Sakata la Mchanga wa Dhahabu: Wanachotakiwa kufanya wapinzani

Hili la kuweka mikataba yote hadharani muhimu sana maana litawaweka MACCM mahali pabaya sana. Rasilimali za nchi ni za Watanzania wote kwanini mikataba yake iwe siri kubwa kwa Watanzania? Kuna kipi ndani ya mikataba hiyo kinachowaogopesha mpaka hawataki tuzijue details husika?

kp06112014-jpg.522112
Unless mikataba yenyewe inakataza kuwekwa hadharani. Mtanange huo.
 
Lowasa na Sumayi ni wana chama wa chadema, sasa watalieleza vipi hili suala mbele ya wananchi na wakaeleweka wakati na wao ndio walikua wahusika wakuu kipindi mikataba hii ilipokua ikipitishwa.
Inatakiwa watulezee jinsi mikataba ilivyopitishwa na walihisika vipi kuipitisha hii mikataba bila kuficha jambo lolote ili tuelewe ilikuaje mpaka wakakubali kupitisha hii ya unyonyaji.
Umenena vyema mkuu!
 
Tofauti na wapinzani ambao ni kama swali hili wamemuachia zaidi Lissu,CCM swala hili sasa limekuwa ni kama agenda yao ya kitaifa kwa kutaka kujaribu kuamisha umma kuwa wao na Magufuli ndio wana uchungu na hili jambo na wapinzani hasa Lissu wanatumika kutetea wazungu wa ACACIA.

Hawa wenzetu sasa hivi kila anaepata fursa ya kuongea na wananchi hii ndio imekuwa ni agenda yao ya majukwaani kwamba Lissu na CHADEMA wanatetea wezi wa Rasilimali za nchi kitu ambacho si kweli.

CHADEMA kama chama cha siasa hivi sasa kinatakiwa kuweka mkakati wa kukabiliana na propaganda hii kwa kuelekeza kila mbunge alitolee ufafanuzi jambo hili kwa wananchi wake tena kwa kueleza historia nzima ya namna sheria hizi zilivyopitishwa Bungeni kwa hati ya dharura na pia kuwaeleza /kuwakumbusha wananchi kuwa ni Lissu aliwahi wekwa ndani kwa kupinga uwekezaji huu wa kifisadi katika migodi.

Chama pia kinapaswa kuita waandishi wa habari na kufafanua jambo hili mara baada ya Ripoti ya Pili kutolewa hiyo Jumatatu maana ni lazima CHADEMA itatajwa tu hata kwa mafumbo lakini mnaweza pia kusubiri mjadala wa Bajeti upite kwanza ili tusiwe na agenda mbili muhimu kwa wakati mmoja pasipo na ulazima wowote.

Pia mnapaswa kutoa press release kwenye magazeti,n.k mkieleza kwa mapana na marefu historia ya juu ya jambo hili na jinsi mlivyolipiganga tangu mwanzo ila hamkusilikilizwa na muelezi pia ni njia gani mmekuwa mkishauri zifuatwe ili kumaliza tatizo hili.

Wapinzani ombeni hata airtime kwenye redio na tv kufafanua jambo hili na kuwakumbusha wananchi tumefikaje hapa na hatari inayoweza kutukumba huko baade busara ikikosekana katika kutatua mgogoro huu.

CHADEMA tusitegemee clip tu za mitandaoni katika kukabiliana na hili jambo bali tunapaswa kuenda mbali zaidi ya hapo.

Jambo hili wapinzani msiishie kulijadili tu ndani ya Bunge na kumuachia Tundu Lissu bali kwa sasa inafaa iwe ni agenda ya chama katika kulitolea ufafanuzi na kujibu propaganda hizi za CCM.

Katibu Mkuu wa CHADEMA naomba jambo hili sasa lipewe uzito unaostahili.

