Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wafuasi wa chama hiko kujitokeza kupiga kura siku ya Oktoba 29, 2025, na kuwahakikishia kuwa hakutakuwa na maandamano zaidi ya maandamano ya kwenda vituoni kupiga kura.
"Niwahakikishie tarehe 29, kesho kutwa tu mwezi huu wa 10, niwaombe tokeni muende mkapige kura. Ninayeongea hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii, ninataka niwaambie, maandamano yatakayokuwepo ni ya watu kwenda vituoni kupiga kura, hakuna maandamano mengine yatakayokuwepo hapa, hakuna tishio la kiusalama litakalokuwepo, anayesema ni Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi hii. Niwaombe ndugu zangu, twendeni mkapige kura, twendeni mkapige kura... Ndugu zangu mengine niachieni mimi, matusi niachieni mimi, ninayabeba kwa niaba yenu"
Samia ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kinondoni, Dar es Salaam.