Salamu ya tahadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salamu ya tahadhari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jun 18, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  SALAMU ZA TAHADHARI

  Ndugu Watanzania

  Wiki iliyopita kulikuwa na Taarifa moja kubwa lakini haikupewa mkazo sana navyombo vingi vya kimataifa , inayohusu baadhi ya kampuni za mtandao katika marekani na nchi zingine za ulaya kupiga marufuku compuer kutoka nchi china ambazo zimewekwa programu maalumu zinazozuia kufunguka baadhi ya tovuti ambazo serikali hiyo haitaki maana yake inakuzuia kuwa na uhuru Fulani unapokuwa na computer yako katika kutembelea baadhi ya mitandao .

  Hili sio jambo jipya wala geni tukumbuke uchina ndio nchi ambayo inaongoza duniani kwa kuzuia tovuti katika mitandao yake mbali mbali kunyima wananchi wao uhuru wa kupata taarifa , kutoa maoni pamoja na kushiriki katika mijadala mingine mingi ya ulimwengu mwingine nchi yao inajitahidi kupigana pale ambapo ina maslahi nako .

  Tumeona pia Mwisho wa wiki iliyopita pia Habari za ushindi wa raisi wa Iran zilivyosambaa katika mtandao , ushindi ule haukupokelea vizuri na nchi nyingi za ulaya kwahiyo walichofanya baadhi ya blogu au tovuti zenye habari zile walijaribu kuzizuia zisitembelewe au kublock kwa muda kwa maslahi yao wenyewe , wengi walitegemea mshindi awe mpinzani hapo ni nchi za magharibi zinapigiania maslahi yao katika nchi hiyo .

  Kama mnakumbuka miezi michache iliyopita niliwahi kuandika makala Fulani kuhusu usalama wa taifa letu katika maeneo kadhaa , nafurahi makala ile imeenda kuchapishwa nchini Nigeria katika gazeti moja pamoja na Ghana pamoja na Rwanda watu wakaipenda sana , Wiki hii nilikuwa nchini Rwanda kwa ajili ya makala hiyo na zingine zinazohusu masuala ya ICT .

  Sasa ninachotaka kusema ni kwamba nchi majirani zetu wanajali sana maslahi yao ndani ya nchi yao na njia ya mipaka yao , popote utakapogusa maslahi yao au chochote kinachohusu picha ya nchi yao basi watakuwa tayari kulinda , kutetea na kupigania sio kupiga kelele tu kama wengine tulivyozoea .

  Jumatano ya wiki ijayo tunategemea kupata Ugeni toka kwa bwana Mmoja wa Kenya , Anasema anauza Antivirus , akishauza Antivirus hizo basi anarudi zake Kenya kwenda kula pesa alizouzia watu wengine , yeye hakupi support wala msaada mwingine wowote ukishanunua bidhaa hiyo tu , pia hana leseni ya kuuza bidhaa hizo nchini mwetu hata nchini mwake .

  Bidhaa anazouza ni Antivirus , huko juu nimeongelea kuhusu baadhi ya wananchi wan chi za ulaya wakilalamikia kompuwer zinazotoka uchina kuwekwa programu za kuzuia baadhi ya tovuti kutokufunguka , kama wameshituka leo basi kuna baadhi ya hata hizo computer kuwekwa programu za kufanya mengine zaidi makubwa zaidi ya kublock hizo tovuti .
  Huyo mtu anayetaka kuuza programu hizo nchini kwetu ni sawa na wachina wanaopeleka computer nchini marekani ambazo zina programu hizo maalumu , hapa kwetu tuna jambo moja nalo ni hii jumuiya ya afrika ya mashariki , kila taifa kutumia watu wake na kuhakikisha wanapata taarifa kuhusu wengine ili waweze kushindana nao katika soko na sehemu zingine zinazohusu mashindano .

  Ndio maana Mimi binafsi nimekuwa na wasi wasi tu haiwezekani mtu atoke huko alipo na bidhaa ndogo rahisi antivirus anakuja kuuza nchini , hata leseni ya kufanya hivyo toka katika kampuni husika , sijui mamlaka ya mapato tanzania inachukuwaje kodi hapo manake hana kibali cha kufanya biashara nchini mwetu na katangaza biashara yake anakubaliwa kuingia tu nchini .

  Sidhani kama kuna mtu yuko tayari sasa kupoteza taarifa zake na rasilimali zake kwa watu hawa , lazima tuwaangalie kwa makini na kwa nguvu zote kuhakikisha maslahi ya nchi yetu yanalindwa , taarifa na mengine mengi yanalindwa bila kuingiliwa wala kuharibiwa na wengine kwa njia yoyote ile .
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Umerudisha post ya watu uliyo chukua?
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  kaka asante sana kwa taarifa hii,
  tatizo mamlaka husika ya nchi hii huwa wanasubiri kwanza madhara yakotee ndo waanze kushughulika ndo maana hata makala zako zinaandikwa nje ya nchi na si hapa kwenu
   
 4. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mjomba vipi tena, ule si ulikuwa utani tu?? au ilikuwa kweli...
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  SHY
  thanks bro

  Ila kama tujuavyo serikali yetu ina utaalam wa kisiasa wala mambo ya teknolojia watakuwambia ni ya kisera. tutashambuliwa kupitia mtandao kirahisi na hawa majinuni wa nje. Na si bure kupitia pc au systems za computers za idara mbalimbali zinatembelewa kama watakavyo kwa kuwa sisi tunajua kununua na kutumia tu na sanasana kufanya matengenezo kama kukiwa na uharibifu.

  Udumu SHY
   
Loading...