duh....hii inaonyesha kiwango tulichofikia sasa na ubinafsi wetu. UFISADI ni adui numba moja wa Africa.
Tatizo nionalo mimi ni watu tumekuwa na matumizi yasiyokuwa ya lazima. Mtu mwenye msharaha wa Mil 10, bado atautumia wote, mwenye mshahara wa laki moja, atautumia wote. Na wote wataona hautoshi. Kitu tunachosahau ni kuwa yote ni kula upepo. Na ndo hapa Shetani anatukamata. Kama aliweza kumkamata Solomon na hekima yote, singali sisi? Ukiangalia kwenye tv, zimejaa matangazo kibao yanayokufanya utumie hela. Na wakati huo huo kuna watu wanakosa basic needs.
Je nani wa kulaumiwa? Serikali au sisi binafsi?