Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Wakuu
Katika kusheherekea na kuadhimisha miaka minne ya utumishi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia tangu alipoingia madarakani Samia 4x4 wakiongozwa na Mtangazaji Salim Kikeke wameandaa ziara ya matembezi ya kiburudani kuelekea Mkoani Tanga Wilayani Pangani kwa ajili ya kutembelea baadhi ya miradi Mkoani humo na kugawa misaada ya mbalimbali kwa Wananchi wenye uhitaji.
Soma, Pia: Waandishi wana njaa mnategemea wataacha kuwa makanjanja na mchawa? Walipeni muone kama watalamba miguu yenu
Akizungumza na waandishi wa Habari Salim Kikeke amesema moja ya usafiri utakaotumika katika safari hiyo kuelekea huko Pangani Tanga ni gari aina ya Landcruiser 4X4 zaidi ya 100.
Pia amethibitisha kupokelewa na Waziri wa maji na Mbunge wa Pangani Jumaa Aweso ambaye atakuwa kama mwenyeji wao baada ya kuwasili Mkoani humo.
Lengo la safari hiyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia pamoja na kusheherekea miaka minne ya utumishi wake na mambo mazuri aliyoyafanya kwenye Nchi yetu ya Tanzania.