Saluni zetu(Barber shop) ni salama kiasi gani dhidi ya maambukizi ya Ukimwi?

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Kwa kweli jitihada za serekali kupambana na maabukizi ya ukimwi zimepungua tofauti na serekali ya Mh Mkapa ambapo zilionekana jitihada za dhahiri kuanzia hotuba za Raisi, matangazo, vipindi maalum vya redio na TV, matamasha n.k.
Kwa kipindi kile ilikuwa rahisi kuelimisha watu wasichangie vifaa kama nyembe na sindano maana uwepo sa salum za kisasa ulikuwa mdogo!

; Kuibuka kwa saluni za kunyolea nywele na ndevu kuna usalama gani kwa watumiaji wasipate maambukizi ikitegemewa mashine ni moja ya vifaa venye ncha Kali?
; vinyozi wa saluni hizi wana elimu ya kutosha jisnsi ya kudhibiti maabukizi zaidi?
 
Mkuu unapoenda kunyoa usiangalie gharama!hakikisha unaenda kunyoa kwenye saluni safi,hakikisha mashine unayonyolewa nayo imetoka kwenye sterilizer na imesafishwa vizuri na spirit,hakikisha taulo wanazotumia kukuoshea zinatoka kwenye towel warmer,vitu kama scrubs usiende saluni bali mfundishe mke wako akufanyie kama ni muhimu sana kwako kwakuwa uwezekana wa maambukizi ni mkubwa sana unaposuguliwa uso kwa mikono mikavu na wale wadada.ikibidi nunua mashine yako na taulo yako uwe unaenda navyo saluni.
naandika haya yote kwa kuwa nimeshashuhudia mtu aliyeathirika na VVU tena yuko hoi akinyolewa na kuoshwa then kufutwa na taulo ambayo ilitaka kutumiwa tena kwa mteja mwingine pasipo mimi kuingilia kati.
 
Ni kweli hz saluni kiasi fulani huogofya wateja...
Bahati nzuri VVU ni very unstable vikiwa nje ya host hivyo kwa kuwa nje tu ya human blood stream kunapunguza virulence yake.. Mashine ikifutwa vzr na spirit hutosha kuzuia uwekano wa maambukizi ya VVU
Ili mtu upate maambukizi kuna suala la infectious dose yaani uwepo wa kiasi fulani ya VVU ndani ya damu iliyoachwa kwenye mashine ili iweze kuwa tatizo kwa mteja anayefuata kunyolewa..
Kwa hili nashukuru MUNGU ametuepusha na mengi..
Elimu ya VVU ni ndeeeefu sana na inahitaji thread nzima ili kuondoa mashaka kwa watu na kupanua uelewa kwa wana jamvi.

Maledhi
 
Aisee UKIMWI ungekuwa unaambukizwa kama mtoa uzi anavyofikiri basi waathirika wangekuwa wengi mnoo,kweli elimu ya UKIMWI bado inahitajika saaana tu
 
naomba kuuliza hapo hivi bacteria anaeambukiza ukimwi anaweza kuishi ktk joto(moto) unaotoka ktk zile mashine??
 
Back
Top Bottom