Salim, Warioba na Butiku

Kiroroma

JF-Expert Member
Feb 6, 2009
370
114
Waheshimiwa hawa wameyasema yote,lakini mbona hawasemi nini kifanyike?Na tuanzie wapi?...........Ni dhahira uongozi ulioko madarakani umeshindwa na kwa makosa hayo hayo viongozi hawa watarudi madarakani 2010!!!Sasa Salimu,Warioba, na Butiku mnaishia kuzungumza tuu kama mmeyaona mapungufu yote??Nadhani kuna haja ya kufikiria a loud zaidi juu ya hoja za wazee wetu hawa,Na kufanya mabadiliko kwani hapo paka keshafungwa kengele sasa kazi ni kuwatoa ndani ya madaraka kwa njia aidha halali au zisizo halali alimradi kuwe na mabadiliko chanya.
 
Last edited:
Waheshimiwa hawa wameyasema yote,lakini mbona hawasemi nini kifanyike?Na tuanzie wapi?...........Ni dhahira uongozi ulioko madarakani umeshindwa na kwa makosa hayo hayo viongozi hawa watarudi madarakani 2010!!!Sasa Salimu,Warioba, na Butiku mnaishia kuzungumza tuu kama mmeyaona mapungufu yote??

Yaleyale ya mvinyo wa zamani katika viriba vipya.
 
Wao wamewaonyesheni uchafu ulipo; nyie hamna akili ya kujua cha kufanya.????!!!!

Yebo Yebo hawa hawa ndo walioko kwenye mfumo wa uongozi Tanzania,Hawa hawa ni wajumbe wa NEC,CC nk Si unajua jinsi ya kuchaguana katika kile chama chetu Tawala???Sasa kama wao wameonyesha ridhaa waonyeshe pia njia ya kupita kwa kizazi kipya kuleta mabadiliko.Uongo si kazi wakati wa vyama vya upinzani kutawala kwa Tanzania bado ni ndoto.Lakini ndani ya Chama hiki tawala tunaweza kupata mbadala.Sasa ndo nimewauliza hawa wakongwe wa siasa za Tanzania ,What is the way forward ??
 
tatiso ni kuwa hawa wote na wengine kama wapambanaji dhidi ya ufisadi wanajua kila kitu kinachoendelea ndani ya serikali yao walikuwa wanashindwa pa kuanzia ila sasa wamepata upenyo...........wanaongea tu hawasemi nin i kifanyike kwa kuwa wanaogopa mkong'oto wa akina makamba maana watawaambia chama kimewalea hivyo wataendelea kulalamika chinichini tu kama watoto......
 
Wao wamewaonyesheni uchafu ulipo; nyie hamna akili ya kujua cha kufanya.????!!!!
Tatizo ni kwamba wasababisha uchafu, waweka uchafu na wazoa uchafu ni wale wale. Mmoja anaropoka, mwingine anasahihisha mropoko wa mwenzie lakini kimsingi ni wale wale, na lao ni lile lile moja. We kumbuka hata wale wa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wanaambiwa watalipwa kwa sheria ya zamani, wakati hawa wa Ubungo maziwa waliambiwa hawawezi kulipwa kwa sheria ya zamani kwa vile bei ya mfuko wa simenti ya zamani ni tofauti na ya sasa.......VIJIMAMBO TUUUU.
 
Last edited:
Hili jambo tusilifanye ngoma ya mdundiko jamani,Kuna jambo la msingi sana ndani ya matamshi ya hawa waungwana!!!Angalieni jambo gani lifanyike kunusuru Taifa mikononi mwA MTU ALIYEKATA TAMAA!!!!
 
Hili jambo tusilifanye ngoma ya mdundiko jamani,Kuna jambo la msingi sana ndani ya matamshi ya hawa waungwana!!!Angalieni jambo gani lifanyike kunusuru Taifa mikononi mwA MTU ALIYEKATA TAMAA!!!!
Siyo mzaa bwana mzee, tatizo matamshi kama haya yameshatolewa sana, lakini muda mfupi baada ya matamshi tunarudi pale pale. We kumbuka enzi za ARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI MPYA, hadi leo tupo wapi??? Ajira milioni moja, hadi leo kuna mwenye takwimu zimeshatoka ngapi...????? Maisha bora kwa kila mtanzania yapo wapi..????? Mwingi naye anakuja na mashangingi, lakini tutarudi pale pale, hao hao watoa matamshi wengine wamo kwenye meremeta and others. Yaani imefika mahala haaminiki mtu, ni bola liende.
 
Hili jambo tusilifanye ngoma ya mdundiko jamani,Kuna jambo la msingi sana ndani ya matamshi ya hawa waungwana!!!Angalieni jambo gani lifanyike kunusuru Taifa mikononi mwA MTU ALIYEKATA TAMAA!!!!


Kuna hadithi fulani huko Uganda ambayo inasema hivi: "Ukimfukuza mwizi kwa mayowe ya huyo huyo mwizi jamani anakimbilia juu kwenu majirani mkamate jamani ......." kama mwizi huyo ana akili atageuza njia badala ya kuelekea juu ataelekea upande mwingine maana tayari juu kuna watu wanamsubiri kumkamata na kumsulubu. Wanachofanya kina Butiku, Warioba na Salum ni kutoa angalizo kwa watawala wetu. Kama wana akili sawa sawa watajua kwamba wanachokifanya kimegundulika na hivyo kugeuza mwenendo (change direction) wao. Bila hivyo wataendelea na mbio zao kuelekea "juu" na hapo ndipo watapambana na wananchi wenye mawe na virungu. Mwenye masikio na asikie!!
 
