Sakata la Mchanga: Naibu Waziri wa Nishati na Madini kaponaje?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,315
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani mbona yeye hajawajibishwa katika sakata hili la mchanga wa dhahabu?

Kama hoja ni muda aliokaa kwenye hiyo wizara,mbona Mama Kilango aliwajibishwa bila kujali muda aliokuwa amekalia kiti kama Mkuu wa Mkoa?

Ni kweli muda aliokaa Naibu Waziri ni mfupi kiasi cha yeye kutoguswa?
 
Tena huyu ndie aliehusika kutunga sheria mbovu za madini wakati alipokuwa mkurugenzi wa sheria nishati na madini
 
Hawezi kumtumbua mbunge wa Chatto hata msema nini
Mnadhani huyo ni Yeriko Nyerere

[HASHTAG]#westillrememberyoubensaa8[/HASHTAG]
 
Mkuu kuteuliwa kuwa waziri au naibu waziri kunaambatana na job description.
Yawezekana hausiki kwa namna mmoja au nyingine na maamuzi ya migodi ya dhahabu kutokana na wadhifa wake wizarani.
 
ivi kwani wahusika ambao saini zao ndio zipo kwenye mkataba wako wapi wametafutwa wakaulizwa nini kilitokea? au kama walipitia hiyo mikataba kwanza kabla ya kusaini [FONT]
 
Mkuu kuteuliwa kuwa waziri au naibu waziri kunaambatana na job description.
Yawezekana hausiki kwa namna mmoja au nyingine na maamuzi ya migodi ya dhahabu kutokana na wadhifa wake wizarani.
Kama kweli kulikuwa na wizi,ina maana alikuwa hajui nini kinaendelea katika wizara yake?
 
Yataka moyo kumuunga mkono huyu bwana!!
Huyo Kalemani ndiyo atakayepokea kijiti ya Muhongo. Huyo ndiyo Waziri wa Nishati na Madini mkitaka msitake, mkinuna, mkicheka Kalemani Waziri mpya wa Nishati na Madini!!!!
 
Tasnifu yake ya Ph.D inahusu mlinganisho wa sheria za madini katika nchi za Tanzania, Namibia, Botswana na Afrika Kusini na ni mbobevu sana wa haya mambo. Amekuwa pale wizarani kwa muda mrefu na ni wazi anafahamu kila kitu. Lakini pia ndiye aliyeachiwa ubunge wa Chato na Mr. President. Hakuna kitakachofanyika...
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani mbona yeye hajawajibishwa katika sakata hili la mchanga wa dhahabu?

Kama hoja ni muda aliokaa kwenye hiyo wizara,mbona Mama Kilango aliwajibishwa bila kujali muda aliokuwa amekalia kiti kama Mkuu wa Mkoa?

Ni kweli muda aliokaa Naibu Waziri ni mfupi kiasi cha yeye kutoguswa?
Kuna haja ya kuelimishana humu somo la Civics, ili watu wajue tofauti ya waziri na naibu waziri, makumu yao ni yapi na dhana nzima ya kuwajibika!.

Prof. Muhongo amewajibishwa kutokana na position yake na sio kumaanisha anahusika.
Edward Lowassa alipojiuzulu aliwajibika na sio alihusika.
Hata Mwinyi akiwa waziri wa mambo ya ndani, aliwahi kuwajibika kwa vifo vya mahabusu kule Mwanza.

Kunapotokea madudu wizara fulani, anayewajibika ni mmoja tuu, waziri, ambaye ni mjumbe wa Cabnet, alipaswa kujua kijachoendelea. Naibu waziri hana shughuli yoyote zaidi ya kujibu maswali bungeni, na kusaidia kumwakilisha waziri wakati waziri hayupo, lakini hata pale inapotokea waziri hayupo, NW sio mjumbe wa cabinet, sasa umwajibishwe kwa lipi?.

Uwajibikaji kwa waziri na naibu wake uliwahi kutokea mara tuu Wizara ya Uchukuzi kwa Waziri Nundu na Naibu wake, Eng. Futakamba kushindwa kuelewana, hivyo wote wakapigwa chini.

Kalemani ndio anasuburia kuibeba mikoba ya Muhongo.

P.
 
Hii ndo double-standard tunayosikia ikifeli wizara ni wangapi wanatakiwa kuwajibishwa. Na mbona kale ka tume ka madini kamepigwa pasi mkausho? Au kuna watu wamelengwa ili kujipatia maujiko hasi.
 
Back
Top Bottom