Salaam kwa Mh. Edward Lowassa na wenzake


Heshima yako mkuu, hii nilikuwa sijaiona hii, mkuu kama unayosema ni kweli kwamba Mwalimu, hakupaswa kuwachekea chekea viongozi wake wa chini, basi kusingekuwa na ishu kabisa hapa, maana yeye alikuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfikisha Lowassa, mahakamani, lakini akaamua kuutumia kumtoa kwenye kugombea urais tu, sasa kama kweli hakutakiwa kuchekea chekea kama ulivyosema, breki ya kwanza ingekuwa mahakamani,

Hakuenda mahakamani kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mahakama na sheria, sasa unashangaa kwa nini Lowassa amejiuzulu na anaendelea kutucheka system nzima ya serikali akiwa nje huku akizoa mafao ya kodi zetu? Sasa kutocheka na kumtukana Kawawa kulisaidia nini? Kama wewe kweli una hoja endelevu na zisizoelea elea, basi ungepaswa kuelewa kuwa haikuwa mara ya kwanza kwa Kawawa kufanya kitendo cha kujaribu kumtetea kiongozi fisadi, je ni nani hao wengine aliowatetea, maana haiwezekani kuwa hii ndio ilikuwa mara yake ya kwanza?

Ukondoo na mapungufu kwenye serikali yetu ulianziwshwa na kulelewa na nani mkuu kama sio yeye Mwalimu? Sasa Mwalimu asiyecheka cheka kama unavyosema ilikuwaje akatuambia kuwa Mkapa ni Mr. Clean, na akaishia kuwa Mr. Chafu? Unajua nyinyi watu wa Mwalimu, mna kazi kubwa sana ya kumsafisha hapa JF.

Ahsante Mkuu!
 
Ndugu zangu wana JF musiomjua Mzee Kasori naomba niwahakikishie kuwa huyo Mzee ana mengi sana moyoni mwake. Sio mnafiki na wala hakuwa muoga pale alipokuwa akifanya kazi. Namfahamu vizuri sana. Namheshimu sana.

Mzee Kasori nakuomba uendelee kusema bila kuogopa vijimaneno vya mitaani vyenye taswira ya kuwatetea "mafisadi" kwani tunajua kuwa kuna watu hapa wamepata hela hizo kwa namna fulani.
 
Sasa yanatimia... Ile nchi ya ahadi ninaiona ileee, no more vifo vya akina mama na watoto wachanga, no more ajali za ajabu ajabu, no more kula majani , no more kuomba haki zetu , no more mafuta kuwa juu kupita kiasi, no more umeme kuwa juu, no more banks zetu kutoza riba za juu, no more walimu kugoma, no more madaktari kutothaminiwa ...no more... Thanks Mzee Kasori, Mwanakijiji,FieldMarshall, Kitila, Mpaka kieleweke, Mkuu Invisible, na wengineo wengi wenye mapenzi mema na Tanzania yetu... Mapambano yataendelea daima ...
 
Kwa kweli article ya Mzee Kasori nilipoisoma tena leo imenipa update kuhusu nchi yangu, TULIKOTOKA, TULIPO na TUENDAKO na kujiuliza ndiko huko kwenye ahadi ya nchi ya Maziwa na Asali??? Sina jibu!!!
 
Kama Lowasa alisema anataka Mwalimu Nyerere aende Monduli kulisafisha jina lake,that was a very impudent thing to say.
Kama Mwalimu alimuambia Kasori,aende kumwambia Kawawa'"usiwe mjinga kama Lowasa",kulikuwa na tatizo gani kwa Kasori kwenda kumuambia Kawawa kwamba "Mwalimu amesema usiwe mjinga kama Lowasa."
Mambo haya anayoandika Kasori ni ambiguous.
Kwa jinsi Kasori anavyoandika,ina maana kwamba anadhani Lowasa ni fisadi,labda,angependa kumuona Lowasa anatiwa pingu,apelekwe mMahakamani kusafisha jina lake. Yes or no,haya ndiyo mambo anyoandika Kasori?
How can he speak in "diplomatic " manner wakati Mwalimu amemuagiza akamwambie Kawawa kwamba yeye ni mjinga. If everyone is going to be "diplomatic",how will these bank robbers get sent to jail?
 
Hii salaam kwa Lowasa inatosha kabisa kuwa ya milele na milele..

 
hawezi kudhibitisha maana niukweli na ameshikwa kwa pabaya maana mwalimu alipoenda south africa akaambiahaka ndio kajumba ka waziri wako nani lowasa alishangaaaaaaaaaa sana
 
Mwenyezi Mungu akubariki na kukujalia maisha marefu na yenye baraka Mzee Wetu Kasori.....Leave longer mzee.
 

Mkuu hapa wakushughulikiwa ni Kikwete maana kuhusu uwaziri mkuu wa Lowasa; Kikwete halikataa ushauri wa kila mtu, alikatazwa sana lakini alikataa na mpaka wanamnunuwa Mtikila kumtukana Mwalimu issue ya Mtikila kumtukana mwalimu ni Lowasa na Rostam ndio waliopa fedha na kumnunuwa kufanya hivyo.

