Mbona watu mna mshambulia housegirl namna hiyo? Ametumia sanaa kufikisha ujumbe. Nashangaa katika point zote alizoziongea mmeona Mzungu tu. Yaani mmechukulia Mzungu kama Mzungu. Ni kama Mrisho Mpoto alivyoimba mjomba etc.
Kiukweli katika ustaarabu na usawa wa gender wazungu wametuzidi mbali. Katika jamii zetu bado tuna unyanyasaji wa kijinsia wa kipumbavu, tunahitaji elimu. Wanawake nao hawajitambui, wanafundwa kuvumilia ujinga wa wanaume. Tuna safari ndefu. Mzungu anaweza akasaidia.
Jamii yetu imejaa unafiki. Kupiga vita ushoga wakati mnakula tigo za wanawake. Ustaarabu ni Kukubali na kuheshimu sex orientation za watu wengine. Msihukumu watu kwa sex orientation. Hao wazungu waliowaletea biblia na dini leo wanafungisha ndoa za jinsia moja, nyie ambao mmeletewa tu ndo mnajidai mnajua sana! Kushinda waliowaletea. Kwani itachomwa moto kwa dhambi za mwenzako. Wewe shika 50 zako na imani yako waache wengine wafanye yao, huo ndo ustaarabu.
Tubadilike, jamani. Tuheshimu wake zetu nao watatuheshimu, tuache visingizio vya kupitiwa na shetani au udhaifu ili kuhalalisha michepuko.