GE2025 Samia: Jimbo la Rais halitakiwi kuwa na shida yeyote ile

GE2025 Samia: Jimbo la Rais halitakiwi kuwa na shida yeyote ile

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuimarisha zaidi huduma za kijamii katika Jimbo la Chamwino ikiwa ni pamoja na afya, maji na barabara.

Akizungumza Agosti 31, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Chamwino, mkoani Dodoma, Dkt. Samia amesema serikali ya CCM ina dhamira ya kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo, ambalo pia ndilo lina Ikulu ya Rais, hawakabiliwi na changamoto za huduma za msingi.

“Niwaahidi kuwa tutakuja kuongeza vituo vya afya, vituo vya afya 10 na zahanati nyingine tano. Jimbo la Rais halitakiwi kuwa na shida yoyote ile, kwahiyo tutakuja kuongeza,” amesema Dkt. Samia na kuongeza,

“Ninajua tuna shida ya maji, mgombea ubunge hapa amesema mradi mkubwa upo, ninataka niwahakikishie tutahakikisha Chamwino yote inapata maji kwa karibu zaidi.”

Aidha, ameahidi kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara, akisema serikali itajenga kilomita 10 za barabara za kiwango cha lami na kuimarisha barabara za changarawe katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
 
Maji, barabara, umeme, afya na elimu😅😅😅😅 hiyo ni FUTUHI
 
Back
Top Bottom