Sakata la wabunge 19

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Kwa siku za karibuni, kumekuwepo na mjadala mkubwa sana juu ya sakata la wabunge 19 wa viti maalumu kutoka Chama cha Demokraaia na maendeleo ( CHADEMA)

Kwa mujibu wa ibara ya 71 (1)(e) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inasema mbunge atakoma kuwa mbunge endapo ataacha kuwa mwanachama wa chama cha siasa, alichokuwamo wakati anachaguliwa au Kuteuliwa kuwa mbunge

Ni kweli kabisa chama cha Chadema kilitoa taarifa kupitia vyombo vya habari, kuwa wabunge hao 19, wamefukuzwa uanachama kwa makosa ya usaliti( kwa mujibu wa taarifa ya Chadema)

Hiyo ni hatua ya kwanza ndani ya chama

Hatua ya pili sasa, ni wao Chama kwa maana ya Chadema kutoa taarifa rasmi kwa mheshimiwa spika juu ya maamuzi yao

Taafira watatoa kwa njia gani?

Ni wajibu wao sasa Chadema, kutoa taarifa ya maandishi kwa mheshimiwa spika kwa kumuandikia barua rasmi ya kumtaarifu hatua yao hiyo ya kuwavua wanachama hao wabunge 19

Na sio barua tu, barua hiyo inatakiwa kuambatana na vidhibitisho vya uhalali wa vikao waliovyokaa kufikia maamuzi hayo( kwa mujibu wa katiba na kanuni za Chadema ya mwaka 2006)

Kwa kawaida spika au ofisi yeyote ile haiwezi kufanya maamuzi kwa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari tu, ni lazima apokee barua rasmi kutoka Chadema kabla ya kufanya maamuzi yeyote

Sasa tatizo lilipo, je Chadema watamuandikia barua spika yupi?

Kwa sababu, kwa mujibu wa msimamo wa Chadema wa sasa, ni kuwa wao hawatambui kabisa matokeo ya uchaguzi mkuu wa October 28, pamoja na wote waliochaguliwa kwenye uchaguzi huo kuanzia Rais , wabunge na madiwani

Maana yake nini?

Ni kwamba hawatambui wabunge, hivyo basi hawamtambui spika mheshimiwa Job Ndugai,aliyechaguliwa na wabunge hao, kwa maana hiyo hawatambui uwepo wa bunge la12

Sasa kwa wao kuandika barua rasmi kwa mheshimiwa spika, na kumtaaarifu hatua za kinidhamu walizochukua dhidi ya wabunge hao 19, tafsiri yake ni kwamba, wanamtambua spika, hivyo wanatambua matokeo ya uchaguzi mkuu wa 28 October

Wakifanya hivyo, kwa maana ya kumpa taarifa ya maandishi mheshimiwa spika, basi mheshimiwa Spika hatakuwa na la kufanya zaidi ya kuwaandikia tume ya taifa yauchaguzi, kuitaharifu kuhusu wabunge hao kuvuliwa ubunge, kwa kùkosa sifa stahili ( kukoma kuwa wanachama wa chama cha siasa kilichowadhamini)

Japo ssa kwa mujibu wa ibara ya 83( 1) ( b) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, bado wabunge hao wanaweza kwenda Mahakamani kupinga uamuzi wa chama chao( Chadema)kuwavua uanachama

Endapo hilo litatokea, basi hawataweza kuvuliwa uanachama, hivyo hawataweza kuvuliwa ubunge,mpaka hapo shauri lao la msingi(la kupinga kuvuliwa uanachama) litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama husika

Japo sasa kwa mujibu wa katiba na kanuni ya Chadema ya mwaka 2006, kifungu cha 8.0(a) (x) kinasema

CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama,kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani, mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu za ngazi za chama,hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama

Kwa maana hiyo, mwanachama wa Chadema akienda Mahakamani kupinga maamuzi ya vikao vya chama, automatically unafukuzwa uanachama wa chama hicho( rejea shauri la mheshimiwa Zitto Kabwe la mwaka 2014)

Kwa hiyo sasa ili mheshimiwa spika aweze kufanya maamuzi, ni lazima Chadema wamuandikie barua rasmi kumuharifu hatua walizochukua juu ya wabunge hao

Bila ya kufanya hivyo, kisheria mpaka sasa mheshimiwa spika hana taarifa yeyote juu ya wabunge hao kuvuliwa uanachama, na kwa mantiki hiyo wabunge hao 19, wataendelea kuwa wabunge ndani ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania


Ngamanya Kitangalala Mwaswala
0756 669494
 
No Wanatakiwa kumwandikia NEC then NEC anamwambia Sipika then NEC wanateua majina mengine 19 kutoka kwenye orodha ya majina 105? yaliyopelekwa kutoka na chama na kujazwa form 8? na kuapa mahakamani
 
Nataka kuuliza swali fikirishi kidogo. Hivi haiwezekani kwamba hawa akina Mama 19 wanautaratibu ambao utakuja kutushangaza? Kwamba waliitwa wakaahidiwa kuteuliwa kuwa viti maalum, wakaliongelea "internally" wakakubaliana wakubali wafanye hivyo halafu wafukuzwe chama ........ aliyetoa offer aumbuke? kwa kuvunja taratibu na katiba? nk. nk.? Hebu tutafakari!
 
Sasa kama CHADEMA hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi kwa nini mnahangaika na kina Halima?
 
Back
Top Bottom