Sakata la TBS na Ekelege | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la TBS na Ekelege

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wanitakiani, Jul 5, 2012.

 1. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wadau leo maeneo ya Mwenge nimekutana na Bw. Charles Mgeta Ekelege, aliyekuwa kibosile wa TBS akiwa kwenye gari ya Shirika la Umma lenye Na. SU 36739. Nikajiuliza maswali mengi, hivi si ndiye aliyesimamishwa kazi TBS?! Ikabidi nitumie muda wangu Wa ziada kufanya utafiti mdogo na kupata dondoo zifuatazo:

  1. Bw. Ekelege bado anapata mshahara wake kamili na si nusu mshahara Kama ilivyo kwa Watumishi wa Serikali/umma wanaposimamishwa kazi

  2. Bw. Ekelege bado anapata marupurupu yote Kama vile kutumia gari, dereva na malipo ya simu

  3. Bw. Ekelege bado anapelekewa nyumbani documents za ofisi ikiwa ni pamoja na mafaili ya ofisi. Jambo linalotekelezwa kwa ufanisi na aliyekuwa Sekretary wake kwa maelekezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Leandri Kinabo na Bibi Kezia Mbwambo, Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora

  4. Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Kinabo aliteuliwa na Bw. Ekelege kushika nafasi hiyo baada ya kusimamishwa kwake. Jambo ambalo si utaratibu kwani aliyepaswa kuteua mtu wa kukaimu ni Bodi ya TBS. Ekelege alimteua Kinabo kinyume na utaratibu kwa kuwa ni mtu wake, ambaye tangu akiwa TBS ndiye aliyekuwa akimkaimisha wakati wote ilhali wapo wakurugenzi ambao ni senior kuliko Kinabo.

  5. Bibi Kezia Mbwambo ambaye ana mahusiano ya karibu na Bibi Joyce Mapunjo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara anahusishwa ktk tuhuma na hujuma mbalimbali pamoja na Ekelege na mama huyo alitajwa ktk ripoti ya CAG. cha ajabu mama huyo hadi leo bado anadunda TBS na Bodi inapaswa kumsimamisha lkn anakingiwa kifua na bibi Joyce Mapunjo.

  6. Kuna safari inayoandaliwa ya kwenda Santiago, Chile mwezi Septemba mwaka huu ambapo ktk tiketi zinazoandaliwa yumo Mwenyekiti wa Bodi ya TBS, Charles Mgeta Ekelege na Thomas Mgeta Mnunguli. Kwanini ktk safari hiyo lipo jina la Ekelege ambaye amesimamishwa kazi? Anajumuishwaje ktk safari hiyo?

  7. Bw. Thomas Mgeta Mnunguli ni ndugu yake wa damu na Bw. Ekelege ambaye amepewa vyeo vya International Liason Officer na ndiye Head of Electrical Standard Section.

  Nimejiuliza maswali mengi, kama Ekelege alisimamishwa kazi na pengine kupisha uchunguzi kazi hiyo itafanyikaje kwa uhuru wakati Ekelege bado ana influence kubwa TBS? Kuna wafanyakazi TBS ambao ni mapandikizi ya Ekelege kama PS wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu na nduguye Bw. Thomas Mgeta Mnunguli ambao bado wanampa taarifa zote za kiofisi na hivyo kupoteza ushabidi?

  Kwanini mama Kezia Mbwambo hadi leo hajachukuliwa hatua licha ya yeye na Ekelege kutajwa kwenye ripoti ya CAG? Kwanini Ekelege alimteua Bw. Kinabo kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa TBS wakati alikwishasimamishwa kazi na huku akijua si utaratibu? Kwanini Bodi imekaa kimya? Bodi/Waziri mhusika anayajua madudu haya ya TBS? Kwanini watu wanafuja mali ya umma na kuua Watz wasio na hatia kwa kuwalisha vyakula visivyo na ubora wala viwango na wakulima kuuziwa mbolea isiyo na viwango ili kuwapa Watz umasikini?

  Who is Ekelege????
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Serikali legelege
   
 3. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Wewe hujui ile ni danganya toto? mzee yule mbali na kuwa ni mtu wa "Sistimu" ni mtu wa ndumba hatari. Kigoda ataona cheche tu na niamini mimi soon atarudishwa kazini kwa madai hakuna ushahidi wa "moja kwa moja" kumtia hatiani. So aendelee na kazi. Wewe huoni Dokta Chamiiii alivyonywea kwake?NDUMBA KWANZA, UBORA BAADAE
   
 4. obm

  obm Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mHH HUU KWELI USAANII NA NDUMBA KAMA ZIPO KAZI IPO A MMEONA MTU TOFAUTI KWA MHESHIMIWA WAZIRI NA KWAO SI NDUBA ZIPO? KWELI SRIKALI DHAIRI NI KAMA MOTO WA KIFUU
   
 5. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwenye sakata kama hili ndio tungeona ufanisi wa TISS na TAKUKURU, lkn wapi bwana!
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ajira za wakurugenzi zinataratibu zake, hata aliesimamishwa kazi anaendelea kupata huduma nyingi zinazotamkwa kwenye mkataba wake,
   
 7. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu TISS hiihii na TAKUKURU hiihii?Au kuna nyingine?Sahau, hii nchi sasa hivi Mungu ndiye anaetulinda
   
 8. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hali ni tofauti kwa Bwana Ekelege, hana mkataba wa namna hiyo aisee!
   
 9. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Magusmashi ya Siasa za Bongo. Tanzania ni zaidi ya wewe unavyoijua.
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwanza ningependa kukushukuru ndugu yangu kwa kuweka maslahi ya nchi yako mbele kwa kuakikisha unafualtilia nini kinachoendelea ndani ya system hii kwani asilimia angalau kumi ya watanzania wangefanya kama unavyofanya wewe nchi hii ingekuwa mbali sana ushauri wangu ni kwanini usimtumie hizi info. mnyika au mdee ili amuulize waziri bungeni ?? au unaweza kumpelekea kupitia ukurasa wake wa facebook au blog yake. Once again thank you for your patriotism.
   
 11. a

  andrews JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SERENGETI LONDON HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEE KWA BWIMBWI ZENU MMEPATA NINI KWA FITINA ZENU SHULE HAMNA STAAA HAMNA NI MAUNGA TU POLENI SANA:israel:
   
 12. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Tusubiri matokeo ya uchunguzi.
   
 13. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Akili kichwani.Aonaye haambiwi ona.
   
 14. h

  hans79 JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Vp chenge na hela za radar!ni nani wa kumfunga paka kengele wakati wote ni walewale?
   
 15. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Serikali legelege,
  haimuwezi Ekelege,
  watazidi kutufanya mabwege,
   
 16. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Silly government
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  tumsubir kigoda atayajibu
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  bss unafaa pombe kali wewe ni mkali
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nikiangalia na muda uliochangia napata mashaka huenda hukua unakusudia kuchangia uzi huu,,,,,
   
 20. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  TISS ya Taliban,ambayo mkuchika anaisifia kuwa imefanya kaz nzuri since 1961,wiki hii mwanzoni ameisifia sana na kuwataka watu wasiishambulie tiss yao maana hawajui walisemalo,then kuhusu TAKUKURU ni hii hii ya tanzania ambayo kwa sasa inaitwa TAASISI YA KUKUZA NA KUENDELEZA RUSHWA,inafanya kazi kwa kujitolea kama NGO fulan tu
   
Loading...