tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Rais Samia Suluhu Hassan amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni, akiwemo Amos Makalla aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ili kuanza rasmi majukumu yao mapya katika utumishi wa umma nchini.
Katika hafla hiyo ya uapisho iliyofanyika Ikulu jijini Dodoma leo Agosti 26, 2025 Rais Samia ametaja sifa zilizombeba Mkalla katika uteuzi huo, mojawapo ikiwa ni utumishi uliotukuka aliouonesha akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Soma pia: Makalla: Profesa Kitila Mkumbo ni hazina kubwa kwa Chama na Taifa
“Amos Makalla umekuwa kiongozi mzuri, kwa muda mfupi umeongoza kwa mafanikio makubwa kwa kukiunganisha chama chetu, sasa tumekuongezea jukumu jipya nenda kafanye kazi kwa uaminifu mkubwa,” amesema Rais Samia.
Mkuu huyo wa nchi ameweka wazi kuwa, Mkoa wa Arusha umepewa kipaumbele katika ujenzi wa miradi ya kimkakati katika kuvutia uwekezaji na utalii hivyo inahitaji uongozi imara akimwagia sifa Makalla kuwa anazo sifa za kutimiza lengo hilo.
Mbali na Mkuu huyo wa Mkoa, Makalla, viongozi wengine walioapishwa katika hafla hiyo leo ni Khatib Kazungu, ambaye ameteuliwa na kuapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, pia ameagizwa kwenda kumsaidia Mkuu wa Mkoa huo kutimiza malengo ya Serikali katika kujenga mji huo.