Kumbuka hata baada ya sakata la Richmond bado Lowasa alikuwa na kiburi cha wazi kusema kuwa hajakutana na Kikwete barabarani, Tatizo hapa ni hilo alilosema Dr. Kitila Unafki na Uoga hasa ndani ya vyombo vyetu vya Dola, maana kama sijakosea Huyu mzee ni moja wa watu wa System wa zamani lakini ndio hivyo walifundishwa kulinda na kuficha maovu ya viongozi na hapo ndipo walipotushikia hawa Mafisadi wanajuwa fika kuwa vyombo vya Dola hawana akili tofauti na ya kulinda na kuficha mambo ya viongozi hata kama ni upuuzi wa kutupwa chooni.
 
Huyo mtoa mada anaonyesha ana chuki binafsi na Lowassa kwa sababu zifuatazo:
1.Amejitahidi sana kutumia different school of thoughts kuelezea truth na anger kwa lengo la kumchambua lowassa na uadilifu wake. Hivi ni kweli viongozi wote ni waadilifu hapa TZ kasoro lowassa at least mtu unapoamua kueleza jambo kwa lengo la kuelimisha jamii usiwe na ubaguzi/biasness wazi wazi hivi-Hiii inaonyesha una lako jambo.

2.RICHMOND; Hivi ni kitu gani kilisambabisha Sita afunge mjadala wa richmond ?huyo mtoa mada anakimbilia tu kumlaumu lowassa wengine hawaoni -bias
3.Mwanzo Lowassa alipojiuzulu nilimuona ni mbaya lakini nimekuja kugundua kuwa Richmond ilitumika kama chambo cha kunasia samaki=mahasimu wake wa kisiasa walitaka auteme uaziri ambao sita alikuwa anautaka
3.Richmond ilielezwa kuwa ni feki na dowans ni feki sasa maajabu symbion ni imekubalika-Hata mtoto mdogo haitaji maelezo kuelewa motive ya kundwa kwa kamati teule.(Lowassa akose U mp katuzibia)
4.Hivi ni kuulize wewe mtoa mada hii richmond ilikuja kunisuru nchi kuingia jizani kama sasa hivi,na kabla ya hapo kulikuwa na makampuni mengine kama songas,IPTL,na agereko nk,je haya makapuni huwa ndio mazuri sana nikimanisha bei na huduma zao? ningekuona una lengo la kutusaidia watanzania na theory zako kama ungeyachambua na haya makampuni mengine ili tuweze kulinganisha.
5.KASORI:Huyu kasori hiyo hadithi yake siwezi kuiamini kwa sababu hakuwai kueleza tangu kipindi mwalimu alivyosema.Tena kwa jinsi mwalimu alivyokuwaga hamuogopi mtu ,lazima angeitisha mkutano na waandishi wa habari na aweke wazi kama alivyomuumbuaga john malecela kuwa anataka kuwa Jummanne. Huyu kasori ni story ya kutunga tu ni chambo kingine kimetungwa na mahasimu wa Lowassa ili waendelee kunasa samaki kama richmond ilivyotumika huku kuna makapuni mengi ya umeme yamefisadi mf IPTL
 

Sidhani kama tunaitendea haki hii mada kwa kuanza kujadili ujumbe tu wa Nyerere kwa Kawawa kwani itakuwa tumeijadili kwa mtazamo finyu mno. Sisi ambao hatujui imetufungua macho kwa kiasi kikubwa kuhusu huyu EL alivyo na historia ya kukosa uadilifu tangu enzi za Mwalimu.

Nyerere kumwambia kawawa usiwe mjinga kama lowassa ni neno la tahadhari na wala siyo tusi wala kumdharau Kawawa . Alimpa tahadhari in strongest term ili Kawawa akae mbali na huo mpango wa kumsafisha Lowassa kwani angekuwa responsible kwa consequences zake na in the lon run hata legacy ya Kawawa ingekuwa highly turnished. Nyerere alimjua Kawawa kuliko sisi na alijua vema kuchagua misamiati ya kuongea naye ambayo ingempa alert kwa haraka.
 
Very funny. Huyu mzee yuko wapi na ni nani sasa hvi? Katiba inasemaje kuhusu kila mtu pamoja na mwizi? Tuache upambe
 
“ Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu” ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu.
........Hakuna jambo linalonikera kama hili.
 
Wakati hii mada inawekwa humu, wengi tulikuwa hatujazaliwa. Sasa tupo wengi humu na ukweli wa juzi unaishi hadi sasa. Wala si utabiri bali ni ukweli ambao mhusika hafanyi jitihada za kuukubali bali kuufunika. Uvundo haufichwi! Now we know. Watanzania tusiwe wajinga kama kawawa!
 
Hata inashangaza watu wanapokuja na mada mpya siku hizi kufanya jitihada za kumsafisha EL. Lowassa ni mchafu na hasafishiki. Kitila kasema kweli, tunasumbuliwa na uoga na unafiki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…