Salaam maalum za kidini zinazotufungulia mikutano

Salaam maalum za kidini zinazotufungulia mikutano

Majimengi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
499
Reaction score
197
Tanzania, imefanikiwa sana kwa kujiweka mbali na udini, (na hata ukabila) katika kufanya mambo yake,ingawa dini zote zinaheshimiwa sana.

Kwa sasa, naanza kuona, kwa mbali udini unatuingia taratibu, - (naogopa sana kama muono wango ni kweli).

Miaka ya nyuma, ilikuwa kila kwenye hadhara au mkutano wowote, lugha ya kusalimia au kufungulia kikao, ilikuwa :- UHURU NA KAZI, KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI, ZIDUMU FIKRA ZA M/KITI, NK. Mambo yakaenda.

Hivi sasa mambo yamebadilika, kuna salaam maalum za kidini,zinazotufungulia mikutano.

Mimi naziheshimu Salam zote hizi, lakini naona, salaam hizi zinaweza kuwaitia unyonge watu wasiohusika na dini zenye salaam za mfumo huo.

Wazo langu ni kwamba, kutafutwe maneno mengine yasiyoelemea upande wa dini yeyote, kama vile viapo vya wateule wa Serikali,mahakamani, dua za kufungulia vikao vyaBunge, nk, ambavyo havina mwelekeo wa dini yoyote, lakini Mungu anatukuzwa, na dini zote zinaheshimiwa; kwani kumtukuza Mungu, ndio kuheshimu dini, na kuheshimu dini, ndio kumtukuza Mungu.

Nawasilisha.
 
Tuache tupumue,Asalam Alykum na Tumsifu Yesu Kristo inakuuma nini wewe mpagani
Mwanamzima unaacha kuhangaika na familiar yako unahangaika na msiki au kanisa. Ni ungese wa kifikra
 
Ni maoni yako,na yanaruhusiwa ...ila hayana msingi...ingekua inatumika salamu moja tu kati ya hizo unazolalamikia ningeweza kuzungumza kidogo...wacha salam ziendelee
 
Tanzania, imefanikiwa sana kwa kujiweka mbali na udini, (na hata ukabila) katika kufanya mambo yake,ingawa dini zote zinaheshimiwa sana. Kwa sasa, naanza kuona, kwa mbali udini unatuingia taratibu, - (naogopa sana kama muono wango ni kweli).
Miaka ya nyuma, ilikuwa kila kwenye hadhara au mkutano wowote, lugha ya kusalimia au kufungulia kikao, ilikuwa :- UHURU NA KAZI, KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI, ZIDUMU FIKRA ZA M/KITI, NK. Mambo yakaenda. Hivi sasa mambo yamebadilika, kuna salaam maalum za kidini,zinazotufungulia mikutano. Mimi naziheshimu Salam zote hizi, lakini naona, salaam hizi zinaweza kuwaitia unyonge watu wasiohusika na dini zenye salaam za mfumo huo.
Wazo langu ni kwamba, kutafutwe maneno mengine yasiyoelemea upande wa dini yeyote, kama vile viapo vya wateule wa serikali,mahakamani, dua za kufungulia vikao vyaBunge, nk, ambavyo havina mwelekeo wa dini yoyote, lakini Mungu anatukuzwa, na dini zote zinaheshimiwa; kwani kumtukuza Mungu, ndio kuheshimu dini, na kuheshimu dini, ndio kumtukuza Mungu.
NAWAKILISHA.
Mkuu hata mimi hizo salamu zinanisumbua; utakuta kiongozi anataka kubalance dini zote na madhehebu: utasikia Salaam Aleykum (Waislamu), Bwana Yesu Asifiwe (Walokole), Tumsifu Yesu Kristo (Wakatoliki), Habari za Asubuhi (Waswahili), Itifaki Imezingatiwa, etc
 
Tabia za unafiki ndivyo zinavyofanya kazi hivyo.

Baada ya kusema hayo ngoja nichangie kidogo.

Utaratibu huu haujatungiwa sheria na wala sio sera. Aliyepo madarakani anaupenda; atakapoondoka akija mwingine ataubadilisha.
Ninachohofia hasa ni huo ukabila. Unaweza kuota mizizi na ikashindikana kuing'oa mizizi hiyo. Itahitaji kiongozi wa wakati huo awe makini sana kuhakikisha kwamba tabia hizi haziendelei.
 
Wazo langu ni kwamba, kutafutwe maneno mengine yasiyoelemea upande wa dini yeyote, kama vile viapo vya wateule wa Serikali,mahakamani, dua za kufungulia vikao vyaBunge, nk, ambavyo havina mwelekeo wa dini yoyote, lakini Mungu anatukuzwa, na dini zote zinaheshimiwa; kwani kumtukuza Mungu, ndio kuheshimu dini, na kuheshimu dini, ndio kumtukuza Mungu.

Patamu hapa nimepapenda hebu rudia tena!!! in Makwaia's tone
 
Tanzania, imefanikiwa sana kwa kujiweka mbali na udini, (na hata ukabila) katika kufanya mambo yake,ingawa dini zote zinaheshimiwa sana.

