Sakata la mauaji Uvinza, Kigoma: Zitto aanza kuibuka kidedea, Lugola amuagiza IGP kuwachukulia hatua vigogo wa Polisi mkoa na wilaya

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Hii ndio tweet ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani:

EB1EA151-806C-4000-8E8B-FC5A6E3DF9DC.jpeg

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amuagiza IGP Simon Sirro kuwaondoa kazini Kaimu Kamanda wa Polisi na Mkuu wa Operesheni mkoani Kigoma.

Waziri huyo pia ameagiza kuondolewa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Uvinza, Mkuu wa Intelijensia Wilaya na Askari wote wa kituo cha Polisi Mpeta na Nguruka.

Asema hayo leo Novemba 11 akiwa wilayani Uvinza mkoani humo zilipotokea vurugu baina ya Polisi na Wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na kusababisha vifo.

Mwishoni mwa Oktoba kuliliripotiwa mapigano katika wilaya hiyo ambayo chanzo chake kilielezwa ni mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.
 
Zitto aendelea kung'ara!!

Nasubiri kuona mwisho wa kesi waliomfungilia kama wataendelea nayo au wataifuta.

Siridhiki na maamuzi ya waziri kwani wahusika sidhani kama wanastahili kuondolewa katika nafasi zao na wa chini yao kuhamishwa bali wasimamishwe kazi kisha uchunguzi ufanyike na watakaobainika sheria ichukue mkondo wake vinginevyo kumshitaki Zitto ni kumuonea tu.
 
MsemajiMamboyaNdani
@ WizaraMNN 55m
#MAUAJI POLISI NA RAIA UVINZA: LUGOLA amemuagiza IGP awaondoe ktk nafasi zao Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma (wakati wa Opereshen), Mkuu wa Opereshen Mkoa, OCD Uvinza na Mkuu wa Intelijensia Wilaya. Pia ameagiza askari wote wa Kituo cha Polisi Mpeta na Nguruka wahamishwe.
Wewe jamaa huwa nakuhurumia sana aisee! Maana kila unachotamani hakitokei.

Sasa ushindi wa Zitto ni upi hapo? Maana Zito alisema wameuawa watu 100

Sasa hapo Lugola kakiri kwamba ni kweli waliuawa hao 100 ndio ushindi wa Zitto ama vipi?
 
Hii ndio tweet ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani:

MsemajiMamboyaNdani
@ WizaraMNN 55m
#MAUAJI POLISI NA RAIA UVINZA: LUGOLA amemuagiza IGP awaondoe ktk nafasi zao Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma (wakati wa Opereshen), Mkuu wa Opereshen Mkoa, OCD Uvinza na Mkuu wa Intelijensia Wilaya. Pia ameagiza askari wote wa Kituo cha Polisi Mpeta na Nguruka wahamishwe.
Kule Tarime mbona OCD alienda kuwapiga wananchi wachimbaji wadogo wadogo masikini wanyonge akawapora madini kisha kuwabambikia kesi mpaka leo yupo? au OCD wa Tarime ana Ubia na Lugola?
 
Hii ndio tweet ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani:

MsemajiMamboyaNdani
@ WizaraMNN 55m
#MAUAJI POLISI NA RAIA UVINZA: LUGOLA amemuagiza IGP awaondoe ktk nafasi zao Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma (wakati wa Opereshen), Mkuu wa Opereshen Mkoa, OCD Uvinza na Mkuu wa Intelijensia Wilaya. Pia ameagiza askari wote wa Kituo cha Polisi Mpeta na Nguruka wahamishwe.
Haitasaidia

Wataenda kufanya yale yale watakapopelekwa
 
Back
Top Bottom