figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Hata hivyo Salehi, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amefafanua kuwa fedha za malipo ya shehena hiyo bado hazijalipwa, hivyo wakati wowote malipo yatakapfanyika Iran itasafirisha shehena hiyo ya maji mazito na kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa suala hilo litafanyika katika wiki zijazo.
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameashiria pia mpango wa kuiuzia Russia tani 40 za maji mazito na kubainisha kuwa mazungumzo juu ya suala hilo yangali yanaendelea.
Dakta Ali Akbar Salehi ameongeza kuwa Iran inaendelea kufanya mazungumzo na nchi kadhaa za Ulaya pia kwa ajili ya kuziuzia maji mazito.
Siku ya Jumatano iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry alizungumzia ununuzi huo wa tani 32 za maji mazito kutoka Iran kwa kueleza kwamba tarehe 22 Aprili Programu ya Isotopu katika Wizara ya Nishati ya nchi hiyo ilisaini mkataba wa kununua tani 32 za maji mazito kutoka Iran na shehena hiyo inatazamiwa kuwasili nchini Marekani katika wiki zijazo.../
Chanzo: parstoday