GE2025 Samia: Mkituchagua tutamaliza tatizo la umeme hafifu

GE2025 Samia: Mkituchagua tutamaliza tatizo la umeme hafifu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Kuna muda unasikiliza sera za CCM unaweza kudhani kuwa kwa miaka 60 iliyopita nchi ilikuwa chini ya CHADEMA au chama kingine

Sasa suala la umeme

=====================

Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa ndani ya miaka mitano ijayo ikiwa watanzania watampa ridhaa ya kuongoza serikali, vitongoji vyote 423 vya wilaya ya Nyasa vitapata huduma ya umeme.

Wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo kwenye mkutano wake wa kampeni Mbamba Bay leo Jumapili Septemba 21, 2025, Dkt. Samia amesema hatua hiyo inafuatia serikali ya awamu ya sita kuwa imeshafikisha umeme kwenye vijiji vyote vya Nyasa,

"Ninafahamu kwamba Nyasa huku kuna changamoto ya umeme kuwa mdogo na niwaambie tutajenga kituo cha kupooza umeme, kipokee umeme kutoka Songea, uingie hapa Nyasa usambaze na hiyo itaondoa tatizo la umeme kuwa mdogo na ndipo tutakapovuta zaidi wawekezaji." Amesisitiza Dkt. Samia.


 
Back
Top Bottom