Sala Kwa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sala Kwa Taifa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masanilo, Sep 3, 2010.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asante Mungu kwa kuipenda Tanzania hata ukamtuma mwanamapinduzi wa pekee Dr. W. Slaa ili kila Mtanzania atakayempigia kura apate kuleta ukombozi wa kweli.


  Tazama umemtuma kwa wapenda haki ili patakatifu (ikulu) pawe na Amani,
  Sasa basi Mungu wasaidie watanzania wenzetu wasio na ujuzi wa Kutambua nani kiongozi Bora wamtambue kuwa amekuwa akidai haki zao yapata miaka 15,
  Mungu tuepushe na rushwa za vitenge, pombe, simu, na Ahadi za uongo maana wewe hupendi uongo.


  Rev Masa K

   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Amen!
   
 3. senator

  senator JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Nami nasema Amina...
  Tuzidi kuomba na kufunga ili sala ya Rev Masa isikiwe huko alipopeleka maombezi haya
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Eee Mola wetu! Uliyetukuka, wajalie waja wako watanzania kupata ufahamu sahihi na kutokufanywa wapumbavu kwa ahadi zisizo tekelezeka na kudanganywa kwa kupewa zawadi vinguo na fedha za rushwa na matokeo ni kuyagharimu maisha yao na ya watoto wao baada yao.

  EeeMola, fungua fahamu zetu tuelewe na maneno aliyotuasa mja wako baba wa Taifa hili,JK Nyerere, ya kwamba "Mtu mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, usipoyakataa anakudharau" akarudia akisisitiza ya kwamba " mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu na wewe unayatii, akijua kwamba ni ya kipumbavu, unayakubali, anakudharau" Tuondolee huku kudharauliwa. Zaidi tunadharauliwa na watu wasio wazawa wa nchi hii uliyotuweka waja wako.

  Mola mwenye enzi yote! Hatukuchagua kuzaliwa Tanzania bali ulitufanye tuzaliwe hapa. Hatukuchagua mama wala baba, ndivyo watoto na wajukuu zetu nao hawakuchagua wazaliwe na sisi. Umetuweka katika nchi yenye utajiri mkuu, tupe waja wako kufaidi matunda ya utajiri huu sisi na vizazi vyetu na si wageni wala wapitaji. Tukiishi kama ndugu na kupendana.

  Tufanyizie ukombozi kwani wewe ni Mungu usiyeshindwa jambo.
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Aleluyaaaah, aleluyaaaah.....@@#$%^&&***&@@@<<???&%%%$$#@@@............................@@##%$^^&&<<MDBHYJVVWGVHUbdbvdhdgdvduu!!@22222@@@......aleluyaaaaah aleluyaaaaah............%#@@,,,,,>>>>>>>>>>>>>>>> Amen!!

  Msishangae wakuu zangu, nilikuwa nanena kwa lugha wakati wa sala, maana mchungaji Masa kaamsha kunena!!!
   
 6. P

  Padri Member

  #6
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mgombea urais wa chadema amepewa milioni 520 ili agombee urais kupitia chadema. Acha shilingi milioni 12 kila mwezi huyu ndio anasema mtetezi wa wanyonge bwana slaa
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kapewa na nani?
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Sep 3, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  upupu na pumba hizi.....CHADEMA wangekuwa na milioni 500 za kumpa mtu mmoja...wasingekosa pesa za kugawa fulana bure......wasio na uchungu ni CCM...ambao wamekomba pesa za kampeni hadi kwa makampuni marehemu kama ATC...na kuzitumia kuweka mabango kila mahali kuliko coca cola...au vodacom.....yaani sijui kwa nini wametumia nguvu kubwa kuliko hata ya mwaka 2005 au 1995......MATANGAZO HADI KWENYE MAJI!!?
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Padri
  Member

  Join Date
  Thu Aug 2010

  Hapo kwa Red noted!
   
 10. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  du umenena kwa lugha kweli kweli
   
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  amepewa mil 520 na nani,RA? hueleweki au mimi sielewi
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ukiulizwa na nani hutakuwa na jibu!
   
 13. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Rev Masa, mimi nilifikiri utaratibu wa kusali kwa ajili ya Taifa ni wa-kila siku. Kulikoni mbona kimya kwenye kutuongoza katika sala?
  Ama unatushauri tuendelee kurudia-rudia hizo hizo? (Ila sala ya Nyunyu ngumu)
   
 14. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  2010 hatudanganyiki
   
 15. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  This message has been deleted by Selemani.
   
 16. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0  Laws of Justice and Mercy

  1 "Do not spread false reports. Do not help a wicked man by being a malicious witness. 2 "Do not follow the crowd in doing wrong. When you give testimony in a lawsuit, do not pervert justice by siding with the crowd, 3 and do not show favoritism to a poor man in his lawsuit.
  4 "If you come across your enemy's ox or donkey wandering off, be sure to take it back to him. 5 If you see the donkey of someone who hates you fallen down under its load, do not leave it there; be sure you help him with it.
  6 "Do not deny justice to your poor people in their lawsuits. 7 Have nothing to do with a false charge and do not put an innocent or honest person to death, for I will not acquit the guilty.
  8 "Do not accept a bribe, for a bribe blinds those who see and twists the words of the righteous.
  9 "Do not oppress an alien; you yourselves know how it feels to be aliens, because you were aliens in Egypt.
  Exodus 23

  Source:Exodus 23 - Passage Lookup - New International Version - BibleGateway.com
   
Loading...