Cha kushangaza nini? Si umesema unamchukulia kama dadako, naye anakuchukulia hivyo hivyo. Nifikiriacho ni wewe ndiye uliyeanza kumuangalia kwa jicho la tatu. Kama uko njia panda na wahisi anamaanisha kitu, basi muulize! Humu jamvini hamna mwenye jibu sahihi, yote utakayopata humu ni maoni na mitazamo ya watu. Ajuaye na mwenye jibu kamili ni huyo huyo "dadako"!