Kuna haja ya kuelimishana humu somo la Civics, ili watu wajue tofauti ya waziri na naibu waziri, makumu yao ni yapi na dhana nzima ya kuwajibika!.
Prof. Muhongo amewajibishwa kutokana na position yake na sio kumaanisha anahusika.
Edward Lowassa alipojiuzulu aliwajibika na sio alihusika.
Hata Mwinyi akiwa waziri wa mambo ya ndani, aliwahi kuwajibika kwa vifo vya mahabusu kule Mwanza.
Kunapotokea madudu wizara fulani, anayewajibika ni mmoja tuu, waziri, ambaye ni mjumbe wa Cabnet, alipaswa kujua kijachoendelea. Naibu waziri hana shughuli yoyote zaidi ya kujibu maswali bungeni, na kusaidia kumwakilisha waziri wakati waziri hayupo, lakini hata pale inapotokea waziri hayupo, NW sio mjumbe wa cabinet, sasa umwajibishwe kwa lipi?.
Uwajibikaji kwa waziri na naibu wake uliwahi kutokea mara tuu Wizara ya Uchukuzi kwa Waziri Nundu na Naibu wake, Eng. Futakamba kushindwa kuelewana, hivyo wote wakapigwa chini.
Kalemani ndio anasuburia kuibeba mikoba ya Muhongo.
P.