Salaam zangu kwa vijana wa Chama NCCR-MAGEUZI

Nicholas J Clinton

JF-Expert Member
Mar 13, 2014
877
486
SALAAM ZA NDUGU NICOLAS JOVIN CLINTON, MWENYEKITI WA KITENGO CHA VIJANA NCCR-MAGEUZI TAIFA KWA VIJANA.

Ndugu Vijana wote, ambao mmejiunga, mnajiunga na mtaendelea kujiunga na NCCR-MAGEUZI kwa pamoja nawasalimia sana na nachukua nafasi hii kuwakaribisha nyote kwa Pamoja NCCR-MAGEUZI ni mahali sahihi na jukwaa muhimu la kufanya siasa za Kitaifa na zenye kujali UTU wa mwanadamu.

NCCR-MAGEUZI inawapenda sana na sisi Kama Vijana ndani ya chama tumejiandaa kuwapokea kwa mikono miwili katika hali ya utulivu wa fikira. NCCR-MAGEUZI siyo chama kipya miongoni mwenu, hivyo chama chetu kinajali watu wote kujiunga ili UTU wa mwanadamu ulindwe kupitia Itikadi yetu ya UTU.

NCCR-MAGEUZI ni mali ya Watanzania wote waasisi wake ni wapigania Demokrasia ya vyama vingi Nchini na hakina mwasisi mmoja au wawili hiki ni chama chetu kinachomilikiwa na Watanzania sote, na ni chama cha Kitaifa. Vijana mnaoendelea kujiunga na wale ambao mnatamani kujiunga na NCCR-MAGEUZI ni wakati wa kukubali siasa za UTU ambazo zinalinda maslahi na UTU wa mwanadamu.

Sisi Vijana wa NCCR-MAGEUZI tumechagua kuwa sehemu ya chama ambacho kinaaminika na watu wote na chenye lengo la kushinda serikali zote mbili Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Chama chenye Itikadi ya UTU na misingi yake muhimu ambayo maslahi ya Taifa kwetu ni Muhimu kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja au maslahi ya watu waliyo nje ya mipaka ya Nchi yetu.

NCCR-MAGEUZI inaamini katika Itikadi ya UTU ambayo ndo Itikadi pekee na bora Duniani katika ulinzi wa viumbe vyote vishivyo hapa Duniani pamoja na Mazingira yetu. Vijana ni faraja kuwa sehemu ya chama kinachoaminika na Watanzania wengi miongoni mwao. NCCR-MAGEUZI inajijenga katika eneo lote la Muungano wa Nchi yetu. Vijana ni muhimu kuwa sehemu ya Ukombozi wa pili wa kiuchumi katika Nchi yetu, na tushiriki kuamasishana kudai mifumo rafiki ya Uongozi (Utawala bora) na taasisi imara za Umma ili kila Mtanzania ashiriki katika kufanya kazi na kukuza uchumi wa Nchi yetu.

Ndugu James Mbatia Mwenyekiti wa chama ni alama tosha kwa Vijana wote Nchini kujifunza na kuishi Itikadi yetu ya UTU kwa maneno na kwa matendo, siasa za kutukuna watu na kutweza UTU wa watu wengine, kutukana viongozi wa Nchi zimepitwa na wakati, siasa za kujadili matukio na watu zisiwe sehemu ya Vijana wa NCCR-MAGEUZI, bali tujikite katika siasa za ukosoaji na kuonesha njia tushughulike na siasa za masuala tuwe mfano wa kuigwa na washindani wetu kisiasa. Sisi tuwe kiongozi wao kama tulivyo baba na mama wa Mageuzi Nchini na vyama vyote vya upinzani Nchini ni watoto wa NCCR-MAGEUZI na hakuna mtu wa kutunyanganya hii heshima kama chama. Vijana wa NCCR-MAGEUZI tufanye siasa zenye kujali UTU wa mwanadamu tusitukane na kuvunja haki za watu wengine ila tujadili masuala ya Kitaifa ambayo yanalenga kubadili hali ya Nchi yetu na chama chetu.

Sisi tumechangua kuwa walinzi wa Amani ya Mama Tanzania, taswira ya chama chetu ni Vijana na Vijana wanaojituma kufanya kazi kwa bidii ili kushiriki kukuza Uchumi wa Taifa letu, Vijana wabunifu katika Masuala ya sayansi na technologia huku tukijenga hoja za msingi wa kubadili mfumo wetu wa Elimu ili uendane na mazingira yetu ya zama hizi za Electronics.

KITENGO cha Vijana tunasisitiza katika Itikadi yetu ya UTU ndo kiwe kipaumbele cha Vijana kujiunga na chama. Misingi ya UTU iwaongoze Vijana wote kujiunga na NCCR-MAGEUZI ili kujenga Taifa lenye uwezo wa kujitegemea Kiuchumi.

Pia Vijana wanaopenda kugombea uongozi serikalini kupitia uwakirishi wa chama chetu katika Uchaguzi mkuu 2020 endeleeni kujitokeza na kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na NCCR-MAGEUZI ili kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Mama Tanzania ni muhimu kuliko maitaji yetu ya mtu mmoja mmoja tuilinde Amani ya Nchi yetu, na viongozi waliyopewa dhamana na Watanzania watende haki, UPINZANI siyo uadui na Vijana tusiwe sehemu ya kujenga uadui na chama chochote hapa Nchini tushindane kwenye hoja za masuala ya Kitaifa.

#UTU ITIKADI YETU

Pamoja na Salaam za Demokrasia na Maendeleo.

"PAMOJA TUTASHINDA"
IMG_20200709_200953_889.jpeg
 
Back
Top Bottom