ya genge la watu wanaokifanya chama kama personal investment lakini kibaya kabisa watu waliojimilisha chama hawakupenda mtu wa Magu kuwa kiongozi wa eneo lao Arusha.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

Chama kilichojengwa kwa misingi ya kilaghai hata uendeshaji wake utakuwa niwa kilaghai.

Waliojimilikisha chama baada ya kugundua kuwa hawana uwezo wa kushinda katika chaguzi za ndani wameamua kuahirisha chaguzi na sasa wanakuja na sababu wakisema kwa mujibu wa katiba, uchaguzi unatakiwa kufanyika 2014 kama vile hawakufahamu wakati wanasema uchaguzi utafanyika 2013.

Hawawezi kushinda katika mapambano yao ya kilaghai kwa sababu ulaghai siku zake ni arobaini na kikubwa zaidi, Watanzania wanafahamu ulaghai wao.

Waacheni wafu wazikane.

Acheni ufala nyie kama kuna ubaguzi mwambie aende CCM au CHAUSTA vyama vipo vingi PPT MAENDELEO mmeng'ang'ania CHADEMA kufanya nini wakati mnaita walaghai?
 
Ulaghai kisiasa ni nguzo dhaifu sana katika mazingira ya siasa endelevu.

CHADEMA kilianzishwa kilaghai na kwa maana hiyo lazima uwe mlaghai kuweza kuwa kiongozi endelevu ndani yake, ndiyo maana wale walaghai ndiyo wanapandishwa vyeo na wasio walaghai wanatapata msukosuko mpaka uongozi wao utakoma.

Samson Mwigamba uzalendo ulimshinda ndiyo maana akaamua kutoa sauti kwa watanzania kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku na vyenzo zingine zitokanazo na pesa za wananchi ambazo zinatumiwa isivyostahili kikanuni na kikatiba na baadhi ya genge la watu wanaokifanya chama kama personal investment lakini kibaya kabisa watu waliojimilisha chama hawakupenda mtu wa Magu kuwa kiongozi wa eneo lao Arusha.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

Chama kilichojengwa kwa misingi ya kilaghai hata uendeshaji wake utakuwa niwa kilaghai.

Waliojimilikisha chama baada ya kugundua kuwa hawana uwezo wa kushinda katika chaguzi za ndani wameamua kuahirisha chaguzi na sasa wanakuja na sababu wakisema kwa mujibu wa katiba, uchaguzi unatakiwa kufanyika 2014 kama vile hawakufahamu wakati wanasema uchaguzi utafanyika 2013.

Hawawezi kushinda katika mapambano yao ya kilaghai kwa sababu ulaghai siku zake ni arobaini na kikubwa zaidi, Watanzania wanafahamu ulaghai wao.

Waacheni wafu wazikane.

mWANAdIWANI nafikiri hizi habari zimekusaidia kufikisha lengo lako! lkn kumbuka si muda mrefu utafahamu maana yake na wala usichekuanza kubadirisha kauli zako!!
 
Hivi alichokizema yeye... WA CCM anaweza kusema dhidi ya VIONGOZI wakuu wa CCM? Kwanini ni kwa CHADEMA tu ndio VIONGOZI wakuu ni Wabaguzi? hawa ea CCM pia... Umejaribu kugombea U-NEC ndani ya CCM? kama haujulikwani na ukatoa hotuba nzuri watakubagua kwasababu wewe sio kwenye KUNDI LAO - A CULT WITHIN

Sasa where is the beef???
 
Ni kweli Chadema kuna ubaguzi. Ukiwa msaliti ni lazima wakubague. Naona hilo ndilo alilotakiwa kulisema sio bla bla anazoleta baada ya kuchezea kichapo cha usaliti humu. Nadhani wewe gamba uliyeleta ushuzi huu umenipata.

Ndugu Bagaile,tumwulize swali lingine kwamba kama CHADEMA kina ubaguzi,ilikuaje akawa mtunza hazina wa Kitaifa wa Chadema.Tena ilikuaje akawa mwenyekiti wa chadema wa mkoa wa arusha?
 
Kwa hili lililotokea ndani ya chadema, kwa kweli ni aibu ya chama, tunawafundisha nini watanzania? Bado natafakari sana juu ya kile kilichotokea huko Arusha!
 
Lini mtatekeleza ilani yenu naona kila siku ni Slaa, Mbowe Chadema tuuuuu

mtatekeleza lini ilani yenu au mnadhani mko salama,

Watch out Mkiti wenu kasema mkicheza ataondoka madarakani na CCM.
 
Sasa si aende huko ambako hakuna ubaguzi au ukanda au hakuna kupigwa au hakuna wasaliti anachosubiri na kulalamika ni nini.
Na swali jingine kwani chama ni CDM tuu kuna vyama vingi kuna CCM kuna NCCR kuna TLP aende huko hakuna ubaguzi wala maneno mengi mbona anang'ang'ania tuu hapa na kutoa matamko mengi na wanamshabikia na kumuanzishia thread ni wale wale waliotuma kufanya kazi yake
 
Lini mtatekeleza ilani yenu naona kila siku ni Slaa, Mbowe Chadema tuuuuu

mtatekeleza lini ilani yenu au mnadhani mko salama,

Watch out Mkiti wenu kasema mkicheza ataondoka madarakani na CCM.

Mkuu Feedback hilo hawawezi kujibu maana kila siku wakiamka ni Slaa au Mbowe au Zitto au Mnyika mpaka wanatuchosha tusio na vyama maana wanaacha mambo ya msingi imebaki ni kujadili watu na vyama tuu
Kila siku ni CDM na CCM mbona NCCR au TLP au UDP au CUF haizungumzwi au wale wasio na vyama au wasio wafuasi waende wapi
Kwa nini msizungumzie matatizo ya wananchi wanaokosa huduma muhimu au wanaokabiliwa na njaa na umaskini wa kutupwa kila siku ni vyama tuu na watu binafsi na maisha yao
 
Last edited by a moderator:
Ulaghai kisiasa ni nguzo dhaifu sana katika mazingira ya siasa endelevu.

CHADEMA kilianzishwa kilaghai na kwa maana hiyo lazima uwe mlaghai kuweza kuwa kiongozi endelevu ndani yake, ndiyo maana wale walaghai ndiyo wanapandishwa vyeo na wasio walaghai wanatapata msukosuko mpaka uongozi wao utakoma.

Samson Mwigamba uzalendo ulimshinda ndiyo maana akaamua kutoa sauti kwa watanzania kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku na vyenzo zingine zitokanazo na pesa za wananchi ambazo zinatumiwa isivyostahili kikanuni na kikatiba na baadhi ya genge la watu wanaokifanya chama kama personal investment lakini kibaya kabisa watu waliojimilisha chama hawakupenda mtu wa Magu kuwa kiongozi wa eneo lao Arusha.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

Chama kilichojengwa kwa misingi ya kilaghai hata uendeshaji wake utakuwa niwa kilaghai.

Waliojimilikisha chama baada ya kugundua kuwa hawana uwezo wa kushinda katika chaguzi za ndani wameamua kuahirisha chaguzi na sasa wanakuja na sababu wakisema kwa mujibu wa katiba, uchaguzi unatakiwa kufanyika 2014 kama vile hawakufahamu wakati wanasema uchaguzi utafanyika 2013.

Hawawezi kushinda katika mapambano yao ya kilaghai kwa sababu ulaghai siku zake ni arobaini na kikubwa zaidi, Watanzania wanafahamu ulaghai wao.

Waacheni wafu wazikane.

Sumu ya CHADEMA ni mtu anayetaka UWAZI.
 
Mkuu Feedback hilo hawawezi kujibu maana kila siku wakiamka ni Slaa au Mbowe au Zitto au Mnyika mpaka wanatuchosha tusio na vyama maana wanaacha mambo ya msingi imebaki ni kujadili watu na vyama tuu
Kila siku ni CDM na CCM mbona NCCR au TLP au UDP au CUF haizungumzwi au wale wasio na vyama au wasio wafuasi waende wapi
Kwa nini msizungumzie matatizo ya wananchi wanaokosa huduma muhimu au wanaokabiliwa na njaa na umaskini wa kutupwa kila siku ni vyama tuu na watu binafsi na maisha yao

Mgogoro wa CHADEMA ni wa wanachadema, wengine ni watazamaji tu na wala msitafute mchawi kwingine. MBOWE na SLAA wakubali tu wameshindwa kutokana na uchu wa madaraka na Ubinafsi na hivyo wakae pembeni wengine wakivushe chama kutoka hapo kinapotaka kuzamia.
 
Kwa hili lililotokea ndani ya chadema, kwa kweli ni aibu ya chama, tunawafundisha nini watanzania? Bado natafakari sana juu ya kile kilichotokea huko Arusha!

chadema mpango wa Mungu namna alivyo kamatwa msaliti Arusha inajizihilusha kuwa chadema ni mipango ya Mungu..
 
Back
Top Bottom