Kwa sasa, naanza kuona, kwa mbali udini unatuingia taratibu, - (naogopa sana kama muono wango ni kweli).

Miaka ya nyuma, ilikuwa kila kwenye hadhara au mkutano wowote, lugha ya kusalimia au kufungulia kikao, ilikuwa :- UHURU NA KAZI, KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI, ZIDUMU FIKRA ZA M/KITI, NK. Mambo yakaenda.

Hivi sasa mambo yamebadilika, kuna salaam maalum za kidini,zinazotufungulia mikutano.

Mimi naziheshimu Salam zote hizi, lakini naona, salaam hizi zinaweza kuwaitia unyonge watu wasiohusika na dini zenye salaam za mfumo huo.

Wazo langu ni kwamba, kutafutwe maneno mengine yasiyoelemea upande wa dini yeyote, kama vile viapo vya wateule wa Serikali,mahakamani, dua za kufungulia vikao vyaBunge, nk, ambavyo havina mwelekeo wa dini yoyote, lakini Mungu anatukuzwa, na dini zote zinaheshimiwa; kwani kumtukuza Mungu, ndio kuheshimu dini, na kuheshimu dini, ndio kumtukuza Mungu.

Nawasilisha.

Huyu jibwana ni mdini,mkabila wa kupindukia.

Karibu Membe ukipasue chama ili arudi kuchunga ngombe
 
Huyu jibwana ni mdini,mkabila wa kupindukia.

Karibu Membe ukipasue chama ili arudi kuchunga ngombe
Hili la ukabila linazungumziwa sana na kuchambuliwa lakini la udini husemwa juujuu tu kua kuna udini, hebu fafanua mkuu kuhusu udini wa huyu bwana, anapendelea dini gani na anaibagua dini gani?

Una mifano au ushahidi wowote labda wa kutetea hoja yako hiyo?
 
Zaidi ya 90% ya teuzi zake zimeegemea ktk ukristu hasa ukatoliki,
 
Mkuu sasa huoni huo mfano umezingua?

Viapo vyote vya kiserikali, kibunge na kimahakama vinafanywa huku mhusika ameshika kitabu cha dini yake.
 
Sio kwamba anachagua kutokana na sifa ya mtu kiutendaji?

Kama ni sifa hao wanaoteuliwa baada ya wengine kutenguliwa kwani hakuwaona tangu awali!!!!???? Kwani wakristu pekee ndo watendaji wazuri!!!?? Kwani watendaji wazuri wengi wanatokea kanda moja!!!!??
Mfano Kitilya alipoingia TRA alikuwa wakikusanya 300b na kaipaisha hadi 900b mda mfupi,na hakuwa anakusanya na za halimashauri, trafic fines, na pia hakutumia migufu kama ilivyo sasa,na mapato hayakuchanganywa na kama ya madini yaliyokamatwa, tozo za mahakama nk.
Sasahivi kila kitu kinachanganywa na kujidai TRA wamekusanya, nyambafu kabisa.
 
Sio kwamba anachagua kutokana na sifa ya mtu kiutendaji?

Mimi siyo mkatoliki lakini ni ukweli kuwa huwezi kuepuka watu wa dhehebu hili kuwa katika nafasi mbalimbali.Siri ya Wakatoliki ni kuwekeza katika elimu.Shule zao nyingi zinafanya vizuri katika kutoa elimu na matokeo mazuri ya mitihani.Hao pia ndio baadaye huja kuwa na vyeo mbalimbali kwenye huduma za jamii.Madhehebu yetu mengine nasi tukijitahidi katika kuanzisha shule zenye kutoa elimu bora,polepole hii dhana ya kupendelea wakristo(na hasa wakatoliki) itaisha yenyewe
 
Kuna maneno mengine kwenye lugha huwa yanazuka tu bila hata utaratibu maalum kulingana na mazingira,muktadha,wakati au tamaduni ya sehemu husika na baadae hupotea yenyewe. Kwahyo mkuu hayo yasikuumize kichwa hayapo katika utaratibu, wewe ukisimama kwenye mkutano toa salam yako unayoipenda.
 
Mtoa mada una hoja nzuri sana. Hizi salaama zinaleta vimelea vya udini. Hakuna sababu ya kutoa salaam za aina hiyo. Pili, mlolongo wa kuwataja wageni wanaohudhuria sherehe nao unachusha sana. Dakika tano zinatumika kuwataja wageni - haya ni matumizi mabaya ya muda.
 
Kaka yangu bora umeliona hili na kuliongelea, japo siku hizi umekuwa muoga wa kuchangia hapa jukwaani au kwenye TV. Woga sio kitu kizuri maana utakufa na unayoyamini au kuyajua bila kuyatoa kwenye jamii. Ukweli ni kuwa hizi ni tabia binafsi za rais, na kwakuwa anazungukwa na wanafiki wengi, utakuta hawamwambii na wao wanaishia kuiga huo udhaifu usio na tija. Nyingi ya hizo salamu zina lengo la kuhadaa umma kwamba ni mcha Mungu na anaongozwa na hofu ya Mungu, jambo ambalo si kweli. Inanikumbusha enzi za Nyerere kuna watu walikuwa wanavaa na kucheka kama Nyerere!
 
Back
Top Bottom