Sambusa Zapigwa Marufuku Somalia

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
5850518.jpg

Kundi la wanamgambo la Al-Shabbab ambalo linatawala baadhi ya maeneo ya Somalia limetangaza kupiga marufuku kupika, kuuza au kula sambusa kwakuwa sambusa zimekaa kikristo zaidi.Kundi la Al-Shabbab ambalo linajulikana zaidi kwa sheria kali linazoziweka nchini Somalia likidai ni katika misingi ya dini ya Kiislamu, limekuja na sheria mpya kwa kupiga marufuku Sambusa.

Sambusa ni miongoni mwa vitafunwa maarufu duniani vyenye umbile la pembe tatu, kukiwa na sambusa za aina mbalimbali, sambusa za nyama, mbogamboga na sambusa zenye kuwekwa mahanjumati mbalimbali ili ladha yake iwe nzuri.

Umbile la pembe tatu la sambusa ndilo lililopelekea sambusa zipigwe marufuku nchini Somalia.

Wanamgambo wa Al-Shabbab walipita mitaani wiki iliyopita wakiwa kwenye magari yenye spika na kutangaza kuwa kuanzia sasa sambusa zimepigwa marufuku nchini Somalia.

Kundi la Al-Shabbab halikutoa sababu yoyote ya kuzipiga marufuku sambusa mbali ya kusema kuwa zimekaa kimaadili ya nchi za magharibi.

Kutokana na marufuku hiyo adhabu kali itawakuta watu watakaokamatwa wakipika, kununua au kuuza au kula sambusa ndani ya maeneo yaliyo chini ya Al-Shabbab.

Hata hivyo imeelezwa kuwa sababu ya kuzipiga marufuku sambusa ni umbile lake la pembe tatu ambalo limefananishwa na umbile la alama ya kikristo ya "Utatu Mtakatifu".

Utatu mtakatifu kwenye Ukristo humaanisha Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu.

Kutokana na alama ya utatu mtakatifu kuwa kwenye umbo la pembe tatu Sambusa nazo kwakuwa zina umbile kama hilo zimepigwa marufuku kwa kuonekana zimekaa kikristo zaidi.

[/QUOTE
Na bunduki zina umbo gani?

Sijawahi kucheka kama leo
wamenikumbusha taliban.walipowacharaza bakora wachezaji wa timu ya taifa ya football
kwa kuvaa bukta

Sikuamini hii kitu, mpaka ikabudi ni tafute ukweli, ila hawa jamaa naona wamechanganyikiwa.

http://www.hiiraan.com/news2/2011/july/somalia_s_al_shabaab_militants_ban_samosas.aspx
[URL="http://www.terrorismwatch.org/2011/07/somalias-al-shabaab-militants-ban.html"]http://www.terrorismwatch.org/2011/07/somalias-al-shabaab-militants-ban.html
[URL]http://www.zambianwatchdog.com/?p=20395]Siasat.pk Forums[/URL][/URL][/URL]

Mirungi ukichanganya na bange akili inakuwa inawaza maovu tu. Wakimaliza kuzipiga marufuku sambusa nyama watapiga marufuku magari kwani ni ya wamagharibi?

mimi huwa nashangaa msimamo kama huu wa kipumbavu huku ukiwa umejikita kwenye misingi ya kidini-hao viongozi wa dini waliosimamia hilo swala nao ni wa ajabu sana-maana wanashindwa kutadadavua vitu vidogo kama hivi-wakishaanza kulinganisha vitu kama sambusa-si watajikuta kila kitu wanakifananisha-thyen kutakuwa hakuna kitu kinachofaa

Naona umefika muda muafaka wa Afrika nzima 'KUWAPIGA MARUFUKU AL-SHABAAB' na kuchukua hatua za dhati kusaidia serikali ya mpito Somalia kuwaondoa hawa jamaa ambao wanaona afadhali watu wafe kwa kutoruhusu misaada ya chakula kuwafikia.

Back
Top Bottom