CC: Tumaini Makene
Jambo muhimu ni kugoma kusupport budget ya wizara ya madini mpka mikataba yote ya madini iletwe bungeni ili wabunge waisome...hiyo mikataba ndio tatizo kubwa isipowekwa wazi tutajua sizonje yuko location kma bashite
 
Lowasa na Sumayi ni wana chama wa chadema, sasa watalieleza vipi hili suala mbele ya wananchi na wakaeleweka wakati na wao ndio walikua wahusika wakuu kipindi mikataba hii ilipokua ikipitishwa.
Inatakiwa watulezee jinsi mikataba ilivyopitishwa na walihisika vipi kuipitisha hii mikataba bila kuficha jambo lolote ili tuelewe ilikuaje mpaka wakakubali kupitisha hii ya unyonyaji.
Unajua Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu ni kwamba mwenye serikali ni Rais na si Lowassa wala Sumaye waliowahi kuwa Rais wa nchi hii. Mikataba yote huingiwa kwa niaba ya Rais na hakuna hata mkataba mmoja unaosainiwa na Waziri Mkuu. Umeshawahi kusikia kwamba Waziri Mkuu anaingia mkabata kwa niaba ya nchi bila ya Rais kuridhia?

Wanaohusika na hiyo mikataba ni Mkapa na Kikwete.
 
Hili la Lowasa na Sumaye, umelileta wakati mwafaka kwani walikuwa Mawaziri Wakuu.

Sumaye ambaye wakati wake ndiyo mikataba hiyo ilisainiwa, na Mh Lissu alilipigia kelele sana na kutishiwa kuwekwa kizuizini, imekuaje leo hii ni washirika!!

Tusubiri ripoti ya Tume ya Pili kujua pumba na mchele.
 
Unajua Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu ni kwamba mwenye serikali ni Rais na si Lowassa wala Sumaye waliowahi kuwa Rais wa nchi hii. Mikataba yote huingiwa kwa niaba ya Rais na hakuna hata mkataba mmoja unaosainiwa na Waziri Mkuu. Umeshawahi kusikia kwamba Waziri Mkuu anaingia mkabata kwa niaba ya nchi bila ya Rais kuridhia?

Wanaohusika na hiyo mikataba ni Mkapa na Kikwete.
Nyie komalieni na mikakati ya kubadilisha hii mikataba. Upinzani ukianza kufukua makaburi basi humo mtaingia nyinyi. Hili ni onyo angalizi.
 
Tofauti na wapinzani ambao ni kama swali hili wamemuachia zaidi Lissu,CCM swala hili sasa limekuwa ni kama agenda yao ya kitaifa kwa kutaka kujaribu kuamisha umma kuwa wao na Magufuli ndio wana uchungu na hili jambo na wapinzani hasa Lissu wanatumika kutetea wazungu wa ACACIA.

Hawa wenzetu sasa hivi kila anaepata fursa ya kuongea na wananchi hii ndio imekuwa ni agenda yao ya majukwaani kwamba Lissu na CHADEMA wanatetea wezi wa Rasilimali za nchi kitu ambacho si kweli.

CHADEMA kama chama cha siasa hivi sasa kinatakiwa kuweka mkakati wa kukabiliana na propaganda hii kwa kuelekeza kila mbunge alitolee ufafanuzi jambo hili kwa wananchi wake tena kwa kueleza historia nzima ya namna sheria hizi zilivyopitishwa Bungeni kwa hati ya dharura na pia kuwaeleza /kuwakumbusha wananchi kuwa ni Lissu aliwahi wekwa ndani kwa kupinga uwekezaji huu wa kifisadi katika migodi.

Chama pia kinapaswa kuita waandishi wa habari na kufafanua jambo hili mara baada ya Ripoti ya Pili kutolewa hiyo Jumatatu maana ni lazima CHADEMA itatajwa tu hata kwa mafumbo lakini mnaweza pia kusubiri mjadala wa Bajeti upite kwanza ili tusiwe na agenda mbili muhimu kwa wakati mmoja pasipo na ulazima wowote.

