DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Dhoruba iliyotokea sisi wengine tukasema hapana. Tukasema hapana kwasababu tunazizuia akili zetu zisitawaliwe na mihemko, tunazizuia akili zetu zijawe na sifa za kuja mbele za watu na kupigiwa makofi huku tukijua hatuna namna yoyote ya kuwasaidia watanzania, tukakataa, ndio sababu tukasema tuachane tu kwa amani. Mabadiliko ya fikra hayajawahi kuwa dhambi kwenye maisha kama fikra zenu ni hizi na zetu ni hizi basi tuachane.
Tukaamua kwenda CHAUMMA, Nako ikawa nongwa, tukiwaambia ndani mnasema sisi ni wabaya, sisi ni wasaliti, tumeshindwa, tuwaachie Chama. Tukiwaambia fanyeni hivi hamtaki. Tumeona basi sisi akili zetu tukazitekeleze kwingine, bado imekuwa nongwa. Sasa hivi adui wao sio CCM tena ni CHAUMMA, matusi, fedheha, kudhalilishana. Hiyo sio Taasisi tuliyoijenga. Kama kutofautiana ni dhambi basi hata upinzani nchi hii usingekuwepo."- Salum Mwalimu, Katibu Mkuu CHAUMMA akiwa kwenye ziara ya Chama hicho Usa River, Mkoani Arusha.
source: JAMBO TV