Marekani kuipelekea Ukraine silaha zenye madini ya urani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Hatua mpya ya Marekani ya kukoleza moto wa vita: Kuipelekea Ukraine silaha zenye madini ya urani

Sep 03, 2023 08:49 UTC

Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani imeamua kwa mara ya kwanza kuipatia Ukraine risasi zenye madini ya urani hafifu. Risasi hizo ni sehemu ya shehena mpya ya silaha ambayo itatangazwa mnamo siku zijazo.

Risasi zenye urani hafifu zitatumiwa kwenye vifaru vya Kimarekani vya Abrams ambavyo itakabidhiwa Ukraine na zina uwezo wa kuteketeza vifaru vya Russia. Kiev inatarajiwa kupokea shehena ya risasi hizo katika kipindi cha wiki chache zijazo; na japokuwa kiwango kamili cha shehena mpya ya silaha itakayopatiwa Ukraine bado hakijafahamika, lakini silaha hizo zitagharimu dola milioni 240 hadi 375.

Miezi michache iliyopita, Uingereza pia ilipeleka Ukraine silaha zenye madini ya urani hafifu, lakini hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kuchukua hatua hiyo, na inatarajiwa kwamba hatua hiyo ya Washington itazusha makelele. Katika hatua tatanishi nyingine inayofanana na hiyo, Marekani tayari ilikwisha ipatia Ukraine shehena ya mabomu ya vishada (cluster bombs) ili iyatumie katika vita na Russia.

Marekani, ikiwa ndiye kinara wa nchi za Magharibi na shirika la kijeshi la NATO, inafanya kila iwezalo kuendeleza na kupanua wigo wa vita vya Ukraine kwa lengo la kuidhoofisha Russia kadiri inavyowezekana na kuisababishia nchi hiyo maafa makubwa ya roho za watu na hasara kubwa kwa zana zake za kijeshi. Hatua ya karibuni kabisa ya Washington katika uga huo ni kupeleka Ukraine risasi zenye urani iliyohafifishwa. Kwa kuzingatia mkwamo uliopo hivi sasa katika mashambulio ya kujibu mapigo yanayofanywa na jeshi la Ukraine, hatua hiyo inachukuliwa kwa matumaini ya kutoa vipigo vikali kwa wanajeshi wa Russia na kuwalazimisha waondoke katika maeneo waliyoyateka. Utumiaji wa risasi zenye madini ya urani hafifu ni miongoni mwa masuala yanayopigiwa kelele; na wapinzani wake, ukiwemo Muungano wa Kimataifa wa Kupiga Marufuku Silaha zenye Urani, wametangaza kuwa aina hiyo ya silaha ni hatari na husababisha saratani au kuzaliwa watoto wenye ulemavu. Urani hafifu ni miongoni mwa mabaki ya urani iliyorutubishwa, ambayo inapotumiwa katika risasi, huwezesha kupenya kwa urahisi kwenye magari ya kivita na kuyateketeza kwa haraka; lakini husababisha pia wingu linalotokana na vumbi la chembechembe za urani ambalo lina athari mbaya kwa wanadamu, viumbe vingine pamoja na mazingira pia. Marekani ilitumia kwa wingi risasi zenye urani hafifu katika vita vya Ghuba ya Uajemi kwenye miaka ya 1990 na 2003. Mnamo mwaka 1999, shirika la kijeshi la NATO, nalo pia lilitumia silaha hizo angamizi katika mashambulio dhidi ya Yugoslavia.

Kwa mtazamo wa serikali ya Biden, kupata ushindi Russia katika vita vya Ukraine, tena mbele ya macho ya NATO, kutalidharaulisha shirika hilo la kijeshi na kupelekea kupanuka zaidi ushawishi na nguvu za Russia kikanda na kimataifa na kubadilisha mlingano wa kiusalama, kijeshi na kisiasa barani Ulaya kwa madhara ya nchi za Magharibi. Kwa hiyo, katika mantiki ya serikali ya Marekani, ni jambo linalokubalika kuchukua hatua yoyote ile itakayozuia kuthibiti kwa jambo hilo ikiwa ni pamoja na kutumia risasi zenye urani hafifu. Aidha, Rais Joe Biden wa Marekani na maafisa wakuu wa kijeshi na usalama wa serikali yake wanaamini kuwa, vita vya Ukraine ni fursa ya kipekee na isiyoweza kujirudia kwa ajili ya kupambana na Russia kadiri inavyowezekana na kuidhoofisha nchi hiyo ili hatimaye kuzuia kukamilika mpango wa kuasisiwa mfumo wa kambi kadhaa duniani. Kwa sababu hiyo, na kama wanavyodai wenyewe, wamejizatiti kuhakikisha wanaizuia Russia kushinda vita vya Ukraine kwa gharama yoyote ile.

Kwa mtazamo wa Moscow, madhumuni ya Marekani ya kuendeleza vita nchini Ukraine ni kuidhoofisha Russia kadiri inavyowezekana, lengo kuu hatimaye, likiwa ni kuigawanya vipande vipande nchi hiyo. Kauli ya karibuni zaidi iliyotolewa kuhusiana na suala hilo ni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken aliyedokeza kuwa ni asilimia tano tu ya bajeti ya ulinzi ya Marekani inatumika kwa ajili kuipatia Ukraine misaada ya kijeshi na silaha. Blinken ameendelea kusema: "sasa hivi tunalidhoofisha na kuliangamiza jeshi la Russia kwa gharama ndogo mno ikilinganishwa na gharama za matumizi yetu mengine ya kijeshi. Ni jambo zuri kuwepo Russia iliyodhoofishwa".

Kutokana na yote hayo inatarajiwa kwamba vita vya Ukraine, ambavyo hadi sasa, vikiwa katika mwezi wake wa 19 vimeshasababisha maafa makubwa ya roho za watu na hasara kubwa za kijeshi sambamba na kuteketeza miundombinu ya Ukraine, sio tu havitaisha, bali vitaendelea na kupamba moto zaidi kutokana na uungaji mkono mkubwa ambao Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine anaupata kwa Marekani na nchi nyingine za Magharibi. Na hiyo ndiyo hali aliyoitabiri pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mnamo siku ya Ijumaa ya tarehe Mosi Septemba, Antonio Guterres alisema, haoni kama kuna matarajio yoyote ya kuhitimishwa mapigano nchini Ukraine, lakini inapasa juhudi zifanyike ili kupunguza athari haribifu za vita.../

4c3p1ba379c0392cufk_800C450.jpg
4c3p61b1d75aa32cudo_800C450.jpg
 
Hizi ndo habari tunataka Sio Zile Za Kimasihara alafu Ukifatilia US Kwa Undani Utagundua wanatumia Akili Sanaa kuliko Nguvu mfano USA akitaka Kukupiga haji Peke yake Lazima Aje na Wenzake NATO Sio kwamba Yeye hana Nguvu ila Nguvu ya Wengi Ni Imara Zaidi kuliko Peke Yako Sasa huyu Putin Yeye anatumia Akili Mgando Enzi za Vita Vya Dunia vya Kwanza Uko
 
Back
Top Bottom