Pia mnapaswa kutoa press release kwenye magazeti,n.k mkieleza kwa mapana na marefu historia ya juu ya jambo hili na jinsi mlivyolipiganga tangu mwanzo ila hamkusilikilizwa na muelezi pia ni njia gani mmekuwa mkishauri zifuatwe ili kumaliza tatizo hili.

Wapinzani ombeni hata airtime kwenye redio na tv kufafanua jambo hili na kuwakumbusha wananchi tumefikaje hapa na hatari inayoweza kutukumba huko baade busara ikikosekana katika kutatua mgogoro huu.

CHADEMA tusitegemee clip tu za mitandaoni katika kukabiliana na hili jambo bali tunapaswa kuenda mbali zaidi ya hapo.

Jambo hili wapinzani msiishie kulijadili tu ndani ya Bunge na kumuachia Tundu Lissu bali kwa sasa inafaa iwe ni agenda ya chama katika kulitolea ufafanuzi na kujibu propaganda hizi za CCM.

Katibu Mkuu wa CHADEMA naomba jambo hili sasa lipewe uzito unaostahili.

CC: Tumaini Makene
Mmechelewa sana. Wakati ule Lissu analikuwa anawatumikia na kuwakuwadia mabwana zake waliokuwa na hasira kwa kuikosa migodi na sasa anawakuwadia wezi wa madini yetu.

Hatudanganyiki. Huyo kama kweli ana uchungu, ni haungi hatua iliyopigwa na rais dhidi ya wizi huo?
 
Lowasa na Sumayi ni wana chama wa chadema, sasa watalieleza vipi hili suala mbele ya wananchi na wakaeleweka wakati na wao ndio walikua wahusika wakuu kipindi mikataba hii ilipokua ikipitishwa.
Inatakiwa watulezee jinsi mikataba ilivyopitishwa na walihisika vipi kuipitisha hii mikataba bila kuficha jambo lolote ili tuelewe ilikuaje mpaka wakakubali kupitisha hii ya unyonyaji.

Mtoa mada anatafuta cheap points lakini kasahau Lowassa na Sumaye wako Chadema. Sumaye alikuwa waziri mkuu miaka 10, akapokewa kijiti na Lowassa. Kipindi hicho ndio mikataba mibovu ilipitishwa kama mvua. Sumaye hakuishia hapo, alisimamia Bunge likapitisha muswada wa Takrima. Madalali watapata shida.
 
Hivi Lowassa na Sumaye wana kinga ya kutoshitakiwa?

Hivi si nyie ndio mliunda Mahakama ya Mafisadi?

Mbona mnakuwa watu wa majungu?!
 
Binafsi nafikiri Mashinji na Makene wamekuwa wakimya kupita stahiki ya watu kama wao. Mashinji kama katibu mkuu alipaswa proactive, creative na aggressive katika issues kama hizi.

Sasa Salary Sleep, mapendekezo yako akikutana na ombwe la namna fulani chamani hayatafanyiwa kazi wakati mimi na wengi tunaamini kuwa kitengo cha propaganda cha Chadema (licha ya kubinywa kiaina na sizo) bado kina nafasi ya kufanya kitu ili kuwafanya wananchi wasiendelee kupotoshwa na CCM ambao bila shaka yoyote ndiyo waliouza nchi yetu na raslmali kwa majizi halafu leo kujifanya watetezi wakuu.

Wadau, kama katibu mkuu chadema anapwaya kuna busara ya kutafuta mtu atakayeiweza hiyo kazi. Katibu mkuu ndiyo mtendaji mkuu. Zamani za Dr Slaa (hata kama alikwishaboronga) mpaka watoto wadogo walimfahamu. Najua Sizo kabana kiasi lakini kamati tendaji chini ya kamanda Mbowe inaweza kusaidia kuondoa ombwe linaloonekana.

Salary Sleep, hoja yako ina mashiko ya ukweli na wengine walioongeza nguvu kwenye pendekezo lako, natamani mngesikilizwa na uongozi ili kwa pamoja tupambane vema udhalimu wa CCM hasa katika suala tajwa!
 
Umeongea point kubwa sana, et sahz ccm wana uchungu na mali za Tz, wez wakubwa hawa!! Inatakiwa iwe ajenda ya kitaifa kupinga hadaa zao, kama wanabadili mikataba inabid wafanye hivyo huku wanaomba msamaha!! Maana nchi hii haijawahi kutawaliwa na wengine zaid ya ccm
 
Mkuu umeongea jambo la maana na linahitaji utekelezaji wa haraka. Umekosea tu hapo ulipomtaja huyo katibu mkuu domo zege. Huyo katibu mkuu hana jipya ni mzigo kama mizigo mingine.
Hapana, hapa ndipo mahali ofisi yake yapaswa kuchukua jukumu lake kisiasa. Vinginevyo hafai!!!
 
Mfano mzuri wa sakata la mchanga ni sawa na mwenye nyumba akimsainisha mkataba mpangaji wakati wa kulipa kodi hakuna namna ambapo mwenye nyumba anaweza kuubadili mkataba kabla haujaisha na akilazimisha kuuvunja mkataba basi kuna hatari ya mwenye nyumba kulipa fidia.

Serikali zilizopita zilipitisha hii mikataba hii mibovu ya madini kwa miaka mingi kiasi kwamba haya mapungufu tunayoyaona ni matokeo tu.

Watanzani ni vyema tutambue kuwa hiyo gharama ya fidia kwa kuivunja hii mikataba mibovu itatupeleka pahala pabaya sana kiuchumi.
 
Umeandika kisomi sana ! Naomba niongeze kidogo kwamba hata hii bajeti , NI LAZIMA UKAWA ISAMBAZE UKWELI KWAMBA BAJETI YA MWAKA ULIOPITA ILIFELI KWA 66% , NA WAAMBIWE HATA ZILE 50ML ZA KILA KIJIJI MMETAPELIWA .
 
Dr. Mashinji naamini unapitia humu nawe unayaona maoni haya. It's time you act brother. Au unamwonea aibu homeboy. Yeye hana aibu anaweza kukuchinja huku ukimtazama na asipepese macho. Katibu Mkuu ni Injini ya ya Chama, na Injini ni lazima iungurume kusababisha mwendo.
 
Hili la kuweka mikataba yote hadharani muhimu sana maana litawaweka MACCM mahali pabaya sana. Rasilimali za nchi ni za Watanzania wote kwanini mikataba yake iwe siri kubwa kwa Watanzania? Kuna kipi ndani ya mikataba hiyo kinachowaogopesha mpaka hawataki tuzijue details husika?

kp06112014-jpg.522112
Noma sana !
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Umeongea point kubwa sana, et sahz ccm wana uchungu na mali za Tz, wez wakubwa hawa!! Inatakiwa iwe ajenda ya kitaifa kupinga hadaa zao, kama wanabadili mikataba inabid wafanye hivyo huku wanaomba msamaha!! Maana nchi hii haijawahi kutawaliwa na wengine zaid ya ccm

Wasema ... et sahz ccm wana uchungu na mali za Tz ... , kwa kuwa hoja iibuliwa na Rais Magufuli! Unajua ni kwa nini?

Mh Lissu, mwanasheria na bingwa wa kukosoa, kwa sauti kubwa na mbwembwe nyingi za ujuaji, amekuwa mbuge vipindi vingi tu, kwa nini apandie kwenye hoja ya Rais Magufuli, sasa hivi, asiliibue bungeni kwa kuwa alikwisha lishupalia hapo awali, anavyodai!
 
Back
Top Bottom