Salaam toka kwa Baba Mtarajiwa.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salaam toka kwa Baba Mtarajiwa..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Aug 9, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Wakubwa,

  Mimi ni baba mtarajiwa ambapo mungu akijalia mwezi ujao basi na mimi naanza kuitwa baba au Dingi / Mshua kwa lugha za kisasa.

  Kati ya mambo mengi niliyopanga kumfanyia mwanangu mtarajiwa ambayo yana kipaumbele cha pekee ni malezi bora including elimu na akiba yake ya baadae.

  Suala geni kidogo kwa wazazi wengi huwa ni kutotunza kumbukumbu za watoto wao, mimi ningefurahi sana kama wazazi wangu wangekuwa wamenitunzia vitu vifuatavyo
  a) Kazi zangu za darasani tangu chekechea hadi darasa la saba
  b) Baadhi ya mavazi yangu from 0 age mpaka 12
  c) Picha zangu nyingi nyingi za utoto katika matukio tofauti.

  Lakini wakubwa mimi nina picha moja tu nikiwa 12 age. kwa maana hiyo nimeamua kufanya yafuatayo kwa mwanangu mtarajiwa ili asipate matatizo kama yangu.

  a) Kutunza kumbukubu za maisha yake ya utoto - Picha na Video from 0 age hadi 14
  b) Kutunza mavazi yake yote ya utoto toka 0 age hadi 14
  c) Kutunza kazi zake za darasani toka 3 years hadi std 7, na kumsaidia kuzitunza hata zile za form one hadi four.

  Nimeamua kufanya hivi sababu wazazi wengi hawajali sana suala la kumbukumbu lakini ki ukweli linasaidia mtoto kujua ametokea wapi, makuzi yalikuwaje na ni vipi wazazi mlichangia malezi yake.

  Ni mimi Baba Mtarajiwa - naomba sara zenu mambo yawe swafi niitwe baba kama baadhi yenu humu.
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Utaitwa Baba na Mungu atalisimamia hilo. Kila la kheri Elnino
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  insharah
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Baba mtarajiwa, muhimu pia kushirikiana na mama mtarajiwa ktk malezi kama kukesha usiku na mtoto,kumlisha akifikia wakati huu,kumpeleka clinic nk.
  kumbukumbu ni kitu kizuri sana, usafishe picha na ziwe kwenye album hiyo ndiyo raha siyo digital tu..

  Maandalizi mema ya malezi,you will be a great dad kwa unavyoonesha kimaandishi!..
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Tengeneza baby book....piga picha ya ujauzito wa mama, mtoto akizaliwa bandika footprints zake kwenye baby book, na document kila hatua ya mwanao...atakapoanza kutambaa, kutembea, n.k.
   
 6. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  All the best Elnino !! Kuhifadhi kumbukumbu ni muhimu sana katika maisha... Nakutakia kila la kheri na Mungu
  atakuongoza katika ujio wa mwanao ile uwe wa salama na afya njema. Be blessed n hope you will be a great DAD !!
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hongera kwa kutegemea kupata mtoto na Mungu atakuvusha katika hili.
   
Loading...