Sakata la Mchanga: Naibu Waziri wa Nishati na Madini kaponaje?

Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani mbona yeye hajawajibishwa katika sakata hili la mchanga wa dhahabu?

Kama hoja ni muda aliokaa kwenye hiyo wizara,mbona Mama Kilango aliwajibishwa bila kujali muda aliokuwa amekalia kiti kama Mkuu wa Mkoa?

Ni kweli muda aliokaa Naibu Waziri ni mfupi kiasi cha yeye kutoguswa?
Usishangae kesho akiwa waziri kamili
 
Kuna haja ya kuelimishana humu somo la Civics, ili watu wajue tofauti ya waziri na naibu waziri, makumu yao ni yapi na dhana nzima ya kuwajibika!.

Prof. Muhongo amewajibishwa kutokana na position yake na sio kumaanisha anahusika.
Edward Lowassa alipojiuzulu aliwajibika na sio alihusika.
Hata Mwinyi akiwa waziri wa mambo ya ndani, aliwahi kuwajibika kwa vifo vya mahabusu kule Mwanza.

Kunapotokea madudu wizara fulani, anayewajibika ni mmoja tuu, waziri, ambaye ni mjumbe wa Cabnet, alipaswa kujua kijachoendelea. Naibu waziri hana shughuli yoyote zaidi ya kujibu maswali bungeni, na kusaidia kumwakilisha waziri wakati waziri hayupo, lakini hata pale inapotokea waziri hayupo, NW sio mjumbe wa cabinet, sasa umwajibishwe kwa lipi?.

Uwajibikaji kwa waziri na naibu wake uliwahi kutokea mara tuu Wizara ya Uchukuzi kwa Waziri Nundu na Naibu wake, Eng. Futakamba kushindwa kuelewana, hivyo wote wakapigwa chini.

Kalemani ndio anasuburia kuibeba mikoba ya Muhongo.

P.
Umempa huyu mtoto majawabu jarabati kabisa. Pia huenda Muhongo msimamo wake upo wazi kulingana na ushauri wake kwenye baraza la mawaziri ambamo Kalemani haingii.
Kuongeza katika kumbukumbu zako sawa hata Prof Mbilinyi aliondoka na manaibu wake Kilonzi Mpolongonyi na mwingine alikuwa Mzanzibari Seif Khatibu. Ilikuwa swala la minofu ya samaki.
 
Pia huyu naibu alishakuwa mwanasheria hapo wizarani, alihusikaje na mikataba inayotupa shida?
 
Pia huyu naibu alishakuwa mwanasheria hapo wizarani, alihusikaje na mikataba inayotupa shida?
Nani kakwambia Mh Rais anahangaika na walioandika mkataba? Unajua kihelehele chenu ni cha kipumbavu sana. Mikataba kahangaikieni nyie na wazazi wenu na wakweni kwa sasa.
Mh Rais atatoa uamuzi juu ya mikataba pale tume ya pili itakapokamilisha kazi na kutoa taarifa yake na mapendekezo. Kwa sasa mkome kuongelea mikataba na sheria.
 
Povu
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani mbona yeye hajawajibishwa katika sakata hili la mchanga wa dhahabu?

Kama hoja ni muda aliokaa kwenye hiyo wizara,mbona Mama Kilango aliwajibishwa bila kujali muda aliokuwa amekalia kiti kama Mkuu wa Mkoa?

Ni kweli muda aliokaa Naibu Waziri ni mfupi kiasi cha yeye kutoguswa?
Tusifukue makaburi
 
Jambo la kusikitisha katika sakata hili la mchanga wa dhahabu ni kuona jinsi ambavyo viongozi wa nchi hii wasivyoona aibu na kutotaka kuwajibika. Mbunge wa Chato na Naibu Waziri Madini na Nishati, Dr. Medard Kalemani kabla ya uteuzi wa kuwa naibu waziri, alikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Madini na Nishati kwa miaka mingi, na mikataba mingi mibovu inayozungumziwa sasa ya madini aliiyona na kuisimamia kama mtumishi wa umma. Leo anadiriki vipi kuendelea kubaki na wadhifa wake huo huku akijua mikataba hiyo yenye matatizo aliisimamia yeye? Haoni hata aibu kuendelea na nafasi hiyo? Jambo la msingi angejiuzulu ili amsaidie Rais Magufuli maamuzi kuhusu nafasi ya kuteua waziri na naibu wake. Fanya heshima kwa kaka yako na wewe atakuheshimu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom