Salaam zenu wakoloni… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salaam zenu wakoloni…

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Oct 27, 2009.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Natumaini wakuu mnafahamu maana na aina za ukoloni. Katika maana zote, ipo moja ambayo tumekuwa tukiiimba bila ya kuzama kwa undani kuitafakari. “inaposemwa ukoloni ni hali ya jamii moja au kikundi Fulani cha watu kuwatawala jamii nyingine kiuchumi, kielimu, kisiasa na kiutamaduni”. Hapo natoka na neno KIKUNDI FULANI CHA WATU katika bandiko hili. Wakuu, najua kuna wadau humu wataona andiko hili halina mashiko, nawaomba radhi kwani siku hizi nimekuwa nawaza KIJINGA kabisa ila ndo hivyo maana hata mwehu ana mawazo!

  Siyo siri sasa kwamba tunatawaliwa kikoloni na kikundi kidogo cha watu ambao wameamua kujimilikisha utashi wa taifa bila ridhaa zetu. Kikundi hiki ni baba zetu, rafiki na jamaa zetu ambao kwa hila na ufundi mkubwa wameweza kuingia na kuchukua hatamu za kuwatawala wabongo kiuchumi, kielimu, kisiasa na kiutamaduni. Hivyo ukoloni si mpaka nasaba nyingine iitawale nasaba nyingine bali pia hata ukoloni wa nasaba moja ndani kwa ndani unawezekana. Shida kubwa ya ukoloni huu ni kwamba ukombozi wake ni mgumu na unahitaji fahamu zilizotulia kwa malengo kufikia ukombozi kamili. Hawa jamaa wametukoloni vipi? Twende sasa………

  Kiuchumi: -
  Malengo ya nchi kuwa huru ilikuwa ni pamoja na kumiliki na kujiimarisha kiuchumi kama taifa. Taifa hapa si viongozi pekee, bali ni mjumuiko wa viongozi na watu wa nchi hii. Haiyumkiniki kwa zaidi ya miaka 45 tangu uhuru eti sisi kama taifa bado ni omba omba na tegemezi ilhali wateule wachache wana ukwasi wa kutisha, yaani wanamiliki utajiri kuishinda serikali wanayoiongoza. Lakini ukienda hatua moja nyuma kihistoria utagundua kwamba wakwasi hawa ni watoto wa wakulima tena hohehahe.

  Zaidi ya hapo, njia zote za kiuchumi zipo mokononi mwao. Wanajiamulia nini wauze, nini wakodishe, nini wabinafsishe, kiasi gani wachote huku wakijiwekea sheria kwamba wanafanya maamuzi kwa niaba ya wananchi hivyo wasihojiwe (hata mpige kelele kukataa msiuzwe, WATAWAUZA TU!). Ujanja ujanja wa kutamalaki ndiyo umewatamanisha hawa wenzetu kwenda mbali zaidi katika kututawala kikoloni. Wameona kana kwamba haitoshi na sasa wameingia tama mbaya zaidi kwa kuamua kutulazimisha tununue afya zetu ilhali tunalipa kodi. Maamuzi yao ya kiuchumi wanapoyafanya huwa hawajali athari za makazi ya watu, afya zao wala hatima ya wataalam katika Nyanja husika.

  Ninachochea hoja tu…..

  Kielimu: -
  Wakoloni hawa wanapoamua kuhusu hatima ya taifa kielimu ilhali wao na jamaa zao (wakoloni wa kesho) hawathubutu wala kuiamini elimu waliyoichechemiza, yaani wanasoma nje ya mfumo wa elimu waliyoibuni. Ni dalili kwamba wanadhibiti fikra zetu na hata namna ya kureason. Najua wadau mtapigwa na butwaa katika hili nitakalowaambia hapa. Nyuma ya pazia, wakoloni hawa wameamua kuanzisha mtindo wa single textbook katika shule kwa kisingizio kwamba too many textbooks for single subject ni kuwakonfyuzi wanafunzi. Sasa wanachokifanya katika mchakato huu ni uamuzi wa kukurupuka kurudisha serikalini uchapaji wa vitabu chini ya taasisi ya ukuzaji mitaala (Tanzania Institute of Education). Kutokana na ufinyu wa fikra na utekelezaji wa hovyo hovyo wa serikali (ukiritimba) sidhani kama taasisi hii ambayo hailipi kodi itaweza kukidhi mahitaji ya vitabu katika shule zote nchini. Wameamua kuwachinjia baharini publishers wa bongo ambao wanalipa kodi na wanatoa ajira kwa watanzania wengi kupitia tasnia ya vitabu. Nimedokezwa kwamba mtafaruku huu umesababisha Waziri wa elimu kukacha na kukataa kuwa mgeni rasmi katika wiki ya maonesho ya vitabu yaliyofanyika pale Dar es Salaam wiki mbili zilizopita. Mi nshawaambia hawa wakoloni hawaambiliki…. Kuna tetesi kwamba mnene Fulani amewekeza ktk scheme hii kupitia mlango wa serikali. Hivyo serikali ina wabia hii.

  Kisiasa: -
  Kama unabisha hatutawaliwi kisiasa, angalia wanavyotekeleza kikamilifu UTELEKEZAJI wa sera maridhawa zilizobunikwa kwa ustawi wa taifa (watu wote), angalia idadi ya waliojiandikisha kupiga kura halafu oanisha na waliopiga kura, angalia ishu ya mgombea binafsi ambapo mahakama imerule kwamba ni kuntu kikatiba kuwa na wagombea binafsi. Lakini wakoloni wana-apeal na ku-apeal katika appeal ya appeal (mie sijui sheria ila nina mashaka na sheria hii ya rufaa kama ina ukomo wa idadi za appeal). Au waambie masikioni mwao kuwa kesho tunataka tume huru ya uchaguzi utaishia kukwanguliwa konzi la utosi halafu unaswekwa ndani kwa kudistab amani ya nchi (wakoloni). Kama unabisha, THUBUTU uone! Na wakigundua wamepoteza credibility wanatunga sheria ya kutamalaki ya GAWANYA UTAWALE (tizama wanavyoyagawa majimbo ya uchaguzi ktk maeneo wanayopoteza kwa wingi).

  Kiutamaduni: -
  Naomba kuuliza kama RUSHWA si utamaduni ili nirekebishe kauli hapa. Wakoloni hawa wametutawala kiutamaduni na kutuletea utamaduni tusiozaliwa nao yaani utamaduni wa
  ·Uroho wa madaraka
  ·Kwapua kwapua mali ya uma (haina mwenyewe ati!)
  ·Kusema uongo hadharani (watakwambia tupo ktk mchakato wa …..)
  ·Kuingiza udini ktk kuendesha nchi (kikatiba serikali haina dini ila watu wana dini na ni budi kutenganisha dini na uongozi)
  ·Kuanzia na kuhamasisha vyama vya kikabila vya kikanda (umoja wa maendeleo wazaliwa wa kufikirika) hivyo wanarudisha ukabila kwa mlango mwingine.
  ·Kujichukulia sheria mkononi
  ·Ukiwa mkoloni unaweza kufisadi ndoa zao na za watu bila kizuizi
  ·…………
  Pamoja na yote hayo, hata ukisema siwapigii kura hawajali (hawana haja na kura yako) kwani wanachotaka ni wewe kupanga foleni kwenye kituo cha kura (ili dunia ijue kwamba wanapractice ya democrazy kikamilifu) kisha wanafanya the rest.

  Wakuu nimechokoza mjadala tu! Ndo maana sijaweka mifano wala majina ya viumbe humu. Na wakoloni hawa wanajifahamu na kujitambua wanajua wafanyacho huku wakijiumbua wenyewe….. Ila naamini kwamba elimu ya kujitambua na kujua wajibu itasaidia watanzania adili kujua nini wafanye.

  Je wewe una maoni gani?
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama wakoloni wanaogopeka ki hivyo.
  nilipigiwa na mshkaji mmoja hapa leo ahsubui hii akisema kwamba bandiko langu limestrike bull eye and jamaa watanifanyia mkakati.

  Niaminicho ni kwamba ukifanya jambo sahii jiandae kwa suprise kwani wema hawalipwi kamwe.....
   
Loading...