Sakata la Richmond: Lowassa amjibu Mwakyembe, asema asitafte mtaji wa kisiasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
New-Doc-2017-04-22_13.jpg


Ikiwa siku chache baada ya dr Mwakyembe kudai Lowasa ni muhusika mkuu wa Richmond na hachomoki waziri mkuu huyo wa zamani amjibu.

Lowasa amedai kama ana udhibitisho inatakiwa aende mahakamani sio bungeni na kwenye majukwaa ya siasa ili ubishi uishe.

Ila Lowasa akamkumbusha ukweli unajulikana hadi kwa watanzania waliompigia kura wanajua muhusika mkuu wa Richmond ni nani.

Na Mnyika adai Kikwete nae ajiandae kuja kuijibia Richmond na aiomba serikali na bunge wapeleke mswada wa kumwondolea rais kinga.

Maoni:
Waziri mkuu najua hasaini mikataba ila ni msimamizi wa serikali bungeni na wala sio mwenyekiti wa baraza la mawaziri ila Rais ndo mwenyekiti. Hii issue la msingi ni kuipeleka mahakama ya mafisadi ilianzishwa kwa nini?
 
Kuhusu kauli ya Mnyika namuunga mkono na ndio maana hata mimi nilileta huu uzi hapa chini:

Hoja ya kurudisha Bungeni sakata la Richmond iende sambamba na kuondoa kinga ya Rais

Ukweli ni kwamba ukipitia taarifa ya kamati ya Mwakyembe mwanzo mwisho huwezi kuamini kuwa yote yale yalifanyika bila bwana fulanj kujua.Ni mwendawazimu pekee ndio atakaeamini hivyo.

Mtu mwenye akili lazima ujiulize maswali haya 9 yafuatayo hapa chini:

1.Kwanini Lowassa hakuhojiwa?

2.Lowassa angehojiwa na katika kujittetea unadhani angemtaja nani?

3.Na kama angetaja mtu/watu katika kujitetea,unadhani angetaja wa chini yake tu bila kumtaja bwana fulani?

4.Je,unadhani Mwakyembe na kamati yake hawakujua hatari ya kumuhoji Lowassa?

5.Kama wangemuhoji Lowassa, unadhani Mwakyembe na timu yake walikuwa tayari kumtaja(kumu-implicate) mh.sana wa wakati huo katika taarifa yao walioiwasilisha Bungeni?

6.Wangemtaja mh.sana wa wakati huo katika ripoti yao,unadhani nini kingefuata?

7.Unadhani Lowassa nae angeweza kueleza kila kitu mbele ya Bunge kabla ya kujiuzulu?

8.Na yeye kama angeeleza ukweli wote anaoujua,unadhani nini kingefuata?

9.Unadhani angeondoka Lowassa peke yake bila fulani kuingia matatani?

Haya mambo yanawezekana tu katika nchi za wenzetu na sio huku kwetu tunakowaona kina fulani kama miungu watu.

Tuache kupotezeana muda na kudanganyana.
 
Mitambo ya Richmond ni mradi wa mashirika ya kijasusi ya marekani ikiwamo CIA,mitambo hiyo baada "ilibadilishiwa jina" na kuitwa Symbion Power.

Marekani ana tabia ya kutojihusisha na miradi yenye harufu ya ufisadi,lakini mitambo ya Richmond(baadae symbion) ilitembelewa na Rais George Bush,Rais Obama,Condoleza Rice(nadhani) na pia mama Hillarly Rodham Clinton. Hii nadhani ilikuwa ni kuwapa ishara wapiga domo kwamba "kaeni mbali na hii kitu"

Obama alizindua mradi wa AfricaPower house wenye lengo la kusambaza umeme Afrika akiwa anaitazama mitambo ya Richmond(sasa symbion power)

Pia baada ya Lowasa kuondoka madarakani,bado serikali iliendelea na bado inaendelea kununua umeme wa symbion power na hakuna transaction wala kampuni inayoonyesha ilipokea au inapokea pesa kwa niaba ya Lowasa kutokana na umeme unaouzwa na symbion power.
 
Lowasa hasafishiki hata kwa dodoki la chuma!
Uvivu wa kufikiri unasababishwa na kunywa chai yenye chumvi!
Sasa hilo dodoki la chuma litamsafishaje kama sio kumchafua damu, wanatumia kitambaa lain, wakisema nenden mahakaman kama mna ushahid wamemaliza hapo!

hii ndo TZ ya viwanda

Polonium ndio inamsumbuw Mwakyembe ubongo umeshaoza umejaa fungus.

Mwakyembe na marehemu Samuel Sitta ni watu wa ajabu sana kuwahi kutokea hapa duniani.
 
Kwa hili babu ungekaa kimya tu maana kipindi kile huyu kubenea mlimmwagia tindikali baregu mkakata mapanga,wewe ng'ang'ania mahakama tu kama hawakukuweka ndani bila dhamana miaka 50 ukafia huko hao si watu!
 
Hawa akina mwakyembe fafafafafa wote wananishangaza sana, wanasema hakuhitajika lowassa kuhojiwa maana ushahidi ulitosheleza. Kama ndivyo sasa mwalimu mzima wa sheria anataka kupeleka shauri bungeni badala ya ushahidi wake kuisaidia serikali kwenye mahakama ya mafisadi!!!?????
 
Back
Top Bottom