Waheshimiwa hawa wameyasema yote,lakini mbona hawasemi nini kifanyike?Na tuanzie wapi?...........Ni dhahira uongozi ulioko madarakani umeshindwa na kwa makosa hayo hayo viongozi hawa watarudi madarakani 2010!!!Sasa Salimu,Warioba, na Butiku mnaishia kuzungumza tuu kama mmeyaona mapungufu yote??

Hawana la kutwambia hao mafisadi wako katika boti moja hawawezi kuruhusu kuwadondosha baharini

acha boti liendelee kupelekwa na upepo

zanzibar ooh zanzibar
 
Good ,we need solution and not problems only.
mdau wa Lusungo Ipinda Kyela

Finding solutions is the hardest part.People would rather go the easy route na ndio kinachofanyika siku zote.Ukiangalia mijadala mingi hapa ni kuibua tu matatizo ambayo kila mtu anayajua.Mara xyz ni mafisadi mara jiji ni chafu, mara watanzania ni wavivu kufikiri, mara wanawake wako vile. Baada ya kujua matatizo inabidi tupige hatua nyingine mbele kuleta suluhisho.
Kwenye mada za mahusiano mara nyingi ndiko wachangiaji wameweza kutoa majibu na suluhisho kwa vile ni mambo yanayowatokea kwenye maisha ya kila siku na hivyo ni rahisi watu kutoa ushuhuda wa ni vipi waliondokana na kero au tatizo fulani kwenye uhusiano.Kwenye siasa bahati mbaya si rahisi kutoa uzoefu huu maana utatuzi wa mambo haya unahitaji wenye dhamana kujitoa muhanga na kutoa alternatives.Hili ni gumu ukizingatia siyo mtu mmoja bali ni mifumo, taratibu, sheria, sera nk.Ila kwa kutumia ballot box huenda baadhi ya hatua muhimu zingewezekana.Kwenye ballot nako kuna ishu zake.Ni vipi mwananchi anaweza kuchagua viongozi bora na si bora viongozi? Elimu ya uraia inahitajika.Elimu hii nayo inatolewa na nani na ki vipi? Tumejionea wenyewe sakata la waraka wa Maaskofu na jinsi wenye kuona watapoteza maslahi walivyoupiga vita kwa kuleta hoja za kugawa wananchi.KAZI IPO!
 
Safari hii tutayasikia mengi, lakini mijadala ya namna hii ni afya njema katika ujenzi wa demokrasia hapa kwetu, hivyo busara za wazee hawa katika kipindi hiki ni muhimu!
 
These are old men with experienced brain,they know what are doing. Retired PM is quite different to resigned PM.You can not solve the problem you don't know.They are showing those problems to our blind leaders in order for loyal citizen to act on it after they(leader) has failed.
Lets chose leader who are not arrogant to their people because of being in power for so long.
 
Nimeyapitia mawazo mbali mbali katika thread hii nimepatwa na hisia kuwa wananchi wanahitaji mabadiliko tena ya dhati kabisa.Japo ni dhahiri kuwa watawala wetu wamepoteza uelekeo hawana matumaini ya kurudisha heshima zao mbele za umma wa watanzania KWA JINSI YA KUENDELEA KUWALAGHAI KWA MANENO,VITENGE,KHANGA,KOFIA na TSHIRT.Jambo la kusikitisha sana ni jinsi wananchi wanavyowaonea huruma na kuwarudisha TENA madarakani ILI hali wakijua hawataleta mabadiliko yoyote yale.Hakika wa kuonewa huruma ni umma wa watanzania wasioelewa tabu wanazopata kwa gharama ya kuwa na viongozi wachovu madarakani. Wanaingia gharama kubwa kufidia ufisadi wa wateule hawa wachache wenye uchu wa mali na rasilimali za nchi hii!!Sasa ni nini hatima ya haya yote?Kama wananchi wamesema basi wamechoshwa.Suluhu moja ni kuitisha kura za maoni kabla ya kuingia uchaguzi mkuu.Nini kifanyike kufikia kuitisha kura za maoni?Wananchi kwa nafasi zao,wawe makazini, majumbani,wafanyabiashara na popote walipo watanzania tuhamasishane kwa nia ya kubadili mwelekeo wa umangi meza wa chama tawala na wale wote walio madarakani!!Ni dhahiri uongozi wa nchi hii utaendelea kubakia mikononi mwa CCM kwa miongo mitatu ijayo Hili halina ubishi kabisa!!Ili tusonge mbele bila kujali itikadi za vyama vyetu wote kwa pamoja tudai mabadiliko.Inawezekana tena inawezekana kabisa.Haya shime watanzania tuelewe uhitaji wetu sasa tusimame kutenda kwa kutekeleza yale yatakayotukwamua katika utumwa wa fikra tegemezi.
 
Back
Top Bottom