Sakata la serikali kutokuwa na imani na uraia wa wananchi wake halafu NIDA wapo kimya huo ni udhaifu

Ulirchdov

JF-Expert Member
Apr 4, 2019
356
258
Salamu kwenu wakuu

Ni muda mrefu kidogo tangu mchakato wa kuandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya utaifa umefanyika na hadi sasa wananchi wengi wa maeneo tofauti nchini wamekuwa wakisubili kupata hivyo vitambulisho.

Zoezi limefanyika likiwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa vifaa, ufinyu wa muda, uhaba wa wataalamu wa kuendesha mchakato na changamoto nyingine nyingi tu.
Wananchi wengi wamekuwa na wasiwasi juu ya ucheleweshaji wa vitambulisho ambavyo vinathibitisha uraia kitu ambacho kimesababishwa na mamlaka husika(NIDA) kushindwa kutoa vitambulisho hivyo kwa wakati.

Wasiwasi huu umechangiwa na matukio yanayoendelea kutokea nchini juu ya jeshi la polisi na uhamiaji kuwaita baadhi ya wananchi ili wakathibitishe uraia wao kisa tu serikali haina imani na uraia halisi wa wananchi wake au wanataka kutuaminisha kwamba haya matukio ya utekaji yanasababishwa na raia wasiojulikana(ambao sio raia wa Tanzania).

Kwanini NIDA wasitoe vitambulisho vya utaifa kama vipo tayari ili iwe rahisi mtu kutoa ushahidi wa nakala halisi ya kitambulisho ambacho kinathibitisha kwamba ni mtanzania halisi au ndiyo kusema kwamba hadi taarifa za wananchi zilizopo NIDA zinafanyiwa uchunguzi na vyombo hivi vya ulinzi na usalama ndo maana vitambulisho vinacheleweshwa???

Kwa hali hii NIDA wanatakiwa kujitathimini juu ya utendaji kazi wao binafsi naweza kusema ni mamlaka dhaifu kwasababu huwezi kuwa na mamlaka ya kutoa vitambulisho halafu wananchi hao hao wanaosubili vitambulisho vyao wanakumbwa na mikasa ya kushikiliwa na kuwekwa rumande kisa tu serikali haina imani na uraia wao halafu wahusika bado wapo kimya, kama ni hivyo basi karibia asilimia kubwa ya wananchi wanahisiwa na serikali kuwa sio raia halisi wa Tanzania.

Serikali pia ihakikishe inaweka mazingira rafiki ili wananchi ambao wamejiandikisha wapate vitambulisho vyao kwa wakati ili kuondoa hisia mbaya juu ya watu wake, wale ambao hawajajiandikisha pia serikali iruhusu zoezi liendelee ili watu wote wapate vitambulisho, kama NIDA ni dhaifu serikali imulike huko ili watu wasiendelee kushikiliwa kisa imani potofu.
 
Serikali yetu ipo makini sana na wanafanya kazi safi. Kikubwa tuwe wavumilivu, hili zoezi linahitaji umakini na uangalifu sana.
Tuliombee Taifa letu tufike tunakokutaka.
 
MI NINAVYOJUA NIDA INATOA VITAMBULISHO VYA AINA TATU
URAIA TANZANIA
UGENI NCHI ZA NJE
UKIMBIZI

NADHANI KUNA WALAKINI MAHALI
 
Back
Top Bottom