Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,705
- 149,938
Tofauti na wapinzani ambao ni kama swali hili wamemuachia zaidi Lissu,CCM swala hili sasa limekuwa ni kama agenda yao ya kitaifa kwa kutaka kujaribu kuamisha umma kuwa wao na Magufuli ndio wana uchungu na hili jambo na wapinzani hasa Lissu wanatumika kutetea wazungu wa ACACIA.
Hawa wenzetu sasa hivi kila anaepata fursa ya kuongea na wananchi hii ndio imekuwa ni agenda yao ya majukwaani kwamba Lissu na CHADEMA wanatetea wezi wa Rasilimali za nchi kitu ambacho si kweli.
CHADEMA kama chama cha siasa hivi sasa kinatakiwa kuweka mkakati wa kukabiliana na propaganda hii kwa kuelekeza kila mbunge alitolee ufafanuzi jambo hili kwa wananchi wake tena kwa kueleza historia nzima ya namna sheria hizi zilivyopitishwa Bungeni kwa hati ya dharura na pia kuwaeleza /kuwakumbusha wananchi kuwa ni Lissu aliwahi wekwa ndani kwa kupinga uwekezaji huu wa kifisadi katika migodi.
Chama pia kinapaswa kuita waandishi wa habari na kufafanua jambo hili mara baada ya Ripoti ya Pili kutolewa hiyo Jumatatu maana ni lazima CHADEMA itatajwa tu hata kwa mafumbo lakini mnaweza pia kusubiri mjadala wa Bajeti upite kwanza ili tusiwe na agenda mbili muhimu kwa wakati mmoja pasipo na ulazima wowote.
Pia mnapaswa kutoa press release kwenye magazeti,n.k mkieleza kwa mapana na marefu historia ya juu ya jambo hili na jinsi mlivyolipiganga tangu mwanzo ila hamkusilikilizwa na muelezi pia ni njia gani mmekuwa mkishauri zifuatwe ili kumaliza tatizo hili.
Wapinzani ombeni hata airtime kwenye redio na tv kufafanua jambo hili na kuwakumbusha wananchi tumefikaje hapa na hatari inayoweza kutukumba huko baade busara ikikosekana katika kutatua mgogoro huu.
CHADEMA tusitegemee clip tu za mitandaoni katika kukabiliana na hili jambo bali tunapaswa kuenda mbali zaidi ya hapo.
Jambo hili wapinzani msiishie kulijadili tu ndani ya Bunge na kumuachia Tundu Lissu bali kwa sasa inafaa iwe ni agenda ya chama katika kulitolea ufafanuzi na kujibu propaganda hizi za CCM.
Katibu Mkuu wa CHADEMA naomba jambo hili sasa lipewe uzito unaostahili.
CC: Tumaini Makene