Sakata la TFF nani mkweli?

Sakata la TFF nani mkweli?

Ukitaka kuamini hii ni vita ya maslai, ukimsikiliza mama Fenela utaona kua kua nawakati kasema "Tenga kwanza uongozi wake umeisha" kama kumpiga dongo vile, na ukisikiliza hotuba ya Tenga utaona naye anasema "huyu mama atakua kashauriwa vibaya, sasa ukiona hapo kama ni dongo nae maana hakusema Waziri kasema huyu mama akimaaniasha "kua yeye ni mwanamke na mpira haujui"
 
Katiba za vyama vya hiari ikiwepo TFF husajiliwa na serikali (msajili)...

Kosa lililofanyika ni kwa serikali kupitia msajili wake kuisajili katiba mpya ya TFF (iliyobadilishwa kwa waraka sio mkutano mkuu kama katiba ya 2006 inavyotaka).

Waziri alitakiwa kumwagiza msajili kutengua usajili on premise kwamba alipotoshwa na TFF.....hapa ingekuwa on TFF kuprove kuwa hawakumdanganya Msajili kwamba mabadiliko ya katiba yalifuata taratibu husika
Kwa hiyo unasema kua katiba ilisajiliwa kinyemela bila kufuata utaratibu?
 
halafu ukimsikiliza Tenga, anang'aangania kua serikali kuwaambia watumie katiba ya mwaka 2006 ni kwamba tubarudi kule kule akisema kua kuanzia miaka ya 2008 mpka 2011 kuna mikutano mikuu imepitisha mambo mengi kwa hiyo eti haiwezi kutumika..

Sio sahihi kusema katiba ya 2006 ni kurudi nyuma.... JMT inatumia katiba ya 1977 ingawa kuna mabadiliko kibao yamefanywa hapa kati including 1992 kuruhusu vyama vingi.....ingawa bado tunaita katiba ya 1977.

Serikali ishike hapo hapo kama kufungiwa na tufungiwe tu....after all tumepata nini kwa kutofungiwa kwetu ukiondoa personal glory???
 
acha tufungiwe kwani tuna faida gani katika soka hapa duniani?
 
Kwa hiyo unasema kua katiba ilisajiliwa kinyemela bila kufuata utaratibu?

Wala sio kinyemela...ni ile hulka ya kufanya kazi kwa mazoea tu.

Kuna minutes za mkutano mkuu zinazotakiwa kuambatanishwa na barua yenye kuomba kusajili mabadiliko kwenye katiba husika.
Sasa swali.....je msajili alipelekewa minutes?? Kama ndio TFF walizitoa wapi wakati hapajakuwa na mkutano mkuu??

Mzigo huu unapaswa kumwangukia msajili, waziri akeep distance then tuone TFF kama watalia kuingiliwa na serikali.
 
Mzigo huu unapaswa kumwangukia msajili, waziri akeep distance then tuone TFF kama watalia kuingiliwa na serikali.
hapo ndipo Tenga kaamua kukomaa na mama baada ya kuona kuna loop hole ya kumbana
 
Kosa kubwa alilofanya Tenga na timu yake ni kumfanyia fitina Wambura kila uchaguzi,Tangu ameingia madarakani kila Wambura akigombea uongozi wa soka popote walikuwa wanamwekea zengwe,tangu huko nyuma wangemwacha agombee ashindwe mwenyewe sidhani kama leo angelipua hilo bomu la katiba.Walidhani hata sasa watamwondoa but wakasahau kujipanga
 
Kosa kubwa alilofanya Tenga na timu yake ni kumfanyia fitina Wambura kila uchaguzi,Tangu ameingia madarakani kila Wambura akigombea uongozi wa soka popote walikuwa wanamwekea zengwe,tangu huko nyuma wangemwacha agombee ashindwe mwenyewe sidhani kama leo angelipua hilo bomu la katiba.Walidhani hata sasa watamwondoa but wakasahau kujipanga
Ndolanga tulimsema tukaja kumpenda Tenga sasa naona Tenga anarudia ya Ndolanga
 
acha tufungiwe kwani tuna faida gani katika soka hapa duniani?

Mimi hili suala la kufungiwa Tanzania sioni linakujaje? Walichokifanya Wizara, kwa maoni yangu, sio kuingilia kazi za uendeshaji wa soka, kwa mujibu wa sheria za FIFA, bali ni utaratibu wa ndani wa kuhakikisha kwamba vyamba vya michezo nchini vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Ndio maana sheria za FIFA haziseme kwamba vyama vya mpira wa miguu visajiriwe FIFA kabla havijasajiriwa katika mamlaka ya nchi husika. Sheria za FIFA zinataka kwanza zisajiriwe katika nchi husika. Kusajili katika nchi husika inamaana ni kucomply na matakwa yote ya usajili.

TFF kwa kulijua hilo waliwaslisha katika ofisi za msajili wa michezo rasimu ya marekebisho ya katiba na muhtasari. Baada ya kuzipitia msajili aliona kwamba marekebisho ya katiba hayakukidhi matakwa ya katiba ya TFF na sheria za nchi. Akatoa maelekezo ya kwamba katiba sahihi ya TFF kwa mujibu wa sheria za nchi ni ile ya mwaka 2006. Sasa mpaka hapo serikali imeingilia nini katika kazi za TFF kama chama cha mpira? Kwani suala la usajili wa marekevbisho ya katiba ya TFF ni moja kati ya kazi za TFF? Kama TFF ingeingilia na kuwaambia TFF msimchague huyu mmuchague huyu? Au msiwa na ligi ya daraja la kwanza bali ligi zianzie daraja la pili hapo tungesema serikali imeingilia kazi za TFF. Lakini kama ni suala la usimamiaji wa utekelezaji wa sheria za nchi hizo ni kazi za msingi za serikali
 
Wadau,

Nimejaribu kufuatilia hili sakata la TFF, kati ya Wizara na TFF nimeona kuna mambo ya kujadili, ukimsikiliza Waziri anadai kua katiba mpya ya TFF imekiuka taratibu na kwa hiyo katiba hiyo ni batili. Ila ukimsiliza Tenga mwenyewe anasema kua maagizo aliyotoa wazir hayatekelezeki na akatoa onyo kua hili lizaweza kupelekea Tanzania kufungiwa na FiFa. Je kwa wale wchambuzi wa mambo hivi hapa nani mkweli kwenye hili Sakata?

soka la bongo uzuhi mtupu tunakomaa basi tu..
 
soka la bongo uzuhi mtupu tunakomaa basi tu..

Enzi za akina Ndolanga ilikuwa almost hivi hivi. Watu wanatuhumiwa kufanya makosa ya jinai wakiwa viongozi wa TFF(FAT) sheria za nchi zinataka kuchukuwa mkondo wake, wao wanakimbilia FIFA na kutia mkwara kwamba nchi itafungiwa kushiriki soka la kimataifa endapo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Hoja yao ilikuwa ni kama hiihii. Kwamba serikali ikitumia sheria za nchi kuwashugulikia itakuwa imeingilia mambo ya soka. Kilichotokea ni kwamba viongozi watuhumiwa waliburuzwa mahakamani na walioonekana na hatia walimwagwa gerezani na Tanzania haikufungiwa kushriki soka la kimataifa wala kutishiwa kufungiwa.

Tenga na wenzake wanajua fika kwamba kwa mujibu wa sheria inayoundwa TFF na katiba ya TFF, katiba inapaswa kubadilishwa na mkutano mkuu wa TFF kwa uwingi maalumu. Katiba ya TFF inatambua mkutano mkuu kwa maana yake ya kawaida ya watu kukutana. Hamna kifungu chochote kwenya katiba ya TFF kinachoruhusu kukutana kwa teleconference au kukutuna kwa msgs. Ukweli usiopingwa hata na Tenga mwenyewe ni kwamba hana mkutano wowote uliowahi kufanya kupitisha marekebisho ya katiba. Sasa hapa Tenga alitaka msajili wa michezo asajili nini kama yanayoitwa marekebisho ya katiba hayakuwahi kufanyika? FIFA wanaingiaje hapa? Maana aliepelekewa kusajili kinachodaiwa kuwa ni marekebisho ya katiba ya TFF ni serikali na sio FIFA. Inaendwa bila kusemwa pia kwamba kwakuwa FIFA hawakupelekewa marekebisho ya katiba kusajili, hawakuwa na ubavu wowowte wa kusema kama marekebisho ya katiba yalikuwa sahihi au haramu. Hilo loko chini ya mamlaka ya sheria za nchi ambayo FIFA katika FIFA Statutes na Regulations wanayaheshimu.

Itakuwa ni ajabu kwa ulimwengu wa leo wa sheria kuwa na taasisi ya mimataifa inayoweza kuingilia utekelezaji wa sheria za kawaida za nchi. Nionavyo mimi, viongozi wa TFF kabla hawajasimikwa kufanya kazi zao wangekuwa wanapelekwa kosi fupi ya sheria za FIFA ili kuondoa migogoro isiyokuwa na maana inayotokana na tafsiri za kibabaishaji za sheria na kanuni za FIFA.
 
Back
Top Bottom