Salum Mwalimu ana watoto, asidhalilishwe


Joined
Dec 10, 2017
Messages
52
Likes
125
Points
40
Joined Dec 10, 2017
52 125 40
Katika uzinduzi wa kampeni za CCM, Jimbo la Kinondoni maeneo ya Biafara, walisimama watu mbalimbali, Bwana Tamim alidai kuwa yeye anatoka Zanzibar na Salum Mwalimu hivyo akadai anamjua kwa undani na anajua sababu za kwa nini hajao hadi sasa, alienda mbali na kusema kuwa mtu asiye na uwezo wa kulea familia awezaje kulea jimbo? Maneno yake ya kwamba anamjua na sababu ya kuwa hajao hadi sasa ni kuwaaminisha wapiga kura wa kinondoni kuwa sababu ya yeye kutooa hadi sasa ni kwa sababu ile nyingine ya kumfanya mwanaume asiwe na nguvu za kiume, michezo ile ya mombasa kwa ufupi.

katika hali ya kuonekana CCM wamejipanga kumshambulia kwa hilo pia Omari Kimbau, ambaye mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo la Mafia kwa tiketi ya CUF pia alimnanga Salum Mwalimu kuwa ni msela na hana familia hivyo hapaswi kupewa jukumu kubwa kama ameshindwa kukuza na kulea familia.

ili kuonyesha mgombea wa CCM ana familia na ni muwajibikaji basi mke wake na mama yake mzazi walipandishwa jukwaani na mwenezi wa CCM - Dar es Salaam, Ndugu Mwakifamba huku akichagiza kwa maneno kuwa mgombea wao Bwana Mtulia sio msela hivyo achaguliwe maana amethibitisha uwezo wa kuongoza kuanzia ngazi ya familia.

JE NI KWELI SALUM MWALIMU HANA MKE NA WATOTO?

Jambo hili lina walakini kidogo lakini kwa image ya Mwalim lazima tuliweke sawa ili kupunguza maneno na chokochoko za CCM kuwa mgombea wetu ana michezo ya kule Mombasa.

Salum Mwalimu anao watoto wawili, wa kwanza wa kike na wa pili ni wa kiume. Mazingira aliyonayo yanakuwa magumu kumpandisha jukwaani mzazi mwenzie pamoja na watoto kwa sababu mzazi mwenzie ni mke wa mtu. Hivyo inakuwa changamoto.

Naamini kuna siku atafanya hivyo , aliyezaa nae kaolewa na Mzee wa makamo hivyo ikamlazimu huyo dada ambaye ni mbunge (CHADEMA) wa jimbo kutoka mkoa wa Mara kutafuta kijana aweze kufurahia ujana wake maana damu bado inachemka, na mapenzi yao yalianzia walipokutana kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Tarime mwaka 2008 baada ya kifo cha Marehemu Chacha Wangwe.

Hivyo maneo kuwa Salum hana watoto kwa sababu ile wanayoisemea sio kweli. hapa chini nitaambatanisha picha za watoto ili muone hata wanavyofanana na baba yao.

img-20180128-wa0005-jpg.686153

Watoto waliozungushiwa na mstari kichwani ndio watoto wa Salum Mwalimu, wa kike wa pili toka kushoto na wa kwanza toka kulia.

img-20180128-wa0008-jpg.686154

Watoto wa Salum Mwalimu wakiwa na mama yao mdogo, Florence Nicholous Matiko, kushoto pamoja na dada yao mkubwa kwa mume wa ndoa wa mama yao.

HITIMISHO

Ni vyema maswali yaliyoibuliwa na wana CCM kuwa hana familia wala watoto yajibiwe kwa ufasaha la sivyo kuna kura nyingi sana zitapotea kwa watu kuaminishwa kinyume na ukweli na uhalisia uliopo.
 

Joselela

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
2,126
Likes
1,985
Points
280

Joselela

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
2,126 1,985 280
CCM huwa wanahoja za kipumbavu ndio maana tunaitwa shithole countries kwa sababu ya type ya siasa kama hizi!!

Siasa za kuchafuana kwa maana hiyo mtulia ataenda kuwakula wanakinondoni wote, ni wananchi wametukanwa kama hawana akili watamchagua ili waliwe na kutiwa!
 

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Messages
6,259
Likes
25,351
Points
280

barafu

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2013
6,259 25,351 280
Jamani Siasa hizi za kuchimbana mambo ya familia ni kukoseana adabu,mambo ya faragha na familia yabaki kuwa sehemu ya familia.Hali hii inawaumiza watoto ambao hawajui "vita" hivi vya kisiasa.

Niliposikia Mwigulu Nchemba anasema atafanya siasa za kistarabu uchaguzi mdogo Kinondoni,tulidhani wanamaanisha,kumbe ni ovyoo.

Sasa hawa watoto mnaanza kuwaanika ili tu kujibu tuhuma za Wahuni wanaoacha sera na kutukana watu?Tukianza kufukua hayo mambo wengi wataaibika.

Tutaanza kuangalia mahusiano ya kuanzia Raia Namba moja mpaka diwani,tutafukua makaburi na kusema maisha yao kabla ya vyeo vyao,halafu tutasema,hawa kama familia iliwashinda ilikuwaje tumewapa nchi?Haya mambo mengine acheni,mtasababisha watu tuongee halafu Maxence Melo aanze kusumbuliwa
 

Muyobhyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Messages
7,897
Likes
5,727
Points
280

Muyobhyo

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2014
7,897 5,727 280
yaani hawa jamaa hawajakoma tu, manake kampeni zao ni kutukana wenzao na kuwapanga, hebu waongelee matatizo ya wana kino, wawape ahadi za kuyatatua
 

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Messages
3,782
Likes
2,843
Points
280

tatum

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2018
3,782 2,843 280
Kwa maelezo ya picha ya pili inaonyesha watoto wanaishi na mama yao hivyo wanaishi na baba mwingine.Nadhani hapo Salum Mwalim alitakiwa kuishi na watoto wake hata kama watasaidiwa na house girl.Na hata jana ktk hiyo kampeni angeweza kuwa nao hao watoto hakuna sheria inayozuia kuwa na familia ktk kampeni.
 

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Messages
6,224
Likes
4,566
Points
280

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2015
6,224 4,566 280
Kwa maelezo ya picha ya pili inaonyesha watoto wanaishi na mama yao hivyo wanaishi na baba mwingine.Nadhani hapo Salum Mwalim alitakiwa kuishi na watoto wake hata kama watasaidiwa na house girl.Na hata jana ktk hiyo kampeni angeweza kuwa nao hao watoto hakuna sheria inayozuia kuwa na familia ktk kampeni.
Huu uzi umemdhalilisha Salum Mwalim na huyo Ester Matiko.
 

Forum statistics

Threads 1,204,755
Members 457,433
Posts 28,168,810