Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, Septemba 24, 2025 aliwasimulia wananchi wa Mtama, mkoani Lindi, namna alivyoingia Kamati Kuu ya chama hicho baada ya kukutana na baba yake Nape Nnauye.
“Lakini mama huyu ana mwanawe anaitwa Nape Nnauye… ngoja niwapeni hadithi kidogo,” alisema Samia.
''Nilipoingia mara ya kwanza Kamati Kuu, nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu, nikaingia Kamati Kuu. Tulipoingia, tukamkuta Mzee Nnauye yuko ndani ya Kamati Kuu. Sasa sisi tumeingia si vichinchili, tuko pale, basi Mzee anazubaa anatuangalia tu, anasema, ‘eeh! Karume kaleta haya mapapai haya!’''
Samia aliongeza kwa utani kwamba, “Kwahiyo, ningezubaa kidogo ndiyo hivyo tena… Kwahiyo Nape mwanangu jamani!”