GE2025 Samia: Tutajenga soko la kisasa na maghala ya chakula Mbogwe

GE2025 Samia: Tutajenga soko la kisasa na maghala ya chakula Mbogwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
gombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa ikiwa wananchi watampa ridhaa miaka mitano ijayo, Serikali yake itajenga maghala ya kuhifadhia mazao pamoja na soko la kisasa Wilayani Mbogwe mkoani Geita, ili kusisimua biashara na kilimo.

Samia ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 12, 2025 kwenye Mji mdogo wa Masumbwe wakati aliposimama kusalimia na kuomba kura kwa wananchi wa eneo hilo, akiwa njiani kutokea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake.

Ameahidi pia kuanza ujenzi wa barabara ya Masumbwe-Kasosobe, kuelekea makao makuu ya wilaya hiyo, barabara yenye urefu wa kilomita 45 na itakayojengwa kwa kiwango cha lami, ili kuondoa adha ya usafiri na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji katika wilaya hiyo.
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
 
Back
Top Bottom