SAKATA LA MAWAKILI BINAFSI: AG lawamani........................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SAKATA LA MAWAKILI BINAFSI: AG lawamani...........................

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,780
  Likes Received: 416,595
  Trophy Points: 280
  SAKATA LA MAWAKILI BINAFSI: Wanasheria wa Serikali watupa lawama kwa AG
  Monday, 27 December 2010 08:48 James Magai
  BAADHI ya wanasheria waliowekewa pingamizi na serikali wasisajiliwe kuwa mawakili binafsi, wamelalamikia kuwa kitendo ni uonevu mkubwa. Wanasheria 50 waliwekewa pingamizi na serikali wakati wa sherehe za 42 za usajili wa mawakili wapya zilizofanyika Desemba 17, mwaka huu, viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Waliozuiwa ni watumishi wa umma wanaofanya shughuli za kisheria chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na walioko kwenye mashirika, taasisi na wakala mbalimbali wa serikali.
  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG), George Masaju, alilieleza Mwananchi kuwa wanasheria hao wamewekewa pingamizi hilo kwa sababu walikiuka sheria Namba 4 ya mwaka 2005 ya Ofisi ya AG.
  Masaju alisema kwa mujibu wa sheria hiyo na kanuni zake za mwaka 2006, wakili wa serikali, ofisa wa sheria au mtumishi yeyote anayefanya shughuli za kisheria kwenye shirika, taasisi au wakala wa serikali ni kinyume cha sheria kuwa wakili wa kujitegemea.
  Alisema kitendo walichofanya waombaji hao ambao ni watumishi wa umma, ni ukiukaji sheria hiyo na kanuni zake hususan kifungu cha 8 (2) cha kanuni.
  Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, wakili wa serikali, mwanasheria au ofisa yeyote anayefanya shughuli za kisheria, haruhusiwi kufanya shughuli za uwakili binafsi.
  Hata hivyo, wakizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya wanasheria hao waliowekewe pingamizi walisema kitendo walichofanyiwa ni uonevu na kwamba, walifanyiwa kwa nia mbaya.
  Walalamikaji hao ambao hawakutaka kutajwa, pia walimtupia lawama Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria kwa kukubaliana na pingamizi hiyo na kuwaengua kwenye orodha ya waombaji waliosajiliwa siku hiyo.
  Mawakili hao walidai kuwa, hata serikali ilijua pingamizi lao halikuwa na msingi na kwamba, ndio maana walivizia na kulitoa dakika za mwisho wakati wakisubiri kusajiliwa na kukabidhiwa vyeti.
  Walidai kuwa, wakati wakifanyiwa usaili mbele ya baraza hilo, AG au mwakilishi wake alikuwepo maana yeye ni mjumbe muhimu ambaye asipokuwepo yeye au mwakilishi wake hakuna usaili unaofanyika.
  “Tulimaliza usaili Septemba mwaka huu, lakini la ajabu serikali inakuja kutuwekea pingamizi siku ya usajili, sasa muda wote huo ilikuwa wapi?” alihoji mmoja wamawakili hao.
  Kuhusu maelezo ya DAG kuwa, hatua hiyo ni kinyume cha sheria, mlalamikaji huyo alisema kinachozuiliwa na sheria hiyo ni kufanya shughuli za uwakili binafsi sio kusajiliwa na kutambuliwa na Chama cha Wanasheria nchini (TLS).
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,780
  Likes Received: 416,595
  Trophy Points: 280
  Kweli hii serikali ni bora liende tu.......iwaje mtu azuiwe kuwa wakili anayejitegemea kwa sababu ameajiliwa serikalini?

  Yaani akose huduma zitolewazo na Chama cha Wanasheria nchini kwa vile ni mwajiriwa serikalini.........................
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi huko nyuma wapo mawakili wa serikali ambao pia kwa wakati huo huo walikuwa mawakili wa kujitegemea?
   
 4. Hiphop

  Hiphop Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hao wafanyakazi wa serikali waache lawama zisizo na msingi,sheria ipo wazi na wao walilijua hilo,walichofanya ni kuijaribu serikali ili waone kama wamelala.Kati ya hao 50 kuna ambao hawakuwa mawakili wa serikali lakini walikataliwa kuapishwa baada ya report ya tabia zao kuwekwa wazi,kuna walioonyesha utovu wa nidhamu walipokuwa field pale kwenye ofisi za AG na yupo aliyekataliwa kuapisha baada ya kujitambulisha kama wakili kwenye vyombo vya habari wakati bado hajaapishwa,hiyo ilikuwa ni unqualified practice.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi wakiapishwa tu na kusajiliwa lakini wasipewe Certificate of Practice hapo Sheria inasemaje? Naomba utusaidie Regulations alizotamka DAG George Masaju kama utakuwa nazo kwenye soft copy!
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakubwa mmepotelea wapi?
   
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mwaka 2005 (The Attorney General (Discharge of Duties) Act. No. 4 of 2005 http://www.bunge.go.tz/Polis/PAMS/Docs/4-2005.pdf ) ilitungwa kwa makusudi kabisa ya kutaka kuwatenganisha wanasheria Serikali na sio kuweka mfumo mzuri wa utendaji kazi miongoni mwa wanasheria hawa wa Serikali ambao kwa muda mrefu ndio wamekuwa wakitumainiwa kuwa ndio wenye upeo na uelewa mpana wa masuala ya sheria kwa kuwa wanahusika katika kutekeleza majukumu ya umma hali kadhalika kushirikina na sekta binafsi.
  Sheria hii mbali na "ku-restablish" Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ile ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), ambazo zipo kikatiba, haina mambo yoyote ya msingi ya kuboresha sekta ya sheria wala masslhai ya wanasheria katika utumishi wa umma.


  Mbali na sheria hii, kwa lengo la kuwatenganisha wanasheria hawa katika sekta ya umma, Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilipitisha Kanuni za Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Tangazo la Serikali Na. 154 la Tarehe 3 Novemba, 2006). Kanuni hizi hazina mambo ya msingi sana kuhusu taaluma ya wanasheria hao zaidi yak u-redefine yale ambayo yapo katika sheria na nyaraka nyingine za Utumishi wa Umma kuhusu maadili ya watumishi wa Umma.
  Kanuni hizi amoja na masula mengine , zinabainisha katika Kanuni ya 6 kuwa "wakili wa Serikali, Afisa sheria na Mwansheria yeyote katika Utumishi wa Umma atakuwa na haki sawa na Wakili Binafis (Advocate).


  Aidha, tofauti na inavyodaiwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hakuna kifungu chochote katika Sheria ya Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali ya Mwaka 2005 na wala Kanuni zake za Mwaka 2006 zinazobainisha kuzuia Wakili wa Serikali au Afisa Sheria kupishwa kuwa Wakili.
  Kupitia Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba 3 wa Mwaka 2007 uliotolewa tarehe 17 Septemba, 2007 na kuanza kutumika Julai, 2007 na ambao ulisainiwa na Katibu Mkuu, Manajemejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi, unabainisha katika Ibara ya 2 na 3 kuwa:

  2. Kufuatia utekelezaji wa Sheria ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Namba 4 ya Mwaka 2005, Wanasheria wote wanaotekeleza kazi zao kwa mujibu wa sheria zinazosimamiwa na taasisi zao na siyo Mwansheria Mkuu wa Serikali, na ambao hawawajibiki kwa Mwansheria Mkuu wa Serikali moja kwa moja wanpotekeleza majukumu yao ya kila siku, wameondolewa chini ya Usimamizi wa moja kwa moja wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


  Waraka huo unaendelea kubainisha kuwa wanasheria walioondolewa kutoka usimamizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni pamoja na Mawakili wa Serikali waliopo katika Utumishi wa Serikali za Mitaa, Wizara, Idara na Taasisi nyinginezo nje ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wasajili Hati Wasaidizi na wengineo.

  Waraka unaeleza katika Kipengele cha 3 kuwa Wanasheria ambao hawapo chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali watatambulika kama "Maafisa Sheria" au kiingereza "Legal Officers".
  Waraka pia unaweka muundo mpya wa Utumishi wa Maafisa Sheria hao na kuweka bayana kuwa mamlaka ya uajiri na nidhamu ya Maafisa Sheria itakuwa ni Mamlaka zao za ajira ambazo zimebainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 na Kanuni zake za Mwaka 2003. Kwa mujibu wa Sheria hii ya Utumishi wa Umma, ajira za wanasheria walipo nje ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zinasimamiwa ni Makatibu wakuu, Wakurugenzi au watendaji wakuu wa Wizara, Idara, au Taasisi husika ya Umma na sio Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Aidha, ni upotofu wa Sheria kudhani kuwa Mwansheria akiapishwa kuwa wakili basi moja kwa moja anaweza kufanya kazi ya uwakili paipo hata kuwa na cheti cha kufanya kazi hiyo kinachotolewa na chini ya Sheria ya Mawakili. Kwa upande mwingine, hata Sheria za Utumishi wa Umma au hata hiyo ya Mwansheria Mkuu wa Serikali haizuii kwa mwanasheria ambae ameapishwa na kufanya kazi kama wakili binafsi kuomba kazi kuwa wakili wa Serikali au Afisa Sheria iwapo nafsi hiyo itatangazwa Serikalini.
  Msingi wa Mwansheria Mkuu kuzuia wanasheria katika Sekta ya Umma kutoapishwa unajengwa na dhana ya kuzuia mgongano wa maslahi. Hata hivyo, suala la mgongano wa mslahi ni jambo binafsi sana kuliko fani (professional) kwani ikiwa ni mgongano wa maslahi, Serikali ingezuia hata Madaktari, Wahasibu na wanataaluma wengine walipo Serikalini wasifungue ofisi binafsi.


  Kama itatazamwa kwa kina, suala la utovu wa maadili ya kisheria pengine lingeanzia kwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu ambapo katika miaka ya hivi karibuni, tumehsuhudia Mshauri Mkuu wa Sheria wa Serikali (AG) akituhumiwa kwa kutumia madaraka yake vibaya katika sakata la ununuzi wa Rada na pia watendaji wa ofisi hiyo wakihusishwa na kadhia kama la Richmond nk.


  Ikiwa mtimzamo huu hautabadilika na kuendelea kuzuia wanasheria waliopo katika serkta ya umma kuapishwa, athari yake ni kupungua kwa idadi ya mawakili Tanzania ukilinganisha na wenzetu wa Afrika ya Mashariki. Pengine, mtazamo wa Mwanasheria Mkuu kuzuia wanasheria wasiapishwe unaweza kujenga matabaka katika utumishi wa umma kwani mpaka hizi sasa wapo wanasheria ambao ni mawakili wa kujitegemea na wana kampuni zao za uwakili na wanafanya kazi katika ngazi nyeti Serikalini wakiwemo Majaji, Mabalozi, Wabunge/Mawaziri, Watendaji wakuu wa Tasisi nyeti kwa mfano:

  1. EDWARD GAMAYA HOSEAH (Mkurugenzi Mkuu Takukuru)
  2. JOHNSON PAUL MATHIAS MWANYIKA (Mwansheria Mkuu Mtaafu)
  3. ABRAHAM HAMZA SENGUJI (Mkurugenzi – AG)
  4. JOHN BILLY TENDWA (Msajili wa Vyama Vya Siasa)

  Tazama hapa kwa orodha ya mawakili wa kujitegemea ambao wengi wapo serikalini mpaka sasa: http://www.tls.or.tz/pdf/rolls.pdf

  Ikiwa tayari wapo wanasheria huko Serikalini ambao waliaishwa kuwa mawakili wa Kujitegemea nab ado wanaendelea kutumikia umma kwa nyazifa zao, kisheria kitendo cha kuzuia wangine kuapishwa ni sawa na kuwaonea kwani kuapishwa hakumaanisha kukufanya mwanasheria ufanye kazi ya uwakili ikiwa hutakuwa na cheti cha kufanyia kazi (Practicing Certificate) \m\bcho kinatoloewa kwa mujibu wa Sheria ya Mawakili http://www.tls.or.tz/pdf/Advocatesact.pdf

  Ikumbukwe kuwa pia, wapo wanasheria mawakili ambao pengine huzuiliwa kufanya kazi hiyo kwa kunyimwa "practising certificate" labda kutokana na ukiukwaji wa maadaili ya uwakili. Hivyo, pamoja na kuwa wameapishwa bado hawawezi kufanya biashara.

  Kwa kuwa hakuna sheria iliyoweka wazi uwezo wa Mwanasheria Mkuu kuzuia mwansheria ambaye hayupo chini ya ofisi yake au usimamizi kuapishwa, itakuwa ni sawa na kuwanyima haki wanasheria wale wanaozuiwa.

  Ni mwema Mwanasheria Mkuu akajifunza kutoka kwa nchi nyingine ambapo mfumo unasimamiwa kwa kujenga na kudumishwa umoja miongoni mwa wanataaluma na sio kuonena husuda, chuki na kukomoana pale wengine wanapoendelea.
  Ni vizuri ikaeleweka pia kuwa suala la ukiukaji wa maadili na mgongano wa maslahi haliwezi kuzuiliwa kwa utaratibu huu kwani hata katika hali ya kawaida, mwanasheria wa Serikali ambaye si wakili wa kujitegemea anaweza pia kuuza kesi za Serikali kwa Kampuni binafsi za Uwakili ikiwa hana maadili katika kazi yake aliyoajiriwa.
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jan 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ngoshwe nashukuru sana kwa ufafanuzi wako!
  Ila kama utaweza naomba utuwekee soft copy zifuatazo:

  1. Kanuni za Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Tangazo la Serikali Na. 154 la Tarehe 3 Novemba, 2006).
  2. Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba 3 wa Mwaka 2007 uliotolewa tarehe 17 Septemba, 2007 na kuanza kutumika Julai, 2007

  Thanks in advance!
   
 9. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Oky mkuu
  Will get it soon
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jan 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Thanks in advance!
   